Kenya na Somalia zabadilishana watuhumiwa ugaidi

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,498
9,279
Polisi wa Somalia wamewakabidhi watuhumiwa wawili wa ugaidi wa Kundi la Al-Shabaab kwa polisi wa Kenya, ikiwa ni sehemu ya juhudi za pamoja za kuzuia mashambulizi ya kuvuka mipaka.

Kamanda wa polisi wa mkoa wa Kaskazini mashariki nchini Kenya Paul Soi amesema, watu hao wawili wanaaminika kukimbilia Somalia baada ya kufanya uhalifu katika kanda hiyo na hasa karibu na mpaka wa Liboi.

Polisi wamesema, wapiganaji hao wanahusika na shambulizi lililotokea tarehe 12 Oktoba huko Liboi, ambapo polisi 11 waliuawa.
 
Back
Top Bottom