Kenya: Hospitali za kibinafsi kujiunga kwenye mgomo Kenya

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,397
_92883791_cd88adc2-c7a3-4786-9ce6-48c10ccd1efa.jpg

Chama cha madaktari nchini Kenya kimetangaza kuwa hospitali zote zikiwemo za kibinafsi zitagoma kwa saa 24 siku ya Jumanne tarahe 13 mwezi huu, ikiwa serikali itashindwa kutekeleza makubaliano ya kuimarisha mishahara ta wafanyakazi wa sekta ya afya na mazingira yao ya kufanya kazi.

Mgomo huo uanoadhiri hospitali zote za umma kwa sasa uko siku yake na nne, baada ya serikali kushindwa kutekeleleza mkatana wa mwaka 2013 wa kuwapa madaktari nyongeza ya mshara ya asilimia 300.

Afisa mmoja wa chama cha madaktari Ouma Oluga, amesema kuwa madaktari kutoka hospitali kuu ya Kenyatta wamejiunga kwenye mgomo huo na kusitisha huduma zao tangu Jumatatu.

Chama cha madaktari kinasema kuwa kimejiondoa kutoka kwa mazungumzo yoyote na serikali na watarudi tu mezani kujadili njia ya kutekelezwa kwa makubaliano yao.

Makubaliano hayo yaliyoafikiwa mwaka 2013 yaliitaka serikali kuajiri madaktari zaidi na kuboresha vituo vya afya, makubaliano ambayo madaktari wanasema kuwa hajajatekelezwa.

Chanzo: BBC
 
Falcon Mombasa.badala ukae ujadili matatizo ya nchi yenu.unajadili kibao.kinachoelekeza mlima Kilimanjaro.
 
Wakenya nawakubali sana kwa kusimamia kile wanachokiamini

Ni kweli kabisa. Kuanzia walimu, madaktari, wakulima na kila kundi wanajitambua sana. WaTZ tuko nyuma miaka mil1 katika hilo. Na niandhani wataendelea sana maana kujitambua ni hatua kubwa sana katika kupiga hatua mbele
 
Hapa kwetu tunalo la kujifunza kutoka kwa hawa wenzetu. Nadhani inatakiwa serikali ijipanga sio mpaka kusubiri haya mashinikizo huwa yanaumiza watu sana haya
 
Back
Top Bottom