Kenya: Afisa wa jeshi afariki baada ya kuumwa na mpenziye

Ikaria

Member
Jul 17, 2019
71
195
Afisa mmoja wa Jeshi la ulinzi KDF Kenya(umri 37) ameaga dunia baada ya kuumwa mara tatu na mpenziye Violet Asale (umri 27).

Idara ya upelelezi DCI imesema kwamba marehemu aliumwa mara tatu; yaani kwenye kidole, kifua na bega baada ya wawili hao kutofautiana usiku katika mtaa wa Kahawa Wendani ilioko katika barabara ya Thika.

Baada ya kugundua kuwa mpenziye ameumia, Violet alimkimbiza katika hospitali ya Kahawa Garrison lakini kwa bahati mbaya marehemu akafia njiani.

Violet Asale anashikiliwa na maafisa wa polisi huku uchunguzi wa maiti ya mpenziye ukitarajiwa kufanyika hapo kesho.
 
Unag'atwa na binadamu mpaka unakufa. Hayo ni meno au ana sumu?
 
kenyan ni wapuuzi
imagine mtu anavaa barakoa siku nzima halafu anang'atwa na mkewe kisha anakufa
Sasa wewe shangaa mtu anapiga nyungu kila siku ya wiki. Hadi anapanda mparachichi kuvuna matawi ya juu kabisa ili ayatie humo humo kwenye nyungu. Alafu baada ya ukinjeketile wote huo unasikia eti alikufa, kisa, matatizo ya kupumua.
 
Wanajeshi wa Kenya wamelainika sana,yani amekufa kwa kung'atwa na meno ya bibiyake?
 
Afisa mmoja wa Jeshi la ulinzi KDF Kenya(umri 37) ameaga dunia baada ya kuumwa mara tatu na mpenziye Violet Asale (umri 27).

Idara ya upelelezi DCI imesema kwamba marehemu aliumwa mara tatu; yaani kwenye kidole, kifua na bega baada ya wawili hao kutofautiana usiku katika mtaa wa Kahawa Wendani ilioko katika barabara ya Thika.

Baada ya kugundua kuwa mpenziye ameumia, Violet alimkimbiza katika hospitali ya Kahawa Garrison lakini kwa bahati mbaya marehemu akafia njiani.

Violet Asale anashikiliwa na maafisa wa polisi huku uchunguzi wa maiti ya mpenziye ukitarajiwa kufanyika hapo kesho.

Huyu ndiye Violet Asale. Binti aliyeng'ata mpenziye akafa jana.

achzian_1617600973819272.jpg
 
Back
Top Bottom