Kenya nako ni kama Tanzania , mgomo wa madaktari waendelea

GeniusBrain

JF-Expert Member
Nov 3, 2010
4,315
306
Katika kile kinacho jionyesha kwamba madaktari wa nchi za Afrika Mashariki wamedhamiria kuteketeza maisha na roho za wananchi. Nchi jirani ya Kenya napo mgomo wa madaktari uliodumu takriban kwa wiki sasa unaendelea. Na waziri wa Afya wa Kenya Prof. Anyang’nyo amewatishia madaktari kuwafukuka kazi endapo leo wasipo ripoti vituo vyao vya kazi. Je hii ni kusema ni migomo ya madaktari ni vuguvugu lakuonyesha mshikamano wao? Sources: -KBC -ITV Habari saa 2 usiku tarehe 06.03.2012
 
Ila hawa wa Kenya wako organised and focused.Siyo hapa kwetu ambapo pametawaliwa na ubazazi wa Ulimboka na Bisimba
 
Hebu fafanua tukuelewe, kwani umetuacha kidogo mkuu


Madaktar wa Tanzania wametawaliwa na ufinyu wa mawazo kwa kuwa wanayoyataka kuwa Waziri na naibu waziri wajiuzulu hayaongezi masilahi ya kada yao. Basically wako myopic
 
Madaktar wa Tanzania wametawaliwa na ufinyu wa mawazo kwa kuwa wanayoyataka kuwa Waziri na naibu waziri wajiuzulu hayaongezi masilahi ya kada yao. Basically wako myopic

Hapo sasa nimekuelewa. Sasa kwa hili tufanyeje ?

 
Back
Top Bottom