Kenya inaelekea kwa wimbi la pili la virusi vya corona

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,001
9,862
Waziri wa Afya Kenya Mutahi Kagwe


Waziri wa Afya nchini Kenya Mutahi Kagwe amethibitisha kuwa watu 685 wameambukizwa virusi vya corona ndani ya saa 24 huku idadi jumla ya walioambukizwa kufikia sasa ikiwa 44,881.

Akiwa anatoa taarifa kuhusu ugonjwa wa virusi nchini humo, Waziri Kagwe amesema kuwa maambukizi ya sasa hivi yameongezeka kwa asilimia 12 ikilinganishwa na asilimia 4 wakati Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya alipotangaza kulegezwa kwa masharti kidogo na kufunguliwa kwa uchumi.

Watu 635 ni raia wa Kenya huku 50 wakiwa raia wa kigeni.

"Kati ya walioambukizwa, 456 ni wanaume huku 229 wakiwa wanawake mdogo kabisa akiwa na umri wa mwaka mmoja na wa umri wa juu akiwa na miaka 99," Kagwe amesema.
Kagwe pia amesema kuna wasiwasi kuhusiana na idadi ya wanaopelekwa katika vyumba vya wagonjwa mahututi ambayo sasa hivi imefikiwa wagonjwa 28.

"Kwa muelekeo huu, bila shaka Kenya inaelekea kwa wimbi la pili la virusi vya corona'', Waziri Kagwe amesema.

Bwana Kagwe ameweka wazi kwamba ikiwa wananchi watashindwa kufuatilia kanuni zilizowekwa kukabiliana na virusi vya corona hali huenda ikawa mbaya zaidi.
Idadi ya leo ni ya juu tangu kuanza kuonekana kana kwamba maambukizi ya virusi hivyo yameanza kushuka nchini Kenya.
 
Back
Top Bottom