Kenya kuisaidia DRC kurejesha utulivu kisiasa

miss zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
2,900
2,000
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ameeleza nia ya nchi yake kuisaidia Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC kurejesha utulivu wa kisiasa.

Kenyatta alitoa ahadi hiyo jana wakati alipokuwa na mazungumzo na mwenazake wa DRC Felix Tshisekedi mjini Nairobi. Amesisitiza kuwa Kenya imepata funzo zuri kutokana na vurugu za kisiasa zilizotokea huko nyuma, funzo ambalo Kenya iko tayari kuipatia DRC. Kenyatta amesema kwa miaka mingi wamekuwa wakiwahifadhi wakimbizi wa Kongo, ambapo baadhi yao wamekuwa raia wa nchi hiyo na kwamba nchi hizo zina mambo mengi ya kubadilishana hususan urithi wa utamaduni.

Tshisikedi aliwasili Nairobi jana ikiwa ni kituo chake cha pili kwenye ziara yake ya nchi tatu ambayo atamalizia nchini Jamhuri ya Congo na kufanya mazungumzo na rais Denis Sassou Nguesso.

Swahili cr
 
game over

JF-Expert Member
Jan 1, 2016
6,861

Unazima moto kwa Jirani na Kwako kunawaka..
imagine unategemea nchi kama Kenya ikuletee utilivu, Huku al shabaab, Huku Mungiki, Huku Polisi, huku Jubilee, huku njaa na ukabila,
 
Amigos J

JF-Expert Member
Nov 25, 2018
236
250
Nchi ya tatu ni ipi? Nilitegemea angepita tanzania ambayo ndio mkombozi wa Congo kwa masuala ya wakimbizi
Huyo rais hajielewi bado hajaa ikulu akapazoea kashaanza ziara kwenye nchi za watu ambao hawajawahi kuwa na msaada kwake na kwa bahati mbaya sanaa hawajui kama ni wanafiki wa kiwango cha lami....Ngoja kwanza azoee ikulu ndio ataijua dunia.
 
Amigos J

JF-Expert Member
Nov 25, 2018
236
250
Kongo wana bahati mbaya maana hata Tanzania waliyotegemea haina amani, ni risasi tangu bungeni mpaka kanisani.

Sent using Jamii Forums mobile app
Tanzania ndio mkombozi wao. Hao akina Uhuru Kenyatta wang'ata ulimi.....wanauma na kupuliza.....hawana misimamo....hawaeleweki.....wanachotazama ni nin utawapa sio wao watakupa nin. Ngoja kwanza atalipata joto la jiwe. Wacha kwanza azoee ikulu atamjua nan mbaya na nan mwema kwake!!
 
pingli-nywee

JF-Expert Member
Sep 16, 2015
10,762
2,000
Unazima moto kwa Jirani na Kwako kunawaka..
imagine unategemea nchi kama Kenya ikuletee utilivu, Huku al shabaab, Huku Mungiki, Huku Polisi, huku Jubilee, huku njaa na ukabila,
Kenya kuna utulivu na ukomavu wa kisiasa. Rais Uhuru Kenyatta na Raila Odinga, mpinzani wake aliyejiapisha kama rais, walipohudhuria kuapishwa kwa rais mpya wa DRC kwa pamoja ilikuwa ni picha nzuri na ya kuigwa. Zaidi ya yote kampuni za Kenya zipo active DRC, tuna mengi sana ya kushirikiana.
 
NairobiWalker

JF-Expert Member
Oct 31, 2012
5,347
2,000
Ninyi mliwahisaidia DRC lini? Huyo Tshekedi kachanganywa na Kenyatta kwenda wakat jamaa akila kiapo......hehehehehehehehehehehehe.......ndio kwanza ameupata urais. Tusubiri tuone:mad::mad::mad:
Kila siku mnajichocha humu jinsi mnaheshimika nchi za Afrika kumbe wapi. Ubaya wenu ni majivuno ya kijinga - yaani mtu tajika kutoka nchi nyingine akiishi Tanzania kwa muda mnaanza kufoka jinsi mmeikomboa hiyo nchi. Yaoneni sasa. Sisi mambo yetu tunafanya kimya kimya.
 
Bishop Hiluka

Verified Member
Aug 12, 2011
6,402
2,000
Kenya kuna utulivu na ukomavu wa kisiasa. Rais Uhuru Kenyatta na Raila Odinga, mpinzani wake aliyejiapisha kama rais, walipohudhuria kuapishwa kwa rais mpya wa DRC kwa pamoja ilikuwa ni picha nzuri na ya kuigwa. Zaidi ya yote kampuni za Kenya zipo active DRC, tuna mengi sana ya kushirikiana.
Nakubaliana na wewe lakini huoni huyu Tshisekedi alitakiwa akae kwanza ikulu aone matatizo na mahitaji ya nchi yake kwanza na kushughulikia yale yanayopaswa kushughulikiwa kabla ya kuanza kuzurura huku na kule? Kaapishwa juzi tu tayari ameanza safari, akimaliza mwaka si atakuwa amezunguka dunia nzima na kumshinda hata Vasco Dagama?... :D:D:D
 
Bishop Hiluka

Verified Member
Aug 12, 2011
6,402
2,000
Kila siku mnajichocha humu jinsi mnaheshimika nchi za Afrika kumbe wapi. Ubaya wenu ni majivuno ya kijinga - yaani mtu tajika kutoka nchi nyingine akiishi Tanzania kwa muda mnaanza kufoka jinsi mmeikomboa hiyo nchi. Yaoneni sasa. Sisi mambo yetu tunafanya kimya kimya.
Hahahaa, kutesa kwa zamu. Zamu yenu sasa kufaidi dhahabu za DR Congo, msiipoteze hii fursa... :D:D:D
 
pingli-nywee

JF-Expert Member
Sep 16, 2015
10,762
2,000
Nakubaliana na wewe lakini huoni huyu Tshisekedi alitakiwa akae kwanza ikulu aone matatizo na mahitaji ya nchi yake kwanza na kushughulikia yale yanayopaswa kushughulikiwa kabla ya kuanza kuzurura huku na kule? Kaapishwa juzi tu tayari ameanza safari, akimaliza mwaka si atakuwa amezunguka dunia nzima na kumshinda hata Vasco Dagama?... :D:D:D
Anahitaji sana huo ushirikiano na Kenya, ndio maana unamuona akiruka ruka. :D Baneni matumizi pekee yenu bana msitupangie tafadhali.
 
makaveli10

JF-Expert Member
Mar 27, 2013
15,058
2,000
Matatizo ya congo anayajua kabla hajawa raisi, si lazima ukae ikulu ya tz ndio ujue matatizo yake, km ni mtu wa kushughulikia atashughulikia huenda hata hizi safar zake ndio anatafta ufumbuzi wa baadhi ya matatizo ya wakongo mkuu, kuhusu kuchagua hizo nchi tatu huenda kwa maono yake na washauri wake wameona hao watu watakuwa msaada mkubwa kwao.
Nakubaliana na wewe lakini huoni huyu Tshisekedi alitakiwa akae kwanza ikulu aone matatizo na mahitaji ya nchi yake kwanza na kushughulikia yale yanayopaswa kushughulikiwa kabla ya kuanza kuzurura huku na kule? Kaapishwa juzi tu tayari ameanza safari, akimaliza mwaka si atakuwa amezunguka dunia nzima na kumshinda hata Vasco Dagama?... :D:D:D
Sent using Jamii Forums mobile app
 
MK254

JF-Expert Member
May 11, 2013
19,462
2,000
Unazima moto kwa Jirani na Kwako kunawaka..
imagine unategemea nchi kama Kenya ikuletee utilivu, Huku al shabaab, Huku Mungiki, Huku Polisi, huku Jubilee, huku njaa na ukabila,
Kuna video nimeona ya wabunge wenu wakitimua mbio kisa king'ora cha tahadhari kimelia, hehehe haijawahi kutokea duniani, yaani kwenu mnavunja rekodi.
Mara muwachinje watoto, mara mabilionea watekwe, wabunge walishwe marisasi na watu wasiojulikana...
 
mkorinto

JF-Expert Member
Jun 11, 2014
17,444
2,000
Kuna video nimeona ya wabunge wenu wakitimua mbio kisa king'ora cha tahadhari kimelia, hehehe haijawahi kutokea duniani, yaani kwenu mnavunja rekodi.
Mara muwachinje watoto, mara mabilionea watekwe, wabunge walishwe marisasi na watu wasiojulikana...
USA wamewaambia nini raia wake wanao visit tz kuhusu hii video uliyoiona!!!!
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom