Kenya: Odinga apendekeza Serikali ya muda iundwe kama sehemu ya kutatua mzozo wa kisiasa

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,262
1e2963bdb051e3b981b2f8a32e995286.jpg
Kiongozi wa Upinzani nchini Kenya Raila Odinga amependekeza Serikali ya muda iundwe nchini humo na kutawala kwa muda wa miezi sita kama sehemu ya kutatua mzozo wa kisiasa nchini humo.

Bw. Odinga ambaye alisusia uchaguzi wa marudio uliofanyika mwezi uliopita, amesema katika kipindi hicho kunafaa kufanyika marekebisho ya Katiba kuchunguza upya mamlaka ya rais.

Kiongozi huyo ambaye ameanza ziara nchini Marekani alisema yuko tayari kufanya mazungumzo na Rais Uhuru Kenyatta kuhusu marekebisho ya kikatiba ambayo anasema yanahitajika kupunguza hatari ya kuzuka kwa fujo kutoka kwa makundi ya jamii za wachache ambao wanajiona kwamba wametengwa.

Rais Kenyatta alitangazwa mshindi wa uchaguzi huo wa marudio uliofanyika tarehe 26 Oktoba akiwa na kura 7.5 milioni ambazo ni sawa na asilimia 98 ya kura zilizopigwa.

Waliojitokeza kushiriki uchaguzi huo ni asilimia 39 ya waliojiandikisha kuwa wapiga kura nchini humo.

Uchaguzi huo ulitokana na hatua ya Mahakama ya Juu, kufuatia kesi iliyowasilishwa na Bw. Odinga, kubatilisha matokeo ya uchaguzi wa Agosti 8 ambapo Bw. Kenyatta alikuwa ametangazwa mshindi kwa asilimia 54 ya kura.

Mahakama ya Juu ilisema uchaguzi huo wa mwanzo ulikumbwa na kasoro nyingi.

Bw. Odinga alisusia uchaguzi wa marudio akisisitiza lazima mageuzi yafanywe katika Tume ya Uchaguzi IEBC.

Chanzo: BBC
 
Atapewa tu maaana amewashika vibaya sana Rais Uhuru na serikali yake.

Ni lazima wafanye juhudi za kumpooza.
 
Kumbeeeeee ndio mana hata mwaka 2007 alisababisha wenzake wakafaa kwa sababu ya uwazir Mkuu na akaupta sasa

2017 asipo angalia atakufa yeye
Mijitu mingine bwana sijui ilizaliwaga ili iweje

Hujui hata unachokisema!!
 
Kumbeeeeee ndio mana hata mwaka 2007 alisababisha wenzake wakafaa kwa sababu ya uwazir Mkuu na akaupta sasa

2017 asipo angalia atakufa yeye
Mijitu mingine bwana sijui ilizaliwaga ili iweje
Alishinda uchaguzi 2007 bila chembe ya walakini
 
Kumbeeeeee ndio mana hata mwaka 2007 alisababisha wenzake wakafaa kwa sababu ya uwazir Mkuu na akaupta sasa

2017 asipo angalia atakufa yeye
Mijitu mingine bwana sijui ilizaliwaga ili iweje
Yaan huyu hii ndio ilikua nia yake sijui mkenya gan yule.
 
Kiongozi wa Upinzani nchini Kenya Raila Odinga amependekeza Serikali ya muda iundwe nchini humo na kutawala kwa muda wa miezi sita kama sehemu ya kutatua mzozo wa kisiasa nchini humo.

Miezi sita siyo mingi kurekebisha kila kitu. Baada ya hapo kuwe na uchaguzi ambao utakuwa free, fair and transparency and whatever the outcome everybody should respect it. It is better option than four years of complete division, boycotts, civil disobedience and paralysis.
 
Back
Top Bottom