Kenya: Rais Samia afungua kongamano la wafanyabiashara nchini Kenya, Rostam Aziz atema madini ukumbi mzima wamshangilia

Nina imani, nchi yetu ipo kwenye njia sahihi baada ya kupotezwa kwa miaka mitano.

Tukazanie kujenga mifumo itakayozuia Taifa kuangukia kwenye uongozi wa watu wasio na uwezo. Mifumo iwezeshe, akitokea kiongozi wa hovyo, kuwe na utaratibu rahisi wa kumwondoa.

Fikirieni miaka mitano tuliyokosa uongozi sahihi, hasara kubwa tuliyoipata kwa sekta mbalimbali. Na ikumbukwe kulikuwa na hatari ya nchi kuburutwa kwa miaka kumi, na pengine zaidi.
Kweli Mkuu Hamatan Mwendazake alikuwa anatupeleka shimoni. Ile ilikuwa ni ajali
 
Nimeingia kwenye hili bandiko kusoma cheche alizotema Rostam Azizi papa wa CCM. Lakini sijaona lolote, ni mbwembe tu za kumpampamba mtu
Shida ya Mtu Mweusi. Yaani ukimchukia Mtu utaona lolote analosema halina maana. Yaani hata Usikie akisema SHETANI M'BAYA wewe UTAMKOSOA
 
Hayati alijenga mazingira wezeshi ya ukuzaji wa biashara. Kufufua reli iliyokufa zaidi ya miaka 25 ni ujenzi wa mazingira ya usafirishaji ambayo ni nyenzo muhimu kibiashara.

Ufufuaji wa shirika la ndege ni urahisishaji wa biashara kimataifa. Kama sio corona muda huu Air Tanzania ingekuwa kila wiki inakwenda China na kurudi kupeleka matikiti. Kama sio corona muda huu biashara ya maua ya Arusha ingeitumia sana Air Tanzania kuyapeleka Amsterdam na kwingineko.

Hayati hakutaka dharau kama zile za kipindi kile mamlaka ya anga ya Kenya kuzuia ndege zetu kisa corona halafu kukubali ziingie kwao ndege za US na UK ambako ugonjwa ulikuwa umepamba moto. Dharau ile ilijibiwa vizuri sana na TCAA kwa kuzuia ndege zao zisiingie nchini.

Tufanye biashara pamoja kwa kila hali lakini tuheshimiane, tusileteane dharau za kutaka kuburuzana.
Mwendazake hakuwa na hekima kabisa, alitanguliza Sana kiburi na majivuno wakati hata biashara ya dunia haijui. Diplomasia inataka majadiliano na uvumilivu
 
Rais Samia amefungua kongamanano la wafanyabiashara nchini Kenya ambalo limehusisha pia wafanyabiashara kutoka Tanzania.

Rostam Aziz ametaka uwepo wa uwiano mzuri wa kibiashara kati ya Kenya na Tanzania badala ya nchi moja kuwa msambazaji wa mali ghafi na mwingine akiwa muuzaji wa finished goods, mmoja atafaidika na ajira kwa watu wake na upande mwingine ajira zitakosekana.

Tukio liko mubashara runinga ya Star.

Kazi Iendelee!
Leo Rostam unamfagilia kama Shujaa wa nchi vile!
Piti mambo yake huku jukwaani uone
 
Shida ya Mtu Mweusi. Yaani ukimchukia Mtu utaona lolote analosema halina maana. Yaani hata Usikie akisema SHETANI M'BAYA wewe UTAMKOSOA
Kwa nini anayekosoa anaonekana ana chuki? Yeye hajaona hoja yoyote, yupo sawa. Na wewe umeona Kuna hoja, upo sawa pia
 
Mwendazake hakuwa na hekima kabisa, alitanguliza Sana kiburi na majivuno wakati hata biashara ya dunia haijui. Diplomasia inataka majadiliano na uvumilivu
Hayati alikuwa na wasaidizi na hakutaka kunyanyasika. Ukinyanyasika kama rais wananyanyasika watu milioni 60 unaowaongoza.

Alikuwa binadamu lakini, upungufu wa hapa na pale haukosekani.
 
Hayati alijenga mazingira wezeshi ya ukuzaji wa biashara. Kufufua reli iliyokufa zaidi ya miaka 25 ni ujenzi wa mazingira ya usafirishaji ambayo ni nyenzo muhimu kibiashara.

Ufufuaji wa shirika la ndege ni urahisishaji wa biashara kimataifa. Kama sio corona muda huu Air Tanzania ingekuwa kila wiki inakwenda China na kurudi kupeleka matikiti. Kama sio corona muda huu biashara ya maua ya Arusha ingeitumia sana Air Tanzania kuyapeleka Amsterdam na kwingineko.

Hayati hakutaka dharau kama zile za kipindi kile mamlaka ya anga ya Kenya kuzuia ndege zetu kisa corona halafu kukubali ziingie kwao ndege za US na UK ambako ugonjwa ulikuwa umepamba moto. Dharau ile ilijibiwa vizuri sana na TCAA kwa kuzuia ndege zao zisiingie nchini.

Tufanye biashara pamoja kwa kila hali lakini tuheshimiane, tusileteane dharau za kutaka kuburuzana.
Reli ya SGR ambayo inaishia Mwanza badala ya Kigoma..hiyo ni akili au matope Ndugu?? Reli ikiishia Mwanza hatutaiona faida yake kwasababu mzigo mkubwa ni wa East Congo yaani Goma na Bukavu..na Burundi.ivyo ni lazima reli iishie Kigoma..hili hata watu wamelipigia kelele sana lakini Meko alikua haelewi..

ATCL ipi?? Hilo ni shirika la kutia nchi hasara tu.
Hakuna mtaalam hata mmoja wa anga katika bodi nzima ATCL..are we serious..??
Sihitaji kusema sana kuhusu ATCL maana CAG amemaliza kila kitu.
 
Haueleweki, Unaweza kuwa na hoja nzuri sana, ila unashindwa kuwakilisha hapa.
Rostam kasema tunahitaji uwekezeji uliosawa sio moja anauza raw na mwingine anazalisha bidhaa na ajira sasa hakuwa muwazi yupi anazalisha ajira zaidi. Nikanukuu kauli ya Rais kuwa Kenya wamewekeza makampuni karibia 500 Tanzania na kuzalisha ajira alfu 56 wakati huo Tanzania wamewekeza kampuni 30 Kenya na kuzalisha ajira alfu 2 ukitizama number tu unajuwa nani kafaidika na hizi ajira. ila nafasi ziko nyingi.
 
Kaharibu mno Uchumi wa Tanzania hasa hasa ( 2005 hadi 2015 ) kwa 'Usamjo Usamjo' wake akibebwa na Kushirikiana waliokuwa 'Maswahiba' wazuri wa Msoga na Monduli.

Naomba niishie hapa tafadhali nisije kusema mengineyo yasiyo na Faida sasa Kwako ( Kwenu ) kuyajua.

Akhsanteni.
Kuna mtu kamtukana Mtusi Kagame kwenye thead huko juu🤣
 
Reli ya SGR ambayo inaishia Mwanza badala ya Kigoma..hiyo ni akili au matope Ndugu?? Reli ikiishia Mwanza hatutaiona faida yake kwasababu mzigo mkubwa ni wa East Congo yaani Goma na Bukavu..na Burundi.ivyo ni lazima reli iishie Kigoma..hili hata watu wamelipigia kelele sana lakini Meko alikua haelewi..

ATCL ipi?? Hilo ni shirika la kutia nchi hasara tu.
Hakuna mtaalam hata mmoja wa anga katika bodi nzima ATCL..are we serious..??
Sihitaji kusema sana kuhusu ATCL maana CAG amemaliza kila kitu.
Huna uhakika kama SGR inaishia Mwanza na hujui kuwa kutakuwa na treni nyingine ya njia ya kuelekea mikoa ya kusini magharibi. Hujui ni ujazo mkubwa kiasi gani utakaotumia hiyo treni.

Masuala ya ATCL ndio kabisa ungekaa kimya kwani huwajui wataalam wanaoendesha shirika wanao uwezo mkubwa kiasi gani.

Ni shirika linaloendelea kupunguza ule ukubwa wa hasara iliyokuwepo likielekea katika miaka ya kuanza kupata faida.

Mawazo yako ni yale halisi hasi. Wapo wenye mawazo chanya na wanapoitazama Tanzania hawawezi kufikiria kushindwa tu.
 
Meko si alikua anakimbiza investors hapo Tz..
Sasa hizo processing industries zingejengwa na nani..??
Lile nyangumi bora halipo kabisa.
Bila ya kuvutia wawekezaji seriously tutaendelea kuuza raw materials tu.
Kabla ya Meko hali ilikuwaje?
Tuoneshe viwanda alivyoua meko ambavyo vilikuwa vinakula hizo raw materials alafu baada meko kuingia madarakni viwanda vikafa na raw materials zikaanza kwenda Kenya.

Hizi mimba alizowapa meko zitawatesa kwa miaka mingi kumbe?
 
Jackline Mkindi Hizi Figure za WATU BIL 2.5 Kwa East Africa come 2050 umezitoa wapi?? Hao watu Bil 2 nadhani umekosea you will need to make it clear once you have an opportunity.
 
Kabla ya Meko hali ilikuwaje?
Tuoneshe viwanda alivyoua meko ambavyo vilikuwa vinakula hizo raw materials alafu baada meko kuingia madarakni viwanda vikafa na raw materials zikaanza kwenda Kenya.

Hizi mimba alizowapa meko zitawatesa kwa miaka mingi kumbe?
Sawa DC Jojo tumekupata..
Pole kwa msiba..na Kubali tu he has gone and he has gone for good..
Hata kama mambo yalikua ya ovyo tangia huko nyumba lakini him was the worst..
Asante MUNGU kwa kusikia kilio cha watz.
 
Nina imani, nchi yetu ipo kwenye njia sahihi baada ya kupotezwa kwa miaka mitano.

Tukazanie kujenga mifumo itakayozuia Taifa kuangukia kwenye uongozi wa watu wasio na uwezo. Mifumo iwezeshe, akitokea kiongozi wa hovyo, kuwe na utaratibu rahisi wa kumwondoa.

Fikirieni miaka mitano tuliyokosa uongozi sahihi, hasara kubwa tuliyoipata kwa sekta mbalimbali. Na ikumbukwe kulikuwa na hatari ya nchi kuburutwa kwa miaka kumi, na pengine zaidi.

Magufuli amechukua nchi ikiwa na GDP gan na ameondoka ameacha tuna GDP ya ngap?
 
Sawa DC Jojo tumekupata..
Pole kwa msiba..na Kubali tu he has gone and he has gone for good..
Hata kama mambo yalikua ya ovyo tangia huko nyumba lakini him was the worst..
Asante MUNGU kwa kusikia kilio cha watz.
Sema kilio chenu nyie wajinga,!

Ufukara unaotafuna ukoo wako sio kwasababu ya meko.

Nmekuuliza nioneshe viwanda vilivyokufa baada ya yeye kuchukua madarakani badala yake unakuja na maneno ya kwenye kanga,,
 
Back
Top Bottom