Kenya kuchunguza ukweli wa raia wake kumteka ulimboka. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kenya kuchunguza ukweli wa raia wake kumteka ulimboka.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mohamedi Mtoi, Jul 15, 2012.

 1. Mohamedi Mtoi

  Mohamedi Mtoi R I P

  #1
  Jul 15, 2012
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 3,326
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 0
  SERIKALI ya Kenya imesema inazifanyia kazi taarifa za raia wake kukamatwa na
  kufikishwa kortini nchini kwa tuhuma za kumteka na kufanya jaribio la kumuua Mwenyekiti wa
  Jumuiya ya Madaktari
  Tanzania, Dk Steven
  Ulimboka.

  Hatua hiyo imekuja siku moja baada ya Jeshi la Polisi kutangaza kukamatwa na kufikishwa mahakamani kwa raia wa Kenya, Joshua Mulundi anayetuhumiwa kuhusika na tukio la kumteka, kumpiga na kumtupa Dk
  Ulimboka katika Pori la Akiba la Pande nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam hivi karibuni.

  Balozi wa Kenya nchini, Mutinda Mutiso, alisema
  kwa njia ya simu jijini Dar es Salaam jana kuwa Serikali yake itachunguza uraia na tuhuma zinazomkabili mtu huyo ili kubaini ukweli.

  “Ndiyo kwanza nimewasili kutoka nje ya nchi…, nitafuatilia kwa makini kupata taarifa sahihi kutoka kwenye vyanzo sahihi na mamlaka husika
  za hapa Tanzania na Kenya ili kupata taarifa ya kweli,”
  alisema Balozi Mutiso na kuongeza: “Siwezi kueleza zaidi kwa sasa kwani itakuwa naeleza uvumi.”

  Chanzo: makinika.
   
 2. Daniel Anderson

  Daniel Anderson JF-Expert Member

  #2
  Jul 15, 2012
  Joined: Aug 7, 2011
  Messages: 879
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  wakenya hawana lonolongo, kama hata uraia wamechakachua jamaa atawaumbua tu. Nawaamini sana kwenye ukweli na uadilifu
   
 3. Nyakageni

  Nyakageni JF-Expert Member

  #3
  Jul 15, 2012
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 13,957
  Likes Received: 1,283
  Trophy Points: 280
  Gwajima kashamaliza. Watajibeba
   
 4. Gajungi

  Gajungi Senior Member

  #4
  Jul 15, 2012
  Joined: Sep 4, 2011
  Messages: 195
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Siku ya ufa nyani miti yote inateleza
   
 5. Gajungi

  Gajungi Senior Member

  #5
  Jul 15, 2012
  Joined: Sep 4, 2011
  Messages: 195
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Siku ya kufa nyani miti yote inateleza
   
 6. s

  sheky Senior Member

  #6
  Jul 15, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 188
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Maelezo ya Kova yalikuwa na kusita sita na kutokuwa na uhakika wa maelezo kama Kamanda kweli. inaonekana kama imepikwa, labda kijana kaambiwa jitose na tutakutunza... Haya sasa Kenya kazi kwenu ama mkae kimya kuwa huyu jambazi wenu au muweke mambo hadharani kulinda hadhi ya Taifa. Na ikiwa ni kweli ni wa huko wala msijikanyage, wekeni mambo hadharani maana hata huko mnao wahalifu.
   
 7. R

  RC. JF-Expert Member

  #7
  Jul 16, 2012
  Joined: May 24, 2012
  Messages: 446
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  wasije nao wakatumiwa na kova!
   
 8. M

  MADORO Senior Member

  #8
  Jul 16, 2012
  Joined: Nov 12, 2011
  Messages: 199
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Jeshi la polisi nchini liache dharau. Kova hawezi kuja kutuambia sisi watanzania eti kuna mtuhumiwa amekamatwa, mtu ambaye hatujaonyeshwa picha zake, alipelekwa mahakamani kwa siri, tena kwa kutegemea ushahidi wa maungamo ya Kanisani ambayo hata mchungaji amekana kutokea kwa tukio hilo. Kova ana akili timamu kweli? anajua kuwa watanzania tunafikiri? nini lengo lake? Tuelezeni Dr. Ulimboka aliteswa na nani?
   
 9. k

  kiliochangu JF-Expert Member

  #9
  Jul 16, 2012
  Joined: Feb 23, 2012
  Messages: 1,122
  Likes Received: 774
  Trophy Points: 280

  Kazi ipo. Mtoa tukio nadhani kuna ulakini. Inawezekanaje mtu akaingia Tanzania siku hiyo hiyo na akafanya ualifu kama huo. kwani amedai hakumbuki hotel aliyofikia akidai ipo katikati ya jiji. Amejuaje msitu wa Makupande (eneo linalofanyika matukio ya ajabu) huku akiwa ni mgeni. Kama alikuja kwa ajili ya kutekeleza tukio, kilichombakiza nini hasa. Huko alikotoka hakuna sehemu za kutubu. Muda mrefu umepita tangu tukio, anafahamu wazi pitia hata vyombo vya habari kuwa uchunguzi unafanyika kuwatafuta wahusika, then aende akaconfess kirahisi hiyo.
  Watanzania sio wajinga. Ila waliosuka huu mkanda wanaonekana kuwa na ulakini hata katika mafunzo yao katika fani.
   
 10. NAFIKA

  NAFIKA Senior Member

  #10
  Jul 16, 2012
  Joined: Dec 3, 2011
  Messages: 125
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  That is just the beggining of the beggining!! Siku si nyingi mtaambiwa huyo jamaa ni alshababu, na alikuja kumwadhibu alshababu mwenzie sababu kuna dili hakulitekeleza!! Hii ndio Tanzania watch and see!!
   
 11. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #11
  Jul 16, 2012
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,355
  Likes Received: 22,220
  Trophy Points: 280
  Jeshi letu la polisi ni zaidi ya legelege
   
Loading...