Kenya imetoa picha gani kwa kuiruhusu Tanzania na kuiacha nje Somalia?

joto la jiwe

JF-Expert Member
Sep 4, 2017
17,375
2,000
Wadau, mtakumbuka kwamba Kenya ilizuia raia wa Tanzania na Somalia kuingia Kenya kama jitihada za kuwakinga wakenya dhidi ya maambukizi ya Corona.

Wakenya wanaamini kwamba Somalia na Tanzania zina idadi kubwa ya maambukizi kwasababu tofauti, wakati wakidai Somalia iko na machafuko ya ndani yanayozuia kufanikisha mapambano ya Corona kuwa na ufanisi, Tanzania inalaumiwa kwa kutochukua hatua zozote za kupambana na Corona Kama ambavyo Kenya na nchi zingine zilivyofanya.

Kitendo cha Kenya kuirudisha Tanzania katika orodha ya nchi salama/ zenye kiwango kidogo cha maambukizi ya Corona bila kuirudisha Somalia, wakati Tanzania haijafanya lolote tofauti linaloweza kutumika kama kigezo cha kuirudisha, hii ni ishara gani?, kwanini Kenya isingezirudisha nchi zote mbili kwa pamoja? Ujirani na mahusiano ya kikanda yatakuwaje?
 
pingli-nywee

JF-Expert Member
Sep 16, 2015
10,856
2,000
Hongereni kwa ustaarabu wenu wa kuwaza pia kuhusu feelings za wake wenza wenu. Tunawapenda wote, ila heshima ya mke wa kwanza itabaki kwa kipenzi chetu cha kwanza, Uganda.
 
luangalila

JF-Expert Member
Jan 12, 2014
2,150
2,000
joto la jiwe Tz ili react na kujitutumua kwamba na yy ana wadhifa wake thats why ikabidi wasalimu amri lkn pia nafikir kwa kiasi kikubwa business factor ime changia coz tuliona baadhi ya vyama vya wafanya biashara waki laumu uamuzi ule. Lkn pasipo ubishi now days muingiliano wa mataifa haya mawili ni mkubwa pia kijamii sasa iv kuna jamii nyingi wamezaliana baina ya watu wa mataifa haya mawili
 
Sina tatizo na Kenya kuiruhusu Tanzania kwasababu hapakua na sababu zozote za msingi za kuifungia Tanzania, kitendo cha kuirudishe Tanzania ni sahihi kwasababu ulizozitaja na muhimi zaidi ni kurekebisha mahusiano ya ujirani.

Kama ilivyokua kwa Tanzania, hata Somalia hali ni hiyohiyo, Kenya ilipaswa kuirudisha Somalia siku ileile ilipoirudisha Tanzania, kwasababu hali ya Corona Somalia ni nzuri kuliko nchi nyingi ambazo Kenya imeziruhusu. Kumbuka Somalia na Kenya wameingiliana zaidi ya Tanzania na Kenya.

Picha inayojionyesha ni kwamba Kenya inabagua jirani zake, au inamdharau Somalia na kuithamini Tanzania zaidi, au Kenya inaiogopa Tanzania, dhana zote hizi sio nzuri kwa nchi ya Kenya, ingezifungulia nchi zote mbili kwa wakati mmoja, Hakuna dhana yotote kati ya hizo ingejitokeza na Kenya isingeathirika kivyovyote vile kwa kuiingiza Somalia.

Sent from my TECNO-L8 using JamiiForums mobile app
 
chongchung

JF-Expert Member
Jun 23, 2013
3,794
2,000
joto la jiwe Tz ili react na kujitutumua kwamba na yy ana wadhifa wake thats why ikabidi wasalimu amri lkn pia nafikir kwa kiasi kikubwa business factor ime changia coz tuliona baadhi ya vyama vya wafanya biashara waki laumu uamuzi ule. Lkn pasipo ubishi now days muingiliano wa mataifa haya mawili ni mkubwa pia kijamii sasa iv kuna jamii nyingi wamezaliana baina ya watu wa mataifa haya mawili
Kuhusu kijamii kati ya Tanzania na Somalia Hakuna nchi yenye mahusiano ya ndani na kina ya kijamii kama Somalia na Kenya, in fact kuna wa Somali wengi sana Kenya nafikiri hata idadi mara 5000 ya watanzania Kenya, hivyo kama ni kijamii Kenya na Somali wapo karibu kijamii kuliko Tanzania na Kenya
 
komora096

JF-Expert Member
Sep 26, 2018
11,986
2,000
Tanzania ni mke wetu, unamtibua akianza kununa nuna unaamua kulegeza kiasi unakuta mwnywe anajiachia na kushau yaliyopita..
Sasa msijali kuhusu somali
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom