Kenya Election 2007: Outcomes

oneni jinsi wakenya wanavyoendelea kuchinjana kwa mujibu wa bbc leo

Watu kumi na wawili wameuawa baada ya kupigwa risasi na wengine kuchomwa wakiwa hai kufuatia mgogoro wa mashamba katika eneo la Mlima Elgon magharibi mwa Kenya.
Kwa mujibu wa msemaji wa polisi, Eric Kiraithe jumla ya nyumba kumi na baadhi ya hizo zikiwa na watu zilitekezwa katika shambulio hilo.

Haijabainika wazi ikiwa mapigano hayo yaliyotokea usiku yanahusiana na mapigano yaliyosababishwa na uchaguzi wa mwaka jana ambapo machafuko yaliyofuatia yalisababisha vifo vya watu 1500.

Pande zote mbili kutoka serikalini na upinzani zimesaini mkataba wa kumaliza mgogoro huo uliozuka kufuatia utata juu ya matokeo ya urais.

Mke na watoto wachomwa

Mkazi mmoja wa eneo hilo, Rabson Mbuya alisema mkewe, watoto wao watatu na mfanyakazi wa nyumbani ni kati ya wale waliouliwa.

Rabson alieleza jinsi watu walipopiga hodi nyumbani kwake katika kijiji cha Embaskasi karibu na Mlima Elgon.

"Mmoja wao alimwagilia petroli kwenye paa la nyumba kabla ya kuiwasha moto."

"Nilimsikia mke wangu pamoja na watoto wakipiga nduru lakini sikuwa na njia yoyote ya kuwanusuru."

Rabson pia alieleza jinsi alishuhudia mvulana wa miaka mitatu akichinjwa wakati alipokuwa akitoroka nyumbani kwao.

HABARI MPYA
Democrats Marekani wasubiri matokeo leo.
Marekani yashambulia Somalia
Wauawa katika mgogoro wa ardhi Kenya
(none)

Mtumie rafiki barua pepe Chapisha

Idhaa Yetu | Wasiliana Nasi
 
Hii ishu sio fahari na kama unalijua swala la Mt Elgon
ungejizuia kabla hujasema "....angalia wakenya wanavyoendelea
kuchinjana!"
 
Back
Top Bottom