Kenya imebaki na wasanii makinikia

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,633
697,529
Wakati huo ikijulikana kama talented country katika uwanja mzima wa sanaa kuanzia nyimbo maigizo vichekesho mpaka kutengeneza vipindi mbalimbali Tanzania na wengineo tulikuwa nyuma kwakweli

Tusizungumzie mbali sana nyakati zile za zilipendwa ambazo mpaka leo zinahit, tuzungumzie tu miongo miwili iliyopita... Enzi za vituko mahakamani, mzee mgongoo, mama kayaii, Mwalla, Mzee Ojwang na wengine wengi waliocheza na kuvaa uhusika kamili kwenye nafasi zao

Kwenye tungo za kisasa wakaibuka kina Nyota ndogo -Nibebe, Benjamin huyu dogo aliyeimba Nchi ya kitu kidogo, bush baby? Tungo zile ziliimbika na zilikuwa na ujumbe wenye hisia

Leo hii Kenya wamebaki wabana pia, wanaojipodoa na kuvaa hereni, na kuigiza kike. Bila kuwa na ujumbe wowote wa maana.... Kweli kila zama na vitabu vyake

93592bfee511c23afa59f9fbde5dff5f.jpg
9a2e765a104069bb346bb4ad1aecff78.jpg
 
Waliposhika Soko la Bongo wakabweteka, Wasanii wa Bongo walipojitambua ndo wakaanza kuwasomesha Namba hadi ss wamepoteana!
 
Kina chokoraa , kina mama kayayii, mzee ojwang, othorong'ong'o , kina karumanzira , mwala na wengineo , kwakweli walibamba sana
 
Tasnia ya sanaa hasa uigizaji kotekote Tanzania na Kenya imekufa. Huu utandawazi wa 'slay queens' na 'socialites' umeua kabisa sekta hiyo.

Pesa..ngono..umaarufu.
 
Back
Top Bottom