Kichuguu
Platinum Member
- Oct 11, 2006
- 15,555
- 19,427
Dah! ya zamani sana hiyo mkuu; niliinunua moja kama hiyo hiyo e-bay mwaka 1997 (yaani ilikuwa imeshatumika pia). Baada ya kuitumia miaka kumi nikaitoa msaada kwenye charity mwaka 2007. Ilikuwa inatoa sauti nzuri sana ila sasa ilikuwa pia imepitwa sana na wakati. Maboksi yalikuwa mengi na waya nyingi za kuyaunganisha zilikuwa ni nyingi sana: Tuner, Graphic Equalizer, Cassete Player, CD Player, Stereo Amplifier. Halafu maboksi hayo mengine yalikuwa yamepitwa sana na wakati kipindi hicho (2007), kwa mfano Casette Player, CD Player, Graphic Equalizer na Stereo Amplifier ni vitu vya kizamani.