KENYA: Mahakama yasitisha kwa muda kodi ya asilimia 16 kwenye bidhaa za petroli

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,445
3,403
Hii inasubiri mahakama kusikiliza ombi la wakazi watatu wa Kisumu. Kupitia mawakili wao Kenneth Amondi, Titus Alila, Jackline Otieno na Francis Ogada, waliomwambia Jaji Stephen Riechi kuwa kodi mpya zitapandisha gharama za maisha.

Uamuzi wa mahakama hiyo tayari hivi sasa umeleta mkanganyiko. Jumanne Septemba 4, 2018, Mahakama Kuu ya Nairobi Chacha Mwita alikataa kusitisha kwa muda kodi hiyo kwa misingi ya kuwa mchakato wa utungaji wa sheria hiyo ulikuwa haujamalizika kwa sababu Rais Uhuru Kenyatta alikuwa hajatia saini msuwada huo au aliutupilia mbali Muswada huo mwaka 2018.

Wachambuzi wa mambo ya biashara nchini Kenya wanasema bei za mafuta katika vituo vya mafuta kuna uwezekano mkubwa zisibadilike kufuatia matangazo yaliyo tolewa na Tume ya Kusimamia Nishati (ERC) Septemba 1, 2018

“Japokuwa hili litabadilika iwapo marekebisho ya muswada wa fedha wa 2018 kama ulivyopitishwa na Bunge ukipitishwa kuwa sheria, mchakato wa bei za mafuta kwenye vituo itarekebishwa..” limesema tamko kutoka ERC Jumamosi.

Kufuatia kodi hiyo mpya, nchi imeshuhudia uhaba wa mafuta kwani wasambazaji wa mafuta wamekataa kuchukua mafuta kutoka kwenye depo za mafuta ikiilazimisha serikali kutoa ulinzi kwa wasambazaji hao wakuu.
 
So ile budget waliokuwa wakipita huku wakijigamba nayo mahakama imesimamisha.
Tutegemee a wide gap between the budget and actual expenditure.
 
Mahakama imefanya jambo la maana sana. Kwa mara ya kwanza naona kesi haikupelekwa mahakamani na mtetezi wa wanyonge Bw. Okiya Omtatah.

Ahaaa haaa haaa
Ile US $ 700 MILLION walioshauriwa na WBG/IFM wataipata wapi? Gap will be narrowed?
 
Mahakama za Kenya zina very wide jurisdiction to operate on tofauti kabisa na mahakama za Tanzania.

Shauri kama hili ambapo serikali inalalamikiwa na wananchi walipa kodi haliwezi kusikilizwa na mahakama yoyote ya Tanzania kwani hapo mahakama zetu zitadai haziwezi kuingilia mhimili mwingine...!!

Nakumbuka ile kesi ya Mtikila V State kuhusu mgombea binafsi jinsi jaji mkuu wa wakati ule alivyo prove kuwa he was nothing but a mere puppet of the ruling party, pale alipotoa uamuzi wa hovyo ktk shauri lile kiasi kwamba jaji yeyote wa Kenya asingetoa uamuzi wa kijinga vile. Mahakama zetu bado saana saana.
 
Nadhani mahakama kuwa na maamuzi ya mwisho ni jambo la maana sana. Mimi binafsi kama mkenya nakubali maamuzi ya mahakama zaidi ya yale ya bunge au serikali ambazo zinaongozwa na wanasiasa akiwemo rais. Hayo ndio matunda ya katiba mpya.
 
Go with that court order and ask for petrol @113 instead of 130 bob then you will know kenya is truly a failed state :D
 
Sasa hivi nikitaka naeza nikawashtaki mahakamani kampuni au serikali na mtu yeyote yule ambaye anakeuka masharti ya mahakama kuhusu bei ya bidhaa za petroli na sheria itakuwa upande wangu. Hiyo haikuwa point yangu na kama kawaida huwa hupati mantiki ya hoja yeyote ile. Tungoje maagizo ya mahakama kwanza, kesi ikishasikizwa. Jaribu kuthubutu kufanya hayo niliyoyaongelea hapo juu huko kwa Jiwe alafu baadaye uje na mrejesho.
 
Tanzania Gvt is sued every other time both internationaly and locally, Sometimes it wins and sometimes it looses..
Here is a recent example of when it lost localy in its own courts
Tanzania bloggers win temporary court order against state crackdown
Wacha porojo na unafik, Lipa ushuru bila kusumbua
 
Unaniletea habari za Jiwe kukandamiza uhuru wa kujieleza na uhuru wa wanahabari wakati tunaongea kuhusu bei ya bidhaa na ushuru ndio iweje sasa? Uhuru wa wanahabari ni jambo la kawaida sana kwenye nchi ambazo haziongozwi na madikteta. Sasa kwa sababu umeamua tubadilishe hoja kama rangi za kinyonga nangoja uniletee habari za kesi ya kupinga uchaguzi wa urais kwenye mahakama za Tz. Alafu sijui kwanini unanijibu kwa kiingereza wakati ni kibovu zaidi ya kile cha Sizonje.
 
What are you struggling to say? Hahahaha..Siku njema kaka kula ujeuri wako :D
 
Back
Top Bottom