Kenya na tume yao huru bado malalamiko ni mengi, sisi tuna tofauti gani na wao?.

Huna cha kunielewesha, kwa sababu nimeulizia masuala kama vile ushindi halali wa Esther Bulaya na namna ambavyo mzee Wassira anashindwa kila anapokata rufaa.

Huna cha kunielewesha kwa sababu ninaongelea namna ambavyo mzee ENL alivyokwenda CHADEMA na kukipatia chama yale majimbo ya kaskazini, kupitia matokeo yaliyotangazwa na tume hii hii ya uchaguzi tuliyonayo.
Kwa hiyo ili ukiri kuna mapungufu kwenye hii tume ya CCM ya uchaguzi ulitaka wapinzani wasipate hata kiti kimoja cha ubunge? Kwamba kama ingekuwa kweli tume haiko huru CCM ilitakiwa ishinde kwa aslilimia 100%! Ndivyo akili zako zinavyokutuma siyo? Well, nilijua napoteza muda wangu, endelea kuamini hivyo hivyo.
 
Kwa hiyo ili ukiri kuna mapungufu kwenye hii tume ya CCM ya uchaguzi ulitaka wapinzani wasipate hata kiti kimoja cha ubunge? Kwamba kama ingekuwa kweli tume haiko huru CCM ilitakiwa ishinde kwa aslilimia 100%! Ndivyo akili zako zinavyokutuma siyo? Well, nilijua napoteza muda wangu, endelea kuamini hivyo hivyo.
Ni kwamba kilicho muhimu ni mwananchi kuridhishwa na sifa anazotaka kuziona kwa anayempigia kura.

Haya mengine ya tume huru au sio huru ni mbwembwe za kutafutia sababu ya kuhalalisha kushindwa.

Kupoteza muda wako au kutopoteza ni tatizo lako binafsi, maadam unachangia mada basi tegemea maoni tofauti na ya kwako.
 
Huko Zanzibar enzi za SUKI (Serikali ya Umoja wa Kitaifa) walienda mbali zaidi ya Kenya na kuunda hiyo waliyofikiri itakuwa tume huru ya uchaguzi. Wajumbe wa tume hiyo nusu wakatoka chama tawala na nusu wakatoka chama kikuu cha upinzani. Kilichotokea kila mtu alikishuhudia. Wajumbe wa tume walitwangana ngumi, wakachaniana mashati, komputa zikavunjwa na hatimaye mwenyekiti wa tume hiyo ambaye kwa muundo wa tume ni wa kutoka chama tawala, akayafuta (deleted) matokeo yote ya uchaguzi na nyaraka zake zote kwenye electronic election system! Kama si kwa uimara wa majeshi yetu damu ingemwagika. Pamoja na Seif kwenda kulalamika kila mahali, walimuona ni zezeta kwani naye alikuwa part ya tume hiyo ya uchaguzi kwani nusu ya wajumbe wa tume hiyo walikuwa ni wa kwake wakitekeleza maagizo yake kwenye tume hiyo!

Hakuna kitu kama tume huru duniani kote. Ni kujidanganya tu. Juzi juzi tu tumeshuhudia huko Marekani Hillary Clinton akiilalamikia tume kumpokonya ushindi. Vurugu nyingi zikatokea katika mitaa mingi ya Marekani zilizodumu kwa miezi kadhaa na kupelekea baadhi ya watu kupoteza maisha. Manual recounting kwenye baadhi ya majimbo zikafanyika nk nk.

Cha muhimu ni transparency of the election process katika hatua zote na si kutegemea sana muundo wa tume inayosimamia uchaguzi. Transparency ambayo itamuwezesha kila mdau kuona dosari zitakazojitokeza kwenye process hiyo ya uchaguzi. Dosari ndogo ndogo hazikwepeki. Kama mdau ataona kuwa dosari hizo ni kubwa kwa kiwango cha kumnyima ushindi basi milango ya mahakama iwe wazi kwake kwenda kutoa hizo duku duku zake.

Hivyo tume yetu ya uchaguzi na election process transparency is one of the best in Africa kwa sasa. Wakati ukifika when we are mature enough na kuacha kupinga kila kitu, milango ya mahakama kutoa duku duku za matokeo ya uchaguzi wa rais, nayo itafunguliwa.

Katiba ya nchi ni mwongozo wa sheria za uendeshaji wa nchi tunazotunga. Zinazotekelezwa ni sheria zilizotungwa kwa kufuta mwongozo huo wa katiba. Katiba tuliyonayo ni nzuri sana na haijawa hata siku moja kuwa kikwazo cha kutuzuia kutunga sheria ye yote nzuri. Katiba yetu imetoa fursa ya kubadili au kuongeza kipengele cho chote kwenye katiba hiyo ambacho tunaona kinakwaza sheria fulani kutungwa. Hivyo tunao uwezo kwa mfano wa kutunga sheria ya kupinga matokeo ya urais mahakamani muda mwafaka utakapowadia. Hatuna sababu ya ku overhaul katiba yote kwa kutunga katiba mpya ambayo utekelezaji wake utatutaka kutunga upya sheria zote za nchi hii.
 
Back
Top Bottom