Kenya: Mwanamke amshambulia Polisi kwa kumn'goa sikio

Ben Zen Tarot

JF-Expert Member
Dec 13, 2014
3,907
6,700
Afisa mmoja wa Polisi huko nchini Kenya ameshambuliwa na mwanamke kutoka eneo la Lang'ata Jijini Nariobi, kwa kung'atwa hadi kutolewa sikio lake wakati wa purukushani kati yake na mwanamke huyo.

Taarifa zinadai kuwa Mwanamke huyo alimshambulia Polisi baada ya kuulizwa kwanini amekaa nje baada ya saa mbili usiku ndipo wakaanza kurushiana maneno kisha akamrukia Polisi na kumshika kichwa chake kwa nguvu na kumng'ata sikio hadi kuling'oa.

Ripoti ya Polisi inaeleza kuwa "Baada ya kugundua amemjeruhi afisa huyo, alikimbilia katika mto unaopakana na Lang’ata na Kibera,

Sajini huyo aliokota sikio lake ambalo lilikuwa limeanguka na kuelekea hadi Hospitali ya Nairobi West”.

Aidha ripoti hiyo imeendelea kwa kusema uchunguzi kuhusiana na kisa hicho unaendelea huku Afisa huyo wa Polisi akisubiri kufanyiwa upasuaji wa kupandikiza sikio lake.
 
Madhara ya lockdown hayo ndio maana Tanzania tuñikataa lockdown

Hilo eneo kiboko ndio.maana linaitwa Lang'ata kuna watu wanaga'ta hatari na meno
 
Siombei yanitokee ya huyo polisi ila endapo mwanamke fulani kanifanyia hivyo mimi Mungu ndio anajua.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom