Kenya Ni Vema Mkaondoa Vikosi Somalia

ibanezafrica

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
7,261
6,543
Ndio uamuzi bora na pekee kupelekea taifa lenu kuishi kwa amani,ni bora mkalinde amani mipakani kuliko kuingia ndani ya ardhi ya Somalia na kupambana na Magaidi

Hakika vita ya namna hii haina ushindi kwenu kama taifa zaidi ya majuto...tukumbuke taifa kubwa LA marekani walipoona mambo yamewawia vigumu somalia walifungasha virago na kurudisha majeshi nyumbani!sembuse nyie?

Sababu za kisiasa zisiwafanye wakenya mzidi kupoteza damu za RAIA wasio hatia miaka nenda rudi,hili sasa lifikie mwisho!
Ni sawa na MTU timamu unarushiana mawe na mwendawazimu ili hali umo ndani ya nyumba ya vioo!

Poleni sana jirani na hasa wale waliopoteza wapendwa wao katika shambulio hili

Mwenyezi mungu awalaze pema peponi marehemu wote walohusika na shambulizi hizi.

Pole sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndio uamuzi bora na pekee kupelekea taifa lenu kuishi kwa amani,ni bora mkalinde amani mipakani kuliko kuingia ndani ya ardhi ya Somalia na kupambana na Magaidi,
Hakika vita ya namna hii haina ushindi kwenu kama taifa zaidi ya majuto...tukumbuke taifa kubwa LA marekani walipoona mambo yamewawia vigumu somalia walifungasha virago na kurudisha majeshi nyumbani!sembuse nyie?
Sababu za kisiasa zisiwafanye wakenya mzidi kupoteza damu za RAIA wasio hatia miaka nenda rudi,hili sasa lifikie mwisho!
Ni sawa na MTU timamu unarushiana mawe na mwendawazimu ili hali umo ndani ya nyumba ya vioo!
Poleni sana jirani na hasa wale waliopoteza wapendwa wao katika shambulio hili
Mwenyezi mungu awalaze pema peponi marehemu wote walohusika na shambulizi hizi.
Pole sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
Revisit your opinion
 
Wewe huna akili kabisa yawezekana hujui lengo la hao magaidi. Hata wakiondoa majeshi kule usidhani kuwa ndio wataacha kufanya ugaidi, ndio watazidisha kwani watapata muda wa kujipanga na kutekeleza lengo lao ambalo ni kuunda DAESH yaani kufuta mifumo yoote ya utawala wa kidemokrasia na kuleta mfumo na mafundisho yao ikiwa ni sambamba na kuwafyekelea mbali wale wote wanaoamini na kutenda kinyume nao. Ninaipongeza serikali ya kenya na inahitaji kuungwa mkono na jumuia ya kimataifa kuwamaliza hao nyangau huko misituni.
 
"Wew huna akili kabisa" Mbona lugha kali sana?

Kwani haiwezekaniki kukosoa bila kumdunisha (Undermine) mchangiaji.?

Ukichangia kwa kumdunisha mtu unakuwa unafanya kitu kinaitwa "Hoja ya nguvu". Mtu anayejenga hoja za kushawishi anakuwa anafanya kitu kinaitwa "Nguvu ya hoja" na ndo inayotakiwa katika majadiliano.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Maswali kuhusu kushambuliwa kwa Kenya na uwepo wa vikosi vyake nchini Somalia.

Kikosi cha kulinda amani nchini Somalia (AMISOM) kinaundwa na wanajeshi kutoka; Kenya, Burundi, Uganda, Djibout na Ethiopia.

Sasa, kama hoja ni vikosi vya Kenya kuwepo Somalia, mbona kuna vikosi kutoka nchi nyingine pia?

Mbona, hao magaidi hawaendi kushambulia Burundi au Ethiopia mana vikosi vyao vimo Somalia pia?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kenya inaponzwa na wasomalia wanye uraia wa nchi hiyo kwani wanakua kama kichaka cha waovu kujificha na kupanga mashambulizi.
Dawa ni kuhakikisha hakuna msomalia mgeni anayeingia Kenya na akitoka hakuna kurudi.
Wasomalia ni watu katili sana.

Wanasikika wakisema watafika mpaka Zanzibar.
Na wanaonekana wanazungumzia suala la Himaya ya Dola la kiislam wakati wa Utumwa.
Dunia imebadilika masuala ya Himaya za kizamani zinawakosti tu.

Hata Hivyo wana wananchi wanaowaunga mkono.
Kujifichi kwenye nchi ndogo kama Kenya yenye mapori machache ni jambo gumu kama hakuna watu wanaojua na kuficha.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wewe huna akili kabisa yawezekana hujui lengo la hao magaidi. Hata wakiondoa majeshi kule usidhani kuwa ndio wataacha kufanya ugaidi, ndio watazidisha kwani watapata muda wa kujipanga na kutekeleza lengo lao ambalo ni kuunda DAESH yaani kufuta mifumo yoote ya utawala wa kidemokrasia na kuleta mfumo na mafundisho yao ikiwa ni sambamba na kuwafyekelea mbali wale wote wanaoamini na kutenda kinyume nao. Ninaipongeza serikali ya kenya na inahitaji kuungwa mkono na jumuia ya kimataifa kuwamaliza hao nyangau huko misituni.
Kaka vita hii ni ngumu sana,kumbuka Luna wakenya wengi wrnye asili ya kisomali wanaishi ndani ya Kenya na wengi wao ndugu zao au family zingali zipo huko somalia
Wamechanganyika mno
Otherwise uniambie Kenya iitawale somalia yote kama nchi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Maswali kuhusu kushambuliwa kwa Kenya na uwepo wa vikosi vyake nchini Somalia.

Kikosi cha kulinda amani nchini Somalia (AMISOM) kinaundwa na wanajeshi kutoka; Kenya, Burundi, Uganda, Djibout na Ethiopia.

Sasa, kama hoja ni vikosi vya Kenya kuwepo Somalia, mbona kuna vikosi kutoka nchi nyingine pia?

Mbona, hao magaidi hawaendi kushambulia Burundi au Ethiopia mana vikosi vyao vimo Somalia pia?

Sent using Jamii Forums mobile app
Nadhani Uganda,Burundi zilisha shambuliwa na sikumbuki Luna nchi walisha withdraw majeshi yao
Hivyo hawa magaidi nao wanaangalia influence ya jeshi husika na wanajibu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jana hoja hiyo ilikua inafanyiwa uchambuzi radio DW na mchambuzi mmoja toka Mombasa amemlaani waziwazi rais mwai kibaki kwa uamuzi wa kupeleka vikosi somalia na kumsema kua uamuzi wake haukuridhiwa na bunge LA kenya tangu mwanzo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nchi zingine za AMISOM zimepeleka majèshi yake kulinda amani lakini hawa jirani wameamua kuiba na kubaka na maumivu mengi, wameshambulia watu kwa ndege na kuuwa innocent people wakiwemo watoto na wazee
Je unategemea watawaacha bila visasi?

Tunayasoma mengi na wao wakitamba kuwa wameuwa wangapi na wao wamepoteza wangapi
Lakini hiyo haitaleta amani hata siku moja ila machafuko tu na watu kukosa amani ya kuishi na kufanya shughuli zao za kila siku.

Wachague kusuka au kunyoa ni maamuzi yao ila pia sisi hatufurahii majirani wakiwindana hivi.
Maana hii sio vita tena bali kuliana timing tu

Sent from my SM using Tapatalk
 
sijui kama itasaidia wengine hawahitaji reason kuua, mnaweza mka pull out na bado mkashambuliwa kwa vile babu zenu walikanyaga Ardhi yao
Siyo hivyo tu !! Kumbuka ni Al shabaab waliokuwa wa kwanza kuteka watalii toka Kenya . Na hii ni hata kabla majeshi ya Kenya hayajaenda Somalia.

Kinachowasumbua Kenya ni kuwa karibu 20% ya raia wake ni wa Somali wa North Kenya . Na hawa wanawaona wenzao wa Somalia ni ndugu kwao zaidi ya wabantu wenzao wa Kenya . Na hili liko ki imani zaidi. Na ni kwa njia hiyo adui hukaribishwa zaidi, na wakati mwingine hutumia waSomali wa Kenya kufanya mashambulizi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Maswali kuhusu kushambuliwa kwa Kenya na uwepo wa vikosi vyake nchini Somalia.

Kikosi cha kulinda amani nchini Somalia (AMISOM) kinaundwa na wanajeshi kutoka; Kenya, Burundi, Uganda, Djibout na Ethiopia.

Sasa, kama hoja ni vikosi vya Kenya kuwepo Somalia, mbona kuna vikosi kutoka nchi nyingine pia?

Mbona, hao magaidi hawaendi kushambulia Burundi au Ethiopia mana vikosi vyao vimo Somalia pia?

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu unachanganya hapa. Kenya walienda kivyao baada ya Al Shabaab kuua watu kule Mombasa na Lamu waliposhambulia hotel. Kenya waanza operation kule kivyao. Walipeleka askari na ndege
 
Sikumbuki na wala sitakiwi kubisha kuwa Kenya walienda kivyao.

Je, baada ya Kenya kufika huko hawakujumuishwa ndani ya AMISOM?

Nashauri, tuwe tunajaribu kufanya utafiti.

Mimi nimezitaja nchi zinazochangia vikosi baada ya kupitia kwenye tovuti ya AMISOM, na Kenya imo. Sasa naona nimedanganywa. Au hii tovuti haiko updated.

Pitia tovuti hii ya AMISOM; AMISOM

Chini kabisa utaona vikosi, naambatanisha na screenshot;
Screenshot_20190120-121955.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom