Kenya nje, Uganda yashikwa

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,072
1,250
MABAO mawili ya mchezaji wa Ethiopia, Shemelles Godo katika kipindi cha kwanza yalitosha kuifungasha Kenya virago kwenye michuano ya Tusker Chalenji baada ya kukubali kipigo cha mabao 2-1, huku mabingwa wa mtetezi Uganda akilazimika kutumia nguzu za ziada kupata sare ya 1-1 na Malawi michezo iliyochezwa jana kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Shemelles alifunga bao lake la kwanza kwa mpira wa adhabu dakika ya 24 uliokwenda moja kwa moja wavuni na kumwacha kipa wa Kenya asijue la kufanya, Godo aliongeza bao la pili dakika moja kabla ya mapumziko kwa kuunganisha kwa ustadi pasi ya Omond Okwury aliyeipangua ngome ya Harambee Stars na kumwachia mfungaji aliyempelea pembeni kipa.

Kenya ambayo iliingia kwenye mchezo huo ikiwa na matumaini ya kujirekebisha baada ya kipigo cha kwanza kutoka kwa Malawi ya cha mabao 3-2, waliamka katika kipindi cha pili na kufanya mashambulizi mengi kwa Ethiopia na kufanikiwa kupata bao lao kufutia machozi kupitia kwa Fred Ajwang aliyeunganisha krosi ya Bob Mugalia dakika ya 84.

Mapema mabingwa watetezi Uganda iliwabadi kusubili hadi dakika ya 76, kupata bao la kusawazisha kupitia kwa mshambuliaji wa Simba, Emmanuel Okwi kupata sare ya 1-1 dhidi ya Malawi.

Malawi ambao katika mchezo wa kwanza walichapa Kenya 3-2, walianza mchezo huo kwa kasi na kufanikiwa kupata bao la kuongoza dakika ya 2, kupitia Victor Nyirenda.

Naye Clara Alponce anaripokuwa rais wa Cecafa, Leodegar Tenga amefurahishwa na kitendo cha mashabiki wengi kujitokeza uwanjani hapo na kuzishangilia timu zao.

Alisema kitendo hicho kimeongeza hamasa ya mashindano hayo na kuwataka waendelea kujitokeza kwa wingi zaidi hadi Jumapili kwakuwa hakutokuwa na viingilio.

"Tuneondoa viingilio hadi mechi za Jumapili tofauti na awali tuvyosema mwisho kesho (leo) baada ya hapo mechi za mtoano zitakuwa na viingilio cha juu kitakuwa elfu 10000 na 3000.
xxxxxxxxxxx
Uwanja wa Taifa, Uhuru
Imani Makongoro
HATIMAYE Uwanja wa Taifa na ule wa Uhuru umepata wasimamizi baada ya Serikali kumtangaza Rishiankira Urio na Josephine John kuwa wasimamizi wa viwanja hivyo.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Sethi Kamuhanda, alisema kuwa serikali imemteua Urio kuwa msimamizi wa Uwanja wa taifa tangu Novemba 11 wakati shughuli ya kumpata mwendeshaji wa uwanja huo ikiendelea.

Mbali na Urio, Kamuhanda alisema kuwa Josephine amechaghuliwa kuwa meneja wa Uwanja wa Uhuru baada ya aliyekuwa meneja wake Charles Masanja kufariki Dunia mwaka jana.

"Kabla ya uteuzi huo John alikuwa Afisa Michezo mkuu, Idara ya Maendeleo ya Michezo, Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo hivyo atasimamia shughuli zote za uwanja huo.

"Urio ni Afisa Mwandamizi wa Ugavi na ununuzi Wizarani, pia ni Mratibu wa ujenzi wa eneo la Changamani la michezo la taifa (National Sports Complex) hivyo amepewa jukumu la kusimamia uwanja huo hadi pale tutakapompata mwendeshaji wa uwanja huo," alisema Kamuhanda.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom