Kenya: Mahakama Kuu yazuia mapendekezo ya mabadiliko ya Katiba yenye "utata"

Lady Whistledown

JF-Expert Member
Aug 2, 2021
1,023
1,609
Marekebisho hayo yangekuwa mabadiliko makubwa zaidi kwa mfumo wa kisiasa wa Kenya tangu ilipoanzisha katiba mpya mwaka wa 2010.

Mahakama ya juu nchini Kenya imetangaza mabadiliko ya katiba yenye utata yaliyopendekezwa na Rais Uhuru Kenyatta na washirika wake kabla ya uchaguzi Mkuu mwezi Agosti kuwa ni kinyume cha sheria.

Lakini uamuzi wake wa Alhamisi ulibainisha uwezekano wa mabadiliko hayo - maarufu kama Building Bridges Initiative (BBI) - kuwasilishwa tena na bunge au kwa njia nyinginezo, mradi tu ikithibitika Rais hakuwa na mkono katika mabadiliko hayo.

"Mswada wa marekebisho ya katiba wa 2020 ni kinyume cha sheria," Mahakama ya Juu ilisema katika uamuzi wa wengi, na hivyo kumaliza vita vya kisheria vilivyodumu kwa takriban miaka miwili kuhusu mapendekezo hayo.

"Rais hawezi kuanzisha marekebisho ya katiba au mabadiliko kupitia mpango maarufu chini ya kifungu cha 257 cha katiba," ilisema.

Marekebisho hayo yangepanua mamlaka na kuongeza idadi ya viti vya ubunge kutoka 290 hadi 360, katika mabadiliko makubwa zaidi ya mfumo wa kisiasa wa Kenya tangu ilipoanzisha katiba mpya mwaka wa 2010.

Uamuzi huo ulitolewa na benchi ya majaji saba katika Mahakama Kuu inayoongozwa na Martha Koome, jaji mkuu wa kwanza mwanamke nchini. Mapendekezo hayo pia yalikataliwa mwaka jana na Mahakama Kuu na Mahakama ya Rufaa, ambayo ilisema Kenyatta anaweza hata kushtakiwa katika mahakama ya kiraia kwa kuanzisha mchakato huo.

Rais alisema kuwa mpango huo - suala la dharura ambalo limegawanya wasomi wa kisiasa - utafanya siasa shirikishi zaidi na kusaidia kumaliza mzunguko wa mara kwa mara wa ghasia za uchaguzi katika taifa hilo la Afrika Mashariki.

Soma: Kenya: Supreme Court blocks controversial constitutional reforms
 
Japo nilikua mojawapo wa waliokua wanaunga mikono haya mabadiliko, ila nimeshukuru kwa hili la ukomavu na uhuru wa mahakama kwenye nchi yetu, kwamba sio rais wala nani yeyote mwenye uwezo juu ya mahakama au sheria au katiba, wengi tungependa baadhi ya hayo marekebisho kweye katiba, maana hamna katiba iliyo bora kwa asilimia 100%, ila taratibu za kikatiba zifuatwe hatua kwa hatua.

Huu ni ushindi mkubwa kwa Wakenya wote, waliounga mikono au waliokatalia, ni wazi mahakama zetu ziko huru na zina uwezo wa kufanya maamuzi bila kuzingatia shinikizo za kisiasa.

Hamna kitu kibaya kwenye taifa kama mahakama hazipo huru, hapo ndio huwa chanzo cha vita, maana kama hauwezi kutendewa haki na vyombo husika, inabidi ufanye yako wewe mwenyewe.

Rais Uhuru kwenye hili alibugi step na kama vipi awajibishwe........
 
Vizuri sana BBI kaanguka na Raila ataanguka kama kawaida yake!😢
A failure since sijui 1977😂

Ruto mpaka ikulu,a blessed man indeed kila kitu anataka akishaomba Mola kinatendeka!
Yaani ata hawaamini watu wa azimio wanajipea moyo tu🙈eti wanasema"eti wametosheka na wako na raha na matokeo ya BBI"💩na venye wametumia nguvu yao nyingi na kuharibu pesa za raia na failed projects"huduma number na BBI"💩
Mungu ako nasi Mahustler🔥
 
Wengine wa Kusini hata hawana mahakama. Wana taasisi ya kupiga rubber-stamp tu.
 
Japo nilikua mojawapo wa waliokua wanaunga mikono haya mabadiliko, ila nimeshukuru kwa hili la ukomavu na uhuru wa mahakama kwenye nchi yetu, kwamba sio rais wala nani yeyote mwenye uwezo juu ya mahakama au sheria au katiba, wengi tungependa baadhi ya hayo marekebisho kweye katiba, maana hamna katiba iliyo bora kwa asilimia 100%, ila taratibu za kikatiba zifuatwe hatua kwa hatua.

Huu ni ushindi mkubwa kwa Wakenya wote, waliounga mikono au waliokatalia, ni wazi mahakama zetu ziko huru na zina uwezo wa kufanya maamuzi bila kuzingatia shinikizo za kisiasa.

Hamna kitu kibaya kwenye taifa kama mahakama hazipo huru, hapo ndio huwa chanzo cha vita, maana kama hauwezi kutendewa haki na vyombo husika, inabidi ufanye yako wewe mwenyewe.

Rais Uhuru kwenye hili alibugi step na kama vipi awajibishwe........
HONGERA Kenya kwa uhuru mkubwa wa Mahakama yenu.
 
The court doing what others country court can not try at al
Yes courts in other countries cannot do that. I mean they cannot enforce a Kenya constitution. That can only be done by Kenyan court which they did! Nothing extraordinary at all!
 
Back
Top Bottom