Kenya na tume yao huru bado malalamiko ni mengi, sisi tuna tofauti gani na wao?.

Phillipo Bukililo

JF-Expert Member
Dec 29, 2015
13,352
2,000
Baada ya uchaguzi wa Kenya kumalizika, kama kawaida ya tamaduni za chaguzi za kiafrika, yamesikika malalamiko mengi.

Raila Odinga na kambi yake wamelalamika vya kutosha, wamelalamikia rafu za chini chini zilizompatia Uhuru Kenyatta nafasi ya kuendelea kubakia ikulu.

Ni wakenya hawa hawa waliobadilisha katiba yao na kubariki uwepo wa tume huru ya uchaguzi. Tofauti na malalamiko ya wapiga kura wa Tanzania wanaotaka kuwepo kwa tume huru ya uchaguzi.

Lakini pamoja na uwepo wa tume hiyo, bado inaonekana sio muarobaini wa kuondoa kabisa na malalamiko ya kisiasa. Bado ni kama vile serikali inayoingia kwenye uchaguzi inakuwa na ushawishi wa ziada wakati wa uchaguzi.

Tanzania inalilia katiba mpya ambayo mapendekezo yake yatakuwa ndio msingi wa kuzaliwa kwa tume huru ya uchaguzi. Kwa uzoefu wa uchaguzi wa Kenya wa mwaka huu, nadhani hata tutakapokuwa na tume huru, vilio vya kuibiwa kura vitakuwa pale pale.

La muhimu kwa wanasiasa wetu wa siku zijazo, ni kutomuangalia yule mtu anayekusikiliza siku za kampeni akiwa yupo hoi kimaisha, halafu ukajidanganya kwa kudhani kuwa hata kiakili yupo hoi.

La muhimu ni kutoushusha thamani uwezo wa mpiga kura katika kumchambua mwanasiasa anayemsikiliza jukwaani.

Tume inaweza kuwa huru na isiwe huru kwa uwezo wa mtu mmoja mmoja katika kuifanyia uchambuzi wa kina, lakini mpiga kura ndiye mfalme. Haya maneno ya kwamba eti tumeibiwa kura yanaweza yasiwe na msaada sana kwa mpiga kura.

Uchaguzi wa Kenya haswa kwa maana ya uwepo wa tume huru, ni funzo kwa wanasiasa wetu, ambao huishi kwa kuuamini ule msemo usemao kuwa mbazi ikinyauka husingizia jua.
 
Babati

JF-Expert Member
Aug 7, 2014
38,329
2,000
Tofauti ni kubwa sana. Tume huru ya Kenya imesikiliza malalamiko ya vyama na kuyafanyia kazi tofauti na sisi 2015. Pili Tume huru ya Kenya haiwajibiki kwa mtu ye yote tofauti na Tume ya Tanzania inawajibika kwa Raisi. Kama mtu haoni tofauti kati ya Tume ya Kenya na ile yetu (TZ) basi huyu Hayuko Sawa.

Sent using Jamii Forums mobile app
CCM toka lini wakawa na ubongo kamili?
 
Phillipo Bukililo

JF-Expert Member
Dec 29, 2015
13,352
2,000
Tofauti ni kubwa sana. Tume huru ya Kenya imesikiliza malalamiko ya vyama na kuyafanyia kazi tofauti na sisi 2015. Pili Tume huru ya Kenya haiwajibiki kwa mtu ye yote tofauti na Tume ya Tanzania inawajibika kwa Raisi. Kama mtu haoni tofauti kati ya Tume ya Kenya na ile yetu (TZ) basi huyu Hayuko Sawa.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kinachoongelewa kwa undani kwa sio taratibu za ndani za namna tume hizo zinavyofanya kazi. Ujumba wa mada unawahusu hao wanasiasa, ambao kwao kutafuta wa kumnyooshea kidole ni jambo la kawaida.

Wanapaswa kujifunza siasa kwa maana ya kutambua heshima ya mpiga kura kwanza, tume yetu inaweza kubadilishwa na ikafanana na hiyo ya Kenya kimuundo na kimamlaka lakini kama mwanasiasa wa nchi hii asipotambua deni lake kwa mwananchi anayempigia kura na akaanza kumheshimu basi tume hiyo huru itageuka sehemu ya lawama.
 
nkese

JF-Expert Member
Mar 8, 2017
2,875
2,000
Tume yetu haina chembe ya uhuru,uthubutu wala utashi wa kutenda haki kwa wadau wengine tofauti n.a. ccm-dola.

Jiulize uhesabuji wa kura umekamilika leo matokeo ya Jimbo tu hadi siku 3! Pia malalamiko yakitolewa yanavyoshughulikiwa ni tofauti sana. Ya kwetu ni aibu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Retired

JF-Expert Member
Jul 22, 2016
26,180
2,000
Baada ya uchaguzi wa Kenya kumalizika, kama kawaida ya tamaduni za chaguzi za kiafrika, yamesikika malalamiko mengi.

Raila Odinga na kambi yake wamelalamika vya kutosha, wamelalamikia rafu za chini chini zilizompatia Uhuru Kenyatta nafasi ya kuendelea kubakia ikulu.

Ni wakenya hawa hawa waliobadilisha katiba yao na kubariki uwepo wa tume huru ya uchaguzi. Tofauti na malalamiko ya wapiga kura wa Tanzania wanaotaka kuwepo kwa tume huru ya uchaguzi.

Lakini pamoja na uwepo wa tume hiyo, bado inaonekana sio muarobaini wa kuondoa kabisa na malalamiko ya kisiasa. Bado ni kama vile serikali inayoingia kwenye uchaguzi inakuwa na ushawishi wa ziada wakati wa uchaguzi.

Tanzania inalilia katiba mpya ambayo mapendekezo yake yatakuwa ndio msingi wa kuzaliwa kwa tume huru ya uchaguzi. Kwa uzoefu wa uchaguzi wa Kenya wa mwaka huu, nadhani hata tutakapokuwa na tume huru, vilio vya kuibiwa kura vitakuwa pale pale.

La muhimu kwa wanasiasa wetu wa siku zijazo, ni kutomuangalia yule mtu anayekusikiliza siku za kampeni akiwa yupo hoi kimaisha, halafu ukajidanganya kwa kudhani kuwa hata kiakili yupo hoi.

La muhimu ni kutoushusha thamani uwezo wa mpiga kura katika kumchambua mwanasiasa anayemsikiliza jukwaani.

Tume inaweza kuwa huru na isiwe huru kwa uwezo wa mtu mmoja mmoja katika kuifanyia uchambuzi wa kina, lakini mpiga kura ndiye mfalme. Haya maneno ya kwamba eti tumeibiwa kura yanaweza yasiwe na msaada sana kwa mpiga kura.

Uchaguzi wa Kenya haswa kwa maana ya uwepo wa tume huru, ni funzo kwa wanasiasa wetu, ambao huishi kwa kuuamini ule msemo usemao kuwa mbazi ikinyauka husingizia jua.
Malalamiko ya Raila not justified. The whole world witnessed the election process! Raila alitaka chochote alichodai alipewa. Jana kasema turudie kuhesabu 34A and 35B ikafanyika, what else then?
 
MISULI

JF-Expert Member
Jan 15, 2014
7,359
2,000
Hawa wanaopongeza tume huru na uchaguz kwenda vizuri huko Kenya mbona sioni wakizungumzia mtaalam wa mifumo ya kompyuta kuawa?Au uhuru wa tume ni pale walipokuwa wanamuunga mkono UK kushinda?

posti fromu Nokia kitochi yuzingi jamii forum
 
Phillipo Bukililo

JF-Expert Member
Dec 29, 2015
13,352
2,000
Hawa wanaopongeza tume huru na uchaguz kwenda vizuri huko Kenya mbona sioni wakizungumzia mtaalam wa mifumo ya kompyuta kuawa?Au uhuru wa tume ni pale walipokuwa wanamuunga mkono UK kushinda?

posti fromu Nokia kitochi yuzingi jamii forum
Kaka wa watu kauwawa siku chache kabla ya uchaguzi!!. Siasa safi kabisa labda zipo katika huo ulimwengu mwingine baada ya maisha haya.
 
Mag3

JF-Expert Member
May 31, 2008
11,673
2,000
Hayo majimbo yote ambayo vyama vingine vinashinda isipokuwa CCM, tume inayokubaliana na matokeo ni hii hii ya sasa au kuna tume nyingine?.
Hata nchini Korea Kaskazini ambapo kumkataa mnyoa kiduku lazima upige kura hadharani watu wake wakishuhudia bado hakuweza kupata asilimia 100%. Hata saa mbovu kuna wakati inaonesha muda wa kweli. Hata kichaa kuna wakati anapata akili kidogo. Hata kwa madikteta uchwara kuna wananchi wenye ujasiri wa kumwambia hapana kama Ben Saanane ingawa anajua atapotezwa. Hata hivyo nadhani napoteza muda wangu kujaribu kukuelewesha.
 
Phillipo Bukililo

JF-Expert Member
Dec 29, 2015
13,352
2,000
Hata nchini Korea Kaskazini ambapo kumkataa mnyoa kiduku lazima upige kura hadharani watu wake wakishuhudia bado hakuweza kupata asilimia 100%. Hata saa mbovu kuna wakati inaonesha muda wa kweli. Hata kichaa kuna wakati anapata akili kidogo. Hata kwa madikteta uchwara kuna wananchi wenye ujasiri wa kumwambia hapana kama Ben Saanane ingawa anajua atapotezwa. Hata hivyo nadhani napoteza muda wangu kujaribu kukuelewesha.
Huna cha kunielewesha, kwa sababu nimeulizia masuala kama vile ushindi halali wa Esther Bulaya na namna ambavyo mzee Wassira anashindwa kila anapokata rufaa.

Huna cha kunielewesha kwa sababu ninaongelea namna ambavyo mzee ENL alivyokwenda CHADEMA na kukipatia chama yale majimbo ya kaskazini, kupitia matokeo yaliyotangazwa na tume hii hii ya uchaguzi tuliyonayo.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom