Kenya na rwanda zazuia bidhaa za tanzania. Long live ea community!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kenya na rwanda zazuia bidhaa za tanzania. Long live ea community!!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by JokaKuu, Jun 26, 2011.

 1. J

  JokaKuu Platinum Member

  #1
  Jun 26, 2011
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,775
  Likes Received: 4,999
  Trophy Points: 280
  ..hivi kwanini Kenya na Rwanda hawaishi kutuzingua?

  ..hebu angalieni jinsi wafanya biashara wetu wanavyonyanyasika.

  ..halafu JK na Pinda hawaishi kutusimanga kwamba fursa za biashara zimejaa tele tatizo ni sisi Watanzania hatuzichangamkii.

  ..Wazalishaji wakubwa kama Azania na SSB wanasumbuliwa hivi, sembuse raia wa kawaida wa Tanzania?

  ..KWA MTIZAMO WANGU JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI NI MRIJA WA KUTUNYONYA WATANZANIA.


   
 2. lifeofmshaba

  lifeofmshaba JF-Expert Member

  #2
  Jun 26, 2011
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 868
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  kama wao wanapiga pin na sisi tufanye hivyo hivyo ndio maana USA na RUSSIA wanaheshimiana maana action na reaction are equal
   
 3. Mimibaba

  Mimibaba JF-Expert Member

  #3
  Jun 26, 2011
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 4,566
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Haya mambo yalitegemewa lakini watu madarakani wanatafuta umaarufu si maslahi ya kitaifa. Mchezo ni mchafu ni mchafu zaidi ya hapo, kwa sababu inaelekea hizo nchi mbili zinajitosheleza kwa bidhaa hizo kwa njia mbadala (magendo) kutoka Tanzania. Mimi ni mkulima, wakenya wako tayari kuja kununua mahindi toka shambani kwangu Dodoma. Wanayapitishaje mpakani wanajua wenyewe.

  Lakini tunalalamika njaa huku wengine tunapata mazao bei ni ya kipuuzi, halafu unazuiliwa usiuze nje. Ni ujinga, upuuzi na uonevu usio halali. Tukija kwa akina Bahresa nao wanataka mazao yetu kwa nguvu kwa bei wanayotaka.

  HAYA YANATOKEA TANZANIA TU KUTOKANA NA SERIKALI ISIYOJIELEWA
   
 4. Congo

  Congo JF-Expert Member

  #4
  Jun 26, 2011
  Joined: Mar 13, 2008
  Messages: 1,272
  Likes Received: 559
  Trophy Points: 280
  La msingi hapa ni kuangalia Rules of Origin. Kenya na Rwanda wanajua kabisa ngano inayosagwa Tanzania huwa imeagizwa kutoka nje ya EAC hasa Canada. Kinachofanyika Tanzania ni usagishaji tu. Gharama za usagishaji huo zinaweza kuwa za chini kiasi kwamba hazifikii asilimia inayoruhusiwa kulingana na Rules of Origin za EAC.
   
 5. Gagurito

  Gagurito JF-Expert Member

  #5
  Jun 26, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 5,610
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  EA COMMUNITY nh usanii tu, hakuna kitu hapo. Ngoja sudan kusini waingie tupigane vita!
   
 6. Mzalendo80

  Mzalendo80 JF-Expert Member

  #6
  Jun 26, 2011
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 2,385
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  Siku nyingi mimi nilikuwa nasema EAC ni usanii kama alivyo Kikwete, bora to stick kwenye SADC kuliko EAC
   
 7. simplemind

  simplemind JF-Expert Member

  #7
  Jun 26, 2011
  Joined: Apr 10, 2009
  Messages: 11,808
  Likes Received: 2,583
  Trophy Points: 280
  Tatizo lipo kwenye import duty ya ngano.Kenya inatoza ushuru wa 25% kuwalinda wa kulima while Tanzania tuliwatupa wakulima siku nyingi import duty ni 10%.Tanzania kuuza unga kenya itawa undercut kenya millers kutokana ushuru mdogo wa kuagiza ngano.,Common external tariffs ndio suluhisho/ hili gumu to implement sera ya Kenya ni kuwalinda wakulima wa ngano ambao wa nazalisha zaidi tani 350000 per year.
   
 8. Kobello

  Kobello JF-Expert Member

  #8
  Jun 26, 2011
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 5,688
  Likes Received: 656
  Trophy Points: 280
  Hivi tanzania ngano inalimwa wapi?...tani ngapi kwa mwaka?.....tunatumia tani ngapi humu nchini mpaka tuweze kuexport nje?
   
 9. F

  FJM JF-Expert Member

  #9
  Jun 26, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Kobello are you serious haujui kama Tanzania inalima ngano? nenda kaulize TBL! GOSH!!!

  Anyway, back to the thread, yule 'waziri mdogo' anaweza kueleza ni kitu gani kinaendelea mpaka Tanzania wapigwe stop?
   
 10. pascaldaudi

  pascaldaudi JF-Expert Member

  #10
  Jun 26, 2011
  Joined: Mar 25, 2009
  Messages: 534
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Wewe unaonekana una pointi, kwa hiyo hizo ROO zinahusikaje na kuzuia kuingiza/import bidhaa?
   
 11. simplemind

  simplemind JF-Expert Member

  #11
  Jun 26, 2011
  Joined: Apr 10, 2009
  Messages: 11,808
  Likes Received: 2,583
  Trophy Points: 280
  somewhere ,somehow someone is making superprofits at expense of Tanzania wheat farmers.
   
 12. Kobello

  Kobello JF-Expert Member

  #12
  Jun 26, 2011
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 5,688
  Likes Received: 656
  Trophy Points: 280
  Mkuu,kuhusu ngano,index zote zinaon yesha kuwa sisi ni net importer wa ngano.
  Domestic consumption yetu ni kama metric tonnes 620 kwa mwaka na tunaproduce kama metric tonnes 150 kwa mwaka.Mimi sitaki kabisa kuamini hizi indexes za masoko ya dunia,ila facts bila namba huwa hazina mshiko.
  Naomba mnijulishe kuhusu production ya ngano tanzania,kwa sababu ninavyojua mimi,ngano ya tanzania haitoshelezi mahitaji yetu kama watu wengi tunavyoshabikia.
  Sitaki kejeli.
  Source:IndexMundi.
   
 13. simplemind

  simplemind JF-Expert Member

  #13
  Jun 26, 2011
  Joined: Apr 10, 2009
  Messages: 11,808
  Likes Received: 2,583
  Trophy Points: 280
  What went wrong with Hanang wheat projects?Mradi ulikuwa unatoa matumaini on the future of large scale mechanized farming in Tanzania. Sadly this wanst to be.
   
 14. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #14
  Jun 26, 2011
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Joka kuu,
  I think there is more than meets the eye. Kama kweli hiyo ngano na mahindi ni ya Watanzania basi then something needs to be done.
  Lakini kama hiyo ngano ni imported, kama alivyodai mchangia mada mmoja hapa, basi Kenya na Rwanda wana kila haki ya kuzuia soko lao
  lisiwe flooded na imported grain. Na sisi je?
   
 15. p

  plawala JF-Expert Member

  #15
  Jun 26, 2011
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 627
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kule kwetu Hanang,nina tani 1000 ghalani(mwenyewe) kobello vipi bwana!
   
 16. Arafat

  Arafat JF-Expert Member

  #16
  Jun 26, 2011
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  Siyo CCM mkuu wavivu sana wakufikiri hawa jamaa, ebu angalia tulivyo bweteka na KCB hapa wakati wakina Kimei wameshindwa hata branch moja nje ya Tanzania? Majeshi yetu yamekaa miaka kibao Uganda baada ya vita vya Amini na ndio ili kuwa opportunity ya kuwekaza Uganda lakini hamna kitu kiwanda cha sukari kagera ndio kwanza hata hatujui wanafanya nini, wakati kama CCM ingeluwa makini wangeweza kukamata soko lote la sukari Uganda mara tu baada ya Vita.

  Hao wanyarundwa hadi kusoma wamesoma hapa na wengine wapo ndani ya CCM hadi leo lakini tumeishia kuwaifadhi tu! wakati kama CCM inge kuwa makini baada ya vita vya Rwanda Tanzania ilikuwa na opportunity nzuri ya kusaini mikataba ya kuijenga upya Rwanda kazi ya ni kusaini mikataba ya kugawa madini na wanyama na mazao ya miti kwa rushwa kwenda ngambo tu!

  Tulikuwa na nafasi ya kuwekeza na kupata nafasi za ajira na nafuu ya visa katika nchni za A.Kusini, Zimbabwe na Msumbuji kwa wamakonde lakini CCM hawajui la kufanya wanasinzia tu!

  Hiki chama lazima kiondoke maana ukikifikiria unaweza kulia bure.
   
 17. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #17
  Jun 26, 2011
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,785
  Likes Received: 2,395
  Trophy Points: 280
  ukweli ni kwamba wa kenya wanataka raw materials tuu toka tanzania,lakini bidhaa zilizotayari hawataki kabisa tuingize kwao.cha muhimu nasi tukataze za kwao kuja kwetu!!!
   
 18. Kobello

  Kobello JF-Expert Member

  #18
  Jun 26, 2011
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 5,688
  Likes Received: 656
  Trophy Points: 280
  Duh! sorry nilimaanisha tunatumia 620,000 tonnes na kuzalisha less than 150,00tonnes.
  Nilipouliza zinalimwa wapi na kwa kiasi gani nilikuwa nataka watu watoe data badala ya porojo,sikumaanisha kuwa sijui zinalimwa.But those questions were supposed to be provocatieve.
   
 19. Kobello

  Kobello JF-Expert Member

  #19
  Jun 26, 2011
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 5,688
  Likes Received: 656
  Trophy Points: 280
  Siipendi EAC,ila hawa wafanyabiashara wanaboa,kwanini waexport ngano ilhali demand hap;a tanznia ni kubwa kuliko production?
   
 20. l

  ladywho Senior Member

  #20
  Jun 26, 2011
  Joined: Apr 28, 2011
  Messages: 107
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  NCHI ILISHALAANIKA HII, tunakuwa vimbwa nyumbani kwe2, tunanyanyaswa na.... Dah! Mpaka nashindwa la kusema! MUNGU INUSURU NCHI HII NA LAANA INAYOITAFUNA SLOWLY!
   
Loading...