G Sam
JF-Expert Member
- Apr 20, 2013
- 11,555
- 35,880
Nchi yetu ni lazima iheshimiwe nje ya mipaka yetu. Kutumia vyanzo vya mapato vya nchi nyingine ili kujipatia mapato kwenye nchi nyingine ni uharamia na kama nchi yenye uhuru wake haitakiwi kamwe kulea hilo!
Marekani haiwezi kuivumilia nchi ya Russia pale itakapo jaribu kutumia vyanzo vyake muhimu vya mapato kiulaghai ili kujipatia kipato, vivyo hivyo kwa Russia na nchi nyingine yoyote ile!
Kenya imekuwa na tabia mbaya ya kuutumia mlima Kilimanjaro ambao kihalali upo Tanzania ili kujipatia watalii na kuongeza mapato ya nchi yao! Huu ni uharamia! Sheria za kimataifa haziruhusu hilo! Wamekuwa wakithubutu hata kutumia vivutio vyetu vingine vya utalii kuendelea kujipatia mapato, kama nchi hatupaswi kuvumilia jambo hilo.
Serikali yetu imekuwa kimya kuhusu hilo huku nchi ikidhulumiwa kwa namna moja ama nyingine! Tunatoa rai kwa serikali kamwe jambo hili lisiendelee kwani waswahili wanasema "ukimchekea mbwa atakufuata hadi msikitini" tujue kuwa jambo hili linadumaza uhuru wa nchi yetu na kutupotezea mapato halali!
Mods naomba musahihishe title kwenye "mzima" pasomeke "mlima"
Samahani sana kwa usumbufu!