KENYA: Mgombea UPINZANI ashinda USPIKA

Mabbyjr

Member
Aug 19, 2007
29
1
Hatimaye mgombea kiti cha USPIKA nchini Kenya kutokea chama cha upinzani ashinda kiti hicho. Mgombea huyo aitwaye Kenneth Marende iliibuka kidedea kwa kura 105 dhidi ya kura 101 za mpinzani wake aliyekuwa akiiungwa mkono na serikali (Francis ole Kaparo)

Tunajua vilifanyika vikao vya siri kati ya PNU na ODM ya Kalonzo kuhakikisha ushindi kwa vyama vyao ambavyo vinaiunga mkono serikali lakini jamani sauti ya watu ikishatamka basi hakuna jinsi. SASA KAZI KWA MWAI KIBAKI, sijui hiyo serikali hataiendesha vipi wakati kapoteza ushindi bungeni.
 
Hatimaye mgombea kiti cha USPIKA nchini Kenya kutokea chama cha upinzani ashinda kiti hicho. Mgombea huyo aitwaye Kenneth Marende iliibuka kidedea kwa kura 105 dhidi ya kura 101 za mpinzani wake aliyekuwa akiiungwa mkono na serikali (Francis ole Kaparo)

Tunajua vilifanyika vikao vya siri kati ya PNU na ODM ya Kalonzo kuhakikisha ushindi kwa vyama vyao ambavyo vinaiunga mkono serikali lakini jamani sauti ya watu ikishatamka basi hakuna jinsi. SASA KAZI KWA MWAI KIBAKI, sijui hiyo serikali
hataiendesha vipi wakati kapoteza ushindi bungeni.
 
Hapo ndipo unapoambia chagua kusuka au kunyoa,huyu Kibaki katuboa kinoma.Tunaomba spika amuapishe Odinga na siyo huyu dictator Kibaki.ODM oyeeeeee.
 
Pia naibu Spika ametoka Upinzani baada ya kuongoza kwa Kura 110 katika Raundi ya kwanza na ktk Raundi ya pili Mshindani wake alijitoa hili kupisha demokrasia ifuate mkondo wake.
 
To me hii naiita democrasia dume

Pamoja na kuwa kumekuwepo na machafuko kadhaa na vifo huko Kenya bado nasifia siasa za Kenya kwa kuwa zinaongoza katika Afrika Mashariki na pengine Afrika nzima. Hii inatokana na namna wakenya walivyolelewa kielimu. Elimu yao ambayo imezama katika Kingereza imewawezesha wakenya kujenga uwezo wa kujieleza na hata kujua haki yao. Hali hii imezaa kundi kubwa la watu wenye uwezo wa kuongoza nchi na hata kusimama ilivyo katika ulingo wa siasa. Mfumo huu licha ya kukuza demokrasia pia ni chachu kwa maendeleo ya nchi. Hakika Kenya itapiga hatua kubwa mara hali ya utulivu itakapotulia. Nasema hivyo kwa kuwa Kenya imepata coverage kubwa kwenye international news media, CNN, BBC, SKY, AL JAAZIRA, SABC, VOICE OF AMERICA, ABC, CCTV, DWTV, RSTV na nyinginezo nyingi. Kwa sasa kila mtu anajihoji kulikoni kenya kuna nini?

Labda niseme kuwa Mzee Jaramogi Odinga alichagua upande sahihi kwa Kenya kwa kuipa nguvu kambi ya upinzani tangu miaka ya 80s. Hii imefanya Kenya kutokujenga tabaka la moja kwa moja la viongozi na badala yake Tabaka hilo limekuwa likipata shida kubwa namna ya kuidhibiti siasa za kenya. Kwa kuwepo kwa Raila kwenye siasa za Kenya napo kumeamsha namna nyingine ya siasa ngumu katika bara la Africa. Kumbuka Raila alisaidia kupunguza nguvu za KANU na kukifanya kuwa chama Kidogo. Na hii ilitokana na kukosekana kwa demokrasia ndani ya KANU mara baada ya Toroitich Arap Moi kuonyesha dhaili kumhunga mkono Uhuru Kenyata kuwa mgombea Urais badala ya kuruhusu wanachama kuchagua mgombea ambapo Raila wakati huo akiwa Katibu wa KANU alikuwa na asilimia kubwa za kusimama kwa tiketi ya KANU. Hali hiyo ilipelekea Raila kudadili siasa za Kenya na kukiondoa KANU na NARC kuchukua uongozi wa nchi huku Kibaki akiwa President. Katika Kenya Wajaluo wamekuwa ni watu wa kuogopwa sana kutokana na misimamo waliyonayo na kujijengea misingi ya kijamaa zaidi. Wajaluo wamekuwa hawafit kwenye system iliyokuwepo madarakani ambayo hata Kibaki alihirithi bila kubadili chochote. Hii ilipelekea kutofautiana na Raila na hatimaye ODM imeibuka na kuwa ni chama chenye nguvu katika siasa za vyama vingi Kenya.

Kuchaguliwa kwa Spika na Naibu speaker ni moja ya msukumo mpya wa siasa nchini Kenya. Tunapongeza kenya kwa hatua hii kubwa. Tunakitakia heri ODM Katika mapambano dhidi ya makundi ya kifisadi ambayo yanaanguka kila utawala unapotoka. Leo hii Nicolaus Bewot anaonekana ni historia katika siasa za Kenya na Moi ndo amekwenda. Kesho hakutakuwepo SAITOT, Michiki, Kibaki, Uhuru, na hata kibaka mwingine wa sauti za wakenya Kalonzo.

Watanzania bado tupo nyuma. Richa ya kuwepo kundi kubwa la watu ambao si wasomi lakini hata wale wasomi wachache waliopo bado hawana uwezo wa kutafakari na kubaini ni jinsi gani mabadiliko yanapaswa kuwepo kwenye jamii yetu. Pia lazima tutambue kuwa maendeleo yetu hayawezi kuja katika njia yakutegemea mipango ya viongozi. Ni lazima tuwalazimishe kujituma na kufanya yale ya msingi vinginevyo wanakaa pembeni. Inawezekana kazi ni tunaanzia wapi. Tusitegemee mtu mmoja kutuletea mabadiliko. JK si suluhu bali tunapaswa kubadili system nzima na kuivuruga ianze upya. Pia lazima tuanze kuandaa viongozi wa Kesho kwa Wingi. Leo hii ni vigumu kujua ni nani anaonekana kufaa nchi hii kama Rais baada ya JK. Just mention 5 strong politicians. You can see the difference with Kenya where there is plenty of them, Bi. Charity,Pro. Wangari, Rahila, Msalia, Pro. Anyang' Nyong'o, Ruto,Balala, Martha Kalua, Matiba, Nyaga na wengine wengi tu. Bongo bado mno. Jiulize katika nchi maskini kama yetu inakuwaje mtu wa chama kile kile tangu uhuru anashinda kwa asilimia 80s?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom