Timu kadhaa zilizoshiriki Senior Challenge Cup huko Kenya, ikiwemo Zanzibar Heroes, zimekwama kwa siku kadhaa zikisota nchini humo hata baada ya kutolewa mashindanoni. Kutokana na sintofahamu hiyo, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar leo imeingilia kati na kuwarudisha mashujaa wake kwa ndege ya kukodi baada ya kuchoshwa na danadana za wenyeji kupitia Shirikisho lao la soka-FKF. Kwa kuzongwa na hasira, viongozi wa Chama cha Soka Zanzibar (ZFA) wamesita kutoa kauli leo kwa kuhofia kukurupuka na kauli inayoweza kuvuruga uhusiano wa nchi!
Source: Radio One Stereo (7:30 p.m. Sports Programme)
Source: Radio One Stereo (7:30 p.m. Sports Programme)