Kenya: Rais na Makamu wanakinzana wanavumiliana, Tanzania Rais ni Bunge, Mahakama na Serikali

kifupi kirefu

JF-Expert Member
Oct 29, 2018
539
3,507
Tutazidi kusindikiza kwenye uchumi na kutengeneza wanafiki wa Taifa kupitia mfumo wa serikali tulioasisi awamu ya Tano. Yupo kiongozi wa Dini amediriki kutamka adharani kwamba tunakosa viongozi wenye maono, naomba niseme siyo wenye maono tu Bali wenye nguvu yakupanbana kwa hoja.

Kenya awapo vizuri Sana kisiasa kwa sababu ya ukabila I mfumo wao wa sheria upo strong enough kumdhibiti Rais na wapambe wake wasiwe mihimili. Lakini mfumo huo pia ndio umewafanya watu wengi kujiona wanafaa kuiongoza Tanzania.

Sasa hivi unaona wazi kwamba awamu ya sita haiwezi kuepuka makundi na mapambano ya kiongozi mmoja mmoja kuutaka urais means walioteuliwa kuwa viongozi na wafanyabiashara wanaamini Wana maono na nguvu kuliko mkuu wa nchi.

Tusipokubali kwamba tunataka maendeleo tukajikita kutengeneza harakati za urais ipo siku uchu utazidi na tutaingiza makundi ya Urais kwenye vyombo vya dola na hapo ndipo uzaliwa mapinduzi.

Ipo wazi kwamba hatuwezi kukua kwa aina hii ya siasa Hadi pale Rais atakapokubali na kutamka adharani kwamba mahakama anairuhusu iwe huru, Bunge analiruhusu liwe huru na serikali iwe huru. Kuendelea kufanya vyombo vyote hivi vitishwe na dola nakunyamazishwa na dola nikufanya nchi kuendelea kujenga bomu ambalo likilipuka si wastaafu Wala waliopo madarakani wataishi.
 
Back
Top Bottom