Kenya mtamlaumu nani kwa hili ikiwa mnakosea mahesabu wenyewe?

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,410
Habari wanaJF,

Katika harakati za kuchukua fursa za nchi ambazo ni LANDLOCKED wakenya wamekosa tena deal la Standard Gauge Railway kutoka Rwanda na Burundi. Tanzania wameibuka vinara tena kwasababu ya unafuu wa gharama ulipo. Huku Kenya wakiponzwa na gharama kuwa juu katika ardhi yao.

Sasa ndugu zangu wanaJF, kufuatia Serikali za Rwanda na Burundi kuamua kujenga mradi wa reli kuziunganisha nchi za Rwanda, Burundi mpaka Bahari ya Hindi nchini Tanzania umechukua sura mpya ambapo nimefanya upembuzi yakinifu na kugundua kuwa umbali wa takribani Km 2,561 Standard Gauge Railway kutoka Pwani ya Tanzania kwenda Burundi na Rwanda itagharimu dola za Kimarekani takribani $7.6bn.

Sasa upande wa pili kutoka ndugu zetu Kenya kujenga Standard Gauge Railway mpaka Rwanda na Burundi ambako ni takribani Km 490 sasa hii itakuwa na gharama za jumla ya dola za Kimarekani $4bn. Jamani huu ni ufisadi mkubwa sana katika ujenzi wa mradi huu. Kwa sababu hii inamaanisha gharama ya kupitisha Kenya ni mara 5 na ushehe kwa gharama ya kupitisha katika ardhi ya TANZANIA.

My Take: Kenya endeleeni kulala na kujifanya mabepari sijui mabeberu, Tanzania wanachapa mwendo.
 
Back
Top Bottom