Habari waungwana,
Kenya na Changarawe ni vitongoji vilivyopo mjini Iringa katika kata ya Migori, vitongoji hivi shughuli nyingi zimekwama kutokana na ukosefu wa maji. Wanakijiji wa mji wa Kenya wanafata maji kilomita 20 huku mfanyabiashara wa maji akitumia mkokoteni inayokokotwa na Punda.
Wanawake katika kijiji hicho wamelalamikia tatizo la maji kusababisha kushindwa kumudu suala la usafu kwenye ndoa zao kwani hununua ndoo kwa Tshs 2,000 na ni mtu mmoja pekee ndio anauza maji kitongoji kizima na zinaweza kupita siku mbili bila mtu kufanikiwa kupata maji kutoka kwa bwana huyo. Baadhi ya wanawake wamepumzishwa ama kuachika kwa waume zao kwa tuhuma za kunuka.
Mfanyabiashara wa maji, Richard Kisinga amesema anauza maji bei juu kutokana na kuyapata umbali mrefu huku wa chini kabisa ukiwa kilomita 15 na kuendelea kutoka na ugumu wa kupata maji siku husika.
Kwa msaada wa RFA.