Kenya kuripoti Kisa cha kwanza cha virusi vya Homa ya Nyani 'Mpox'

Wild Flower

JF-Expert Member
Jul 20, 2023
311
661
Wizara ya Afya imethibitisha kesi ya kwanza ya ugonjwa wa virusi vya 'Mpox' mpakani mwa Taita Taveta na Tanzania baada ya kugunduliwa kutoka kwa mtu mmoja aliyekuwa akisafiri kutoka Uganda kuelekea Rwanda

Mamlaka hiyo imetoa tahadhari kwa raia wa Kenya Julai 31, 2024 kujilinda dhidi ya mlipuko wa Ugonjwa wa Ndui ya Nyani maarufu kama "Mpox" kwa kuwashauri kunawa mara kwa mara kwa maji na sabuni au vitakasa mikono na kuepuka misongamano

Nchi nyingine zenye maambukizi ya Ugonjwa huu barani Afrika ni Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo inayoongoza kuwa na idadi kubwa ya visa hivi​

================For English Audience============

Kenya has confirmed its first Mpox case at a Taita Taveta border point with Tanzania. The virus was detected in an individual who was travelling from Uganda to Rwanda through Kenya.
The infection, which is caused by the monkeypox virus, spreads through close contact, causing flu-like symptoms and a painful rash. Most cases are mild but it can kill.

The Ministry of Health did not divulge any more information about the individual. However, it advised Kenyans to be vigilant and wash hands often in order to reduce risk of infection.
"Wash hands often with soap and water or hand sanitiser. If you have symptoms, seek health advise and avoid close contact with other persons...avoid close contact with persons with suspected or confirmed disease," the Ministry said in a statement.

"Person-to-person transmission can occur through direct contact with infectious skin or other lesions such as in the mouth or on the genitals. The disease can also be transmitted through respiratory droplets."
The virus is endemic to the Democratic Republic of Congo, as well as forested areas in East, Central and West Africa.

Earlier this month, Kenya had issued a travel advisory to all counties and border entry points. This came as a response to recent outbreaks of Mpox in the Democratic Republic of Congo, which currently has the biggest outbreak of the viral Mpox disease ever recorded, with tens of thousands of people infected as of June.
SOURCE: THE NATION
 
Huyo ni mtu wa kongo tu ndio huwa wana hayo magonjwa ya ajabu ajabu. Na saa hii wanaingia sana Tanzania sijui kufanya biashara gani, serikali iwaweke quarantine ya mwaka m'moja pale mpakani. Tutaambukizana mangonjwa ya hovyo kwasababu za kipuuzi puuzi tu hapa.

Majitu yanakula popo, bundi, nyani, panya, kitu chochote kinachotembea yanakula kwann yasiwe na magonjwa ya ajabu ajabu.

Tanzania kushika Dini zetu na kutii Imani imetuweka mbali sana na maradhi ya hovyo hovyo.
 
Mamlaka hiyo imetoa tahadhari kwa raia wa Kenya Julai 31, 2024 kujilinda dhidi ya mlipuko wa Ugonjwa wa Ndui ya Nyani maarufu kama "Mpox" kwa kuwashauri kunawa mara kwa mara kwa maji na sabuni au vitakasa mikono na kuepuka misongamano
Huu watakuwa wameutengeneza kupunguza makali ya Gen-Z movement
 
.

Kenya imethibitisha kisa cha kwanza cha maradhi ya homa ya nyani maarufu Mpox katika eneo la kusini-mashariki mwa nchi hiyo inayopakana na Tanzania.
Virusi hivyo viligunduliwa kwa mtu aliyekuwa akisafiri kutoka Uganda hadi Rwanda kupitia Kenya.
Wizara ya afya inasema msongamano mkubwa wa watu kati ya Kenya na mataifa mengine ya Afrika Mashariki unaleta hatari kubwa ya kuenea kwa ugonjwa huo katika eneo hilo.
Kupitia katibu wa wizara ya afya Mary Muthoni Muriuki, Wizara hiyo imesema kuwa inashirikiana na serikali za kaunti ili kuhakikisha kuwa maradhi hayo yanazuiwa haraka iwezekanavyo.
Wasiwasi unaongezeka kuhusu kuenea kwa aina mpya na hatari ya maradhi hayo katika eneo la Afrika Mashariki.
Maambukizi mengine ya ugonjwa huo pia yameripotiwa DRC, Burundi na Jamhuri ya Afrika ya Kati.
Homa ya nyani, ambayo zamani ilijulikana kama monkeypox ni ugonjwa unaosababishwa na virusi vya monkeypox.
Unaenezwa kwa kugusana moja kwa moja na ngozi iliyoambukizwa. Unaweza pia kupitishwa kupitia mate mtu anapokohoa
Dalili ni pamoja na upele wa ngozi, vidonda mdomoni na sehemu za siri.
Kawaida hutibika bila matatizo ndani ya wiki mbili hadi nne.
Hatahivo maambukizi sugu yanahitaji matibabu maalum.

Ushauri kwa umma:​

  • Wakenya wametakiwa kufuata masharti ya kiafya katika maeneo ya umma ili kujilinda binafsi, familia zao na jamii kutokana na kuenea zaidi kwa ugonjwa huo.
  • Waoshe mikono kwa sabuni na maji mara kwa mara
  • Walio na dalili wametakiwa kufuata ushuari wa kiafya na kuzuia kushikana na watu wengine ili kuzuia maambukizi kabla ya kwenda katika kituo cha afya kilicho karibu
  • Kuzuia kushikana kimwili na mtu anayeshukiwa kuwa na maradhi hayo

Homa ya Nyani ni maradhi gani?​

.

Maelezo ya picha,Virusi vinasababisha homa kali na vipele
Aina mpya ya virusi vya Homa ya Nyani {Mpox} inaenea kwa haraka katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, na wataalamu wanasema ni aina hatari zaidi waliyoishuhudia.
Maradhi hayo, ambayo zamani yaliitwa monkey pox, yameenea katika sehemu za magharibi na kati mwa Afrika na kesi zimekuwa zikiongezeka katika bara hilo kwa miongo kadhaa.
Mwaka 2022, janga la ulimwengu la Homa ya Nyani liliathiri Ulaya, Australia, Marekani na nchi nyingine nyingi.
Ugonjwa wa Mpox husababishwa na virusi vya monkeypox, familia moja ya virusi na ndui, ingawa si kali sana.
Virusi hivi awali vilisambazwa kutoka kwa wanyama hadi kwa wanadamu, na hupatikana zaidi katika nchi zilizo karibu na misitu ya mvua ya kitropiki.
Katika maeneo hayo, kuna maelfu ya wagonjwa na mamia ya vifo kutokana na ugonjwa huo kila mwaka, na watoto chini ya umri wa miaka 15 wameathirika zaidi.
Kuna aina mbili kuu za virusi zinazojulikana kuwepo. Hali mbaya zaidi ilisababisha mlipuko wa kimataifa mnamo 2022 ambao ulienea kwa karibu nchi 100 ambazo hazikuwahi kukumbwa na virusi hivyo.
Aina ya pili hatari zaidi ipo katika Afrika ya kati mbayo ni aina mpya iliyogunduliwa hivi karibuni nchini DR Congo.
Aina hizi mbili hubeba hatari tofauti za ugonjwa na vifo.

Dalili za ugonjwa wa Mpox​

.


Dalili za awali ni pamoja na homa, maumivu ya kichwa, uvimbe, maumivu ya mgongo na misuli kuuma.
Mara baada ya homa , upele unaweza kutokea, mara nyingi huanza kwenye uso kisha kuenea kwenye sehemu nyingine za mwili, mara nyingi viganja vya mikono na nyayo za miguu.
Upele, ambao unaweza kuwasha au kuumiza sana, hubadilika na kupitia hatua tofauti kabla hatimaye kutengeneza kipele, ambacho hutumbuka baadaye. Vidonda vinaweza kusababisha makovu.
Maambukizi kawaida huisha yenyewe na hudumu kati ya siku 14 na 21.
Kesi mbaya zinaweza kutokea kwa kushuhudia vidonda vikishambulia mwili mzima, na haswa mdomo, macho na sehemu za siri.

Je, hueneaje?​

Mpox huenea kutoka kwa mtu mmoja hadi kwa mwingine kwa kuwa karibu na mtu aliyeambukizwa, ikiwa ni pamoja na kupitia ngono, kugusana ngozi na kuzungumza au kupumua karibu na mtu mwingine.
Virusi vinaweza kuingia mwilini kupitia ngozi iliyo na michubuko, njia ya upumuaji au kupitia macho, pua au mdomo.
Inaweza pia kuenea kwa kugusa vitu ambavyo vilishikwa au kutumiwa na mwenye virusi, kama vile matandiko, nguo na taulo.
Kugusana kwa karibu na wanyama walioambukizwa, kama vile nyani, panya na Kuchakuro (squirrels), ni njia nyingine.
Wakati wa mlipuko wa kimataifa mnamo 2022, virusi vilienea zaidi kupitia mawasiliano ya ngono.
Mlipuko wa sasa wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo unasukumwa na mawasiliano ya ngono, lakini pia umepatikana katika jamii nyingine.

Ni nani aliye hatarini zaidi?​

.


Kesi nyingi mara nyingi hupatikana kwa watu wanaofanya ngono mbali na wanaume wanaofanya ngono na wanaume wenzao. Watu walio na wapenzi kadhaa au wapenzi wapya wanaweza kuwa katika hatari zaidi.
Lakini mtu yeyote ambaye ana mawasiliano ya karibu na mtu aliye na dalili anaweza kupata virusi, pamoja na wafanyakazi wa afya na wanafamilia.
Ushauri ni kuepuka kugusana kwa karibu na mtu yeyote mwenye mpox na osha mikono yako kwa sabuni na maji ikiwa virusi viko katika jamii yako.
Wale ambao wana mpox wanapaswa kujitenga na wengine hadi vidonda vyao vyote vipotee.
Mpira wa kiume unapaswa kutumika kama tahadhari wakati wa kufanya ngono kwa wiki 12 baada ya kupona, Shirika la Afya Duniani (WHO) linasema.

Je, inaweza kutibiwa?​

Tiba iliyoundwa kutibu ndui inaweza pia kuwa muhimu katika kutibu Homa ya Nyani, lakini kuna utafiti mdogo kuhusu jinsi inavyofaa.
Milipuko ya mpox inaweza kudhibitiwa kwa kuzuia maambukizi, njia bora ya kufanya hivyo ni kwa chanjo.
Kuna chanjo tatu ambazo zipo lakini ni watu walio hatarini tu au ambao wamewasiliana kwa karibu na mtu aliyeambukizwa kwa kawaida wanaweza kuipata.
WHO kwa sasa haipendekezi kuchanja watu wote.
Majaribio zaidi ya chanjo dhidi ya aina mpya za mpox yanahitajika ili kuelewa ni kiasi gani cha ulinzi kinachotoa.
chanzo. BBC
 
Watalaamu mtuambie kunakuaje na hi miingiliano mpaka inafika kwa binadamu...

Mtu wa kwanza kupata hiko kitu kwanini wase m excute tuu
 
Back
Top Bottom