Kenya: Mwandishi wa BBC amejiuzulu na kujiunga na mapambano ya silaha Ethiopia

Rahma Salum

Member
Sep 7, 2020
30
59
Desta Gebremedhin Asefa aliwahi kuwa mwandishi wa BBC katika ofisi zilizopo Kenya. Mei 28, 2021 ameachana na chumba cha habari na kujiunga na uwanja wa vita huko Tigray, Ethiopia.

Million Haileselasie, mwandishi wa habari wa DW Amharic, ali-tweet, "Desta Gebremedhin @Desta_Geb, mwandishi wa BBC, alijiuzulu kutoka BBC na amejiunga na mapambano ya silaha huko Tigray."

Hata hivyo, BBC imetoa taarifa ndani ya ofisi kwa wafanyakazi kuwa Desta hatambuliki kama mwenzao tena.

Ni miezi sita tangu mzozo ulipozuka katika eneo la Tigray nchini Ethiopia. Ripoti zinaonyesha kuwa vita vilianza baada ya serikali ya Ethiopia kutaka kukiondoa chama kilichokuwa kikitawala eneo hilo, Tigray People's Liberation Front (TPLF).

Kulingana na ripoti ya BBC, TPLF ilikuwa na mzozo na Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed juu ya mabadiliko ya kisiasa kwa mfumo wa shirikisho wa Kitaifa. Mzozo huo ulisababisha vita kati yao.

Aidha, kukamatwa kwa TPLF na vituo vya jeshi vya serikali huko Tigray kunaaminika kuzidisha hali hiyo.

Hadi sasa, ripoti zinaonesha kuwa maelfu ya watu wameuawa wakati takriban milioni 1.7 wamelazimika kuhama makazi yao.

Chanzo: Nairobi Leo​


20210529_200927.jpg
 
Back
Top Bottom