KENYA: Dawa Aina ya Misoprostol Yaweza Kuwa Mkombozi wa Wanawake Wajawazito | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

KENYA: Dawa Aina ya Misoprostol Yaweza Kuwa Mkombozi wa Wanawake Wajawazito

Discussion in 'JF Doctor' started by MziziMkavu, Mar 7, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Mar 7, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,212
  Likes Received: 4,010
  Trophy Points: 280
  Dawa Aina ya Misoprostol Yaweza Kuwa Mkombozi wa Wanawake Wajawazito Susan Anyangu-Amu

  Precious Nabwire alikaribia kufariki dunia kutokana na kujifungua mtoto wake wa nne. Kama wataalam wa magonjwa ya akina mama wa Kenya wangefika, dawa ya kuzuia kutokwa na damu kwa wingi baada ya kujifungua mtoto ingepatiwa kibali, ingeweza kutoa ulinzi kwa makumi kwa maelfu ya wanawake wanaokabiliwa na hatari hiyo.

  NAIROBI, Agosti 4 (IPS) -
  Binti yake – kwa jina la Chausiku, kutokana na kuzaliwa wakati wa usiku wa manane – alizaliwa nyumbani kwa Nabwire.

  "Uchungu ulianza usiku na kwenda hospitali ya wazazi ya Pumwani ni suala mbalo lisingewezekana kutokana na kwamba ningetakiwa kutumia teksi na hii ingegharimu kiasi kikubwa cha shilingi za Kenya 1,000 (dola za Kimarekani 12.50.)," Nabwire anakumbuka.

  Alipelekwa kwa mkunga wa jadi ambaye aliishi karibu. Nabwire ana uhakika kujifungua kwake kungekuwa kwa kawaida kama ilivyokuwa kwa watoto wake watatu wa kwanza.

  "Nilikuwa nimekosea. Uchungu, kama ulivyotabiriwa, ulichukua muda mfupi lakini kondo la nyuma halikutoka na hivyo kuanza kupata maumivu makali lakini TBA alinihakikishia mara tu kondo la nyuma litakapotoka maumivu yangepungua," Nabwire anasema.

  Dakika ishirini baadaye, alikuwa akiugulia kwa maumivu, ambayo alisema yalikuwa makali zaidi ya uchunguz wa kuzaa. Alikuwa akitokwa na damu kwa wingi na kuangaliwa na mkunga wa jadi hakukumsaidia kitu.

  "Kwa bahati kondo la nyuma lilitoka na damu iliacha kutoka. Niliweza kusubiri hadi asubuhi kabla ya kwenda hospitali. Hata hivyo, hadi ilipofika siku iliyofuata nilikuwa dhaifu mno na ilibidi kulazwa hospitalini kwa wiki moja."

  Postpartum haemorrhage – kitendo cha kutokwa na damu nyingi baada ya kujifungua – ni moja ya sababu kuu tano zinazosababisha vifo vya uzazi nchini Kenya. Katika Afrika nzima, inasababisha theluthi nzima ya vifo vya uzazi, kulingana na takwimu za USAID.

  Chama cha Madaktari wa Akina Mama na Uzazi nchini Kenya (KOGS) kinashinikiza kusajiliwa kwa dawa inayojulikana kama misoprostol, ambayo jina lake la biashara ni Cytotec, ambayo wanasema inaweza kudhibiti kikamilifu kitendo cha postpartum haemorrhage, hasa katika mazingira yenye rasilimali chache.

  Kulingana na utafiti wa hali ya afya wa taifa uliofanyika kwa mara ya mwisho na kutolewa mwaka 2009, asilimia 57 ya wanawake nchini Kenya wanajifungua nyumbani. Mtaalam wa magonjwa ya wanawake na uzazi Dk Omondi Ogutu aliiambia IPS kuwa dawa aina ya misoprostol ambayo inapatikana katika vituo vya afya, inasaidia kuokoa maisha ya mamilioni ya wanawake.

  "Kwa sasa misoprostol imesajiliwa kwa ajili ya kutibu vidonda vya tumbo lakini tunashinikiza kuwa na sera ili matumizi yake yapanuliwe kuruhusu kutumika kwa ajili ya masuala ya uzazi. Dawa hii ambayo haiuzwi kwa bei ya juu ambayo inapatikana kwa wingi katika maduka ya rejareja kwa kiasi cha shilingi 240 (kama dola 3) itasaidia kuokoa maisha ya wanawake wengi ambao hufariki kutokana na kutokwa na damu nyingi baada ya kujifungua au kutokana na utoaji mimba usiuokuwa salama," Ogutu alisema.

  Dk Joachim Osur, mtaalam wa afya ya uzazi katika shirika la Ipas (asasi isiyokuwa ya kiserikali inayohusika na kulinda afya ya wanawake), anasema asilimia 20 ya vifo vya uzazi nchini Kenya inahusika moja kwa moja na kutokwa na damu nyingi baada ya kujifungua. Kushindwa kutoa kondo la nyuma kama kwa tukio la Nabwire mara nyingi kunasababisha kifo.

  Utafiti uliofanywa kuhusu usalama na ufanisi wa misoprostol umeonyesha kuwa inasitisha kutokwa na damu mara moja wakati huo huo ikisaidia kutoka kwa kondo la nyuma.

  "Misoprostol ni dawa yenye ufanisi mkubwa; hata hivyo, utata unaozunguka matumizi yake kwa watu wanaotoa mimba umezingira kuaminika kwake," anasema Osur. "Wale wanaolenga kutumia kama dawa ya kutoa mimba wanakosea na wanasababisha wanawake wa nchi hii kukosa faida zake nyingi."

  Hofu ya wale wanaosita kutengeneza madawa hayo ambayo inapatikana kwa wingi inaelezewa na uzoefu wa Namibia, ambapo misoprostol inajulikana zaidi kwa kutoa mimba.

  Kama ilivyo kwa Kenya, utoaji mimba nchini Namibia unaruhusiwa kwa watu waliobakwa, waliofanya mapenzi ya ndugu au wakati maisha ya mwanamke yanapokuwa hatarini. Osur anaonya kuwa sheria inayokataza kutoa mimba inafanya kazi ndogo mno kuzuia wanawake wasifanye hivyo. Wastani wa wanawake 800 wanakufa kutokana na utoaji wa mimba usioruhusiwa kila siku nchini Kenya; wengi wakifariki kutokana na kutokwa na damu nyingi ambapo dawa hiyo ingeweza kuzuia.

  "Hatuna sera inayozunguka matumizi ya dawa ya misoprostol kutokana na kwamba wale waliopo katika wizara ya afya ambao wanatakiwa kutunga sera wanajikita zaidi katika suala la utoaji wa mimba. Hofu ni kwamba misoprostol haitatumiwa vizuri katika utoaji wa mimba," Osur anaelezea.

  Anasema kuwa wizara ya afya inatakiwa kuja na mwongozo unaopanua matumizi yaliyopitishwa ya dawa hiyo wakati huo huo ikihakikisha inapatikana tu katika vituo vya afya, ikiwa ni pamoja na kliniki za jamii ambako mahitaji ni makubwa zaidi.

  "Kutokana na udhibiti wa matumizi, dawa hii siyo lazima kutumiwa vibaya. Ukweli ni kama mwanamke ambaye amejifungua anatumia dawa hii hana hatari ya kutokwa na damu hadi kufa. Hii itakuwa na faida kubwa kwa wanawake katika maeneo ya mbali ambao hufariki wakiwa njiani kutoka vituo vidogo vya afya kwenda hospitali kuu kwa ajili ya kupata tiba," Osur anasema.

  Mwezi Februari, Nigeria ilikuwa nchi ya kwanza Afrika kusajili misoprostol kwa ajili ya matumizi ya uzazi. Hata hivyo, serikali ilizuia matumizi yake kwa wataalam wenye elimu katika vituo vya afya, kutokana na asilimia 75 ya wanawake kujifungulia nyumbani chini ya wakunga wa jadi.

  Wanaharakati wanasisitiza kuwa dawa hiyo ipatikane kwa bei nafuu katika ngazi ya chini zaidi kwenye mfumo wa afya ya umma, ili iweze kuwa na faida kubwa zaidi ya kupunguza vifo vya uzazi.

  Misoprostol inaweza kutumika kukata damu kwa mwanamke ambaye mimba imetoka; pia inatumika kuzuia kutokwa na damu baada ya kujifungua. Mtaalam wa uzazi Joachim Osur anasema dawa hiyo inauzwa bei nafuu na hivyo kuwa chaguo bora kwa tiba kuliko upasuaji.

  Dawa hiyo inaweza kutumika kuchochea uchungu wakati mwanamke akiwa ameshapitisha muda wake wa kujifungua au mtoto anapokuwa amechoka. Katika hali ambapo mimba lazima itolewe kuokoa maisha ya mama, misoprostol pia ni salama na rahisi badala ya upasuaji.

  Osur anasema misoprostol inaweza pia kupanua fupanyonga wakati madaktari wanapotaka kumchunguza mama mjamzito

  source.
  KENYA: Dawa Aina ya Misoprostol Yaweza Kuwa Mkombozi wa Wanawake Wajawazito
   
Loading...