Kenya: Lockdown yasabibisha uhalifu kuongezeka, Marekani yatahadharisha raia wake

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,001
9,867
Marekani imetahadharisha Raia wake wasisafiri kipindi hichi cha #COVID19 kuingia Kenya kwa kuwa matukio ya kihalifu yameongezeka mara dufu.

Onyo limetolewa kuwa kuna ongezeko la ugaidi, utekaji watu, na utekaji magari pia masuala ya afya na ujambazi ambayo ni pamoja na kuvunjiwa nyumba.

Maeneo yaliyowekewa mkazo ni mpakani mwa Kenya na Somalia, kaunti ya Turkana, Kibera na maeneo ya mwambao.

Kwa wamarekani walioko Kenya wameshauriwa wakikabwa wasiwe wabishi ili kuepuka madhara, pia wameshauriwa kutembea na photocopies za pasi zao za kusafiria.

 
Serikali ya Marekani imeshauri raia wake dhidi ya kutembelea Kenya kutokana na hatari kubwa ya kuambukizwa virusi vya corona.
Screenshot_20210407-203344.png


Kituo cha kudhibiti magonjwa kimeiweka Kenya kwenye 'kiwango nambari nne' (level 4) cha nchi zinazokumbwa na hatari ya Covid19.

Hali ya Kenya ilivyo sasa hivi inaonekana kuzua hofu machoni mwa nchi nyingi za Ughaibuni; Ikumbukwe tayari Uingereza ilishapiga marufuku wasafiri wote wanaotokea Kenya - jambo lililopelekea Kenya nao kuwajibu kwa kuweka karantini ya lazima ya siku 14 kwa raia yeyote wa kigeni anayetua Nairobi akitokea Uingereza.

Idadi ya Maambukizi imefikia 141,367 huku vifo vikiwa 2,276.
 
Yasemekana sisi wapiga nyungu kwenda UK, US na kote duniani ruksa.

Au nasema uongo ndugu zangu?
 
Baada ya uingereza kupiga ban mizungu feki ya kikenya kutia mguu UK, USA nao wameongeza maumivu..Wananchi wa Usa ni marufuku kuingia kenya
Sasa wabobezi wa kidhungu waende kibera vijiweni waongee huko hicho kilugha chao cha malkia😂😂😂
IMG_20210408_121444.jpg
 
Ndio mjue mabeberu hayana urafiki au undugu!! Kenya kuna tone tu LA corona ukilinganisha na marekani na uingereza lakini wameanza kuwanyanyapaa as if mmejinyea!! Ndugu na marafiki Wa kweli ni majirani zenu Wa afrika ya mashariki!! Tumieni nguvu nyingi kuboresha mahusiano among east african countries!
 
Ndio mjue mabeberu hayana urafiki au undugu!! Kenya kuna tone tu LA corona ukilinganisha na marekani na uingereza lakini wameanza kuwanyanyapaa as if mmejinyea!! Ndugu na marafiki Wa kweli ni majirani zenu Wa afrika ya mashariki!! Tumieni nguvu nyingi kuboresha mahusiano among east african countries!

Eti leo hii uingereza na marekani ndiyo wa kuwatamkia wakenya maneno haya!!!?
 
Hawa jamaa kujikombaga kote kule kwa wazungu ila bado wanawaona takataka tu
 
Back
Top Bottom