Kenneth Mwaisabula: ‘Amasha’ jina langu la soka enzi zangu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kenneth Mwaisabula: ‘Amasha’ jina langu la soka enzi zangu

Discussion in 'Sports' started by nngu007, Jun 27, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Jun 27, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  [TABLE]
  [TR]
  [TD="bgcolor: #ffffff"][TABLE]
  [TR]
  [TD]  Kenneth Mwaisabula
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [TD="width: 140, bgcolor: #ffffff"] [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD][TABLE]
  [TR]
  [TD]
  KABLA ya kuanza makala yangu leo, yenye kichwa cha habari kinachosema ‘Amasha’ jina langu la soka utotoni’. Kwanza niwapongeze wapenzi wote wa Kona ya Mwaisabula na gazeti hili kwa ujumla wake, kwa kuiona tena Jumatatu nyingine, mkiwa na afya njema na ninawaombea kwa Mungu wale wote ambao afya zao sio nzuri wapone haraka, ili tulisukume gurudumu letu kwa pamoja.
  Awali ya yote, ni lazima nikiri kuwa, sasa kalamu ya waandishi imeanza kuwafikia wadau wa michezo nchini na taratibu sasa wanajua mbivu na mbichi.
  Nilitegemea makala yangu ya wiki iliyopita, nigepata adha kubwa kama niliyoipata miaka miwili iliyopita nilipoandika: ‘Makocha wazawa wakiwezeshwa wanaweza.’
  Lakini kinyume na hapo, wengi wameniunga mkono kuwa sasa Wazungu basi, tuwape shule kina Kanakamfumu, Julio, Marsh, Mwasamaki, Adolf na wengineo.

  Baadhi ya wadau, walifika mbali zaidi na kusema, tatizo ni mfumo na si Wazungu na kama Wazungu mali, basi kwanini wasiwe Ikulu na baraza lote la Mawaziri likawa Wazungu watupu?
  Huo ni mfano mmoja tu, katika mingi niliyopigiwa simu na mingine katika barua pepe yangu, lakini mwingine ni ndugu yangu yuko hapo mjini Kibaha mkoa wa Pwani, yeye anasema ni kweli imefika wakati, makocha wazawa kupewa kipaumbele katika kupewa mafunzo, lakini aliwaasa kuwa haiba nayo ni muhimu kwao, alitoa mfano wa Fabio Capello alimnyang’anya unahodha John Terry kwa mambo ya nje na si ya uwanjani, kwa hiyo kuna wakati kocha kama Jamhuri Kihwelu ‘Julio’ anaponzwa na tabia zake za kusema na mambo ya nje na si suala la ufundishaji, huyo ni Ndugu Mapunda.
  Basi tuachane na hayo, turudi kwenye makala yetu ya leo hapo juu, jina muhimu sana katika ramani ya soka hapa nchini.
  Ni jambo la kawaida na wala halishangazi, kwa mtu aliyepita katika soka kuwa na majina ya utani kutokana na soka lake au kipaji chake, hasa kutokana na mwonekano wa mchezaji mwenyewe na wale wanaomwona wakati anasakata kabumbu, maarufu kama ‘gozi la ng’ombe’.
  Nimewahi kushuhudia watu wakiitwa majina kama vile Mogella, Kizota, Masatu, Gaga, Lunyamila, Kaseja, Mensah, Ronaldo, Etoo, Diego Maradona, Messi, Marco Van Bastern (alikuwa akitumia rafiki yangu Kingsley Malwilo akiwa Bandari Mtwara) na majina mengi tu ya mfano huo, ili mradi tu ilikuwa ni burudani kwake na kwa wapenzi wake.
  Wakati nasoma pale Tabora, katika Shule ya Msingi Kiyungi, mtaalamu wangu Ahmed Amasha alikuwa anasoma Shule ya Msingi Isike na nilikuwa nikishuhudia kwa macho yangu, uwezo wake mkubwa wa kusukuma kabumbu na niliendelea kumwona hadi alipoenda Sekondari ya Uyui, halafu Kazima, KAMISETA pale Tabora hadi kombaini yake, yaani UMISSETA.
  Pia niliendelea kumwona akiwa Tumbaku Tabora, Tumbaku Moro, hizo timu zilikuwa maarufu kwa majina ya TAT, Yanga Africans hadi Taifa Stars.
  Nilipokuwa Mwadui Shinyanga, nilijikuta mashabiki wa soka wakiniita jina la Amasha na sijui ni kwa nini, lakini kwa wale waliokuwa Mwadui miaka hiyo ya 1980 hadi 1986, ukiuliza jina la Kennedy Mwaisabula huwezi kumpata.
  Lakini ukiuliza Amasha, utanipata na utaambiwa shughuli yake ilikuwaje katika soka.
  Sio mara zote napenda kuzungumzia jinsi nilivyokuwa napiga soka, lakini kwa matumizi ya jina hilo la Amasha, huenda nami nilikuwa mtaalamu, lakini sikufika mbali sana kutokana na majukumu yaliyonizunguka.
  Wakati namkumbuka Ahmed Amasha au ‘Mathematics’ yaani mtu wa mahesabu, yuko wapi na kajichimbia wapi, ndipo nilipokumbuka maisha yangu ya kuitwa jina hilo la Amasha.
  Mtu ambaye alikuwa ni mmoja wa viungo bora kabisa niliopata kuwaona na baadaye kuhamishiwa katika nafasi ya ulinzi wa pembeni kushoto, ambayo kuanzia miaka ya 60 ilishikiliwa na Mohamed Chuma na baadaye miaka ya 70 mwishoni kuchukuliwa Mohamed Kajore kabla ya kutwaliwa na Amasha na kuwa hazina kubwa sana kwa taifa na soka kwa ujumla.
  Leo sijui yuko wapi na utaalamu wake kwa vijana wa leo, nadhani bado unahitajika.
  Nikizikumbuka zile mechi akiwa na timu za mchanganyiko wa shule za sekondari akiwa na kina Hassan Shengo, Lawrence Mwalusako, Mtemi Ramadhani, Wagadugu, Yahaya Tostao (sio yule aliyekuwa Pan) na wengineo wengi walivyokuwa wakitoa burudani nafarijika sana; wale wapenzi wa soka pale Mwadui walionipa jina hilo, ambalo leo hakuna mtu anayejua zaidi ya wale waliokuwepo Mwadui enzi hizo.
  Nazidi kuvuta hisia zaidi ya kumwangalia Amasha akitengeneza ukuta wa Berlin pale Yanga, uliowatoa nishai watani wao wa jadi Simba mwaka 1981 kwa bao 1-0, lililofungwa na Juma Mkambi ‘General’ kutokana na mpira safi sana wa kona iliyochongwa na Ahmed Amasha, hapo ndio nafarijika na jina hilo la utani nililopewa enzi hizo za Mwadui.
  Ukuta ule wa Berlin uliokuwa ukiongozwa na Amasha, pia walikuwapo akina Juma Shaabani, Yusuph Bana, Athumani Juma Chama ‘Jogoo’ na Alan Shomari ‘Moringe’ unanifanya nijisikie fahari mno kutumia jina la Amasha, mtu wa mahesabu, ingawa mimi nilikuwa nikicheza nafasi ya ushambuliaji yeye ulinzi, lakini inaelekea mashabiki nami waliniona ni mtu wa mahesabu mno.
  Natamani nyakati zile nikipewa jina hilo, ingekuwa ni leo, dunia ingenitambua. Mpira leo unalipa, mpira leo ni kila kitu.
  Ni kama vile unalala maskini, unaamka tajiri, Mbwana Samata jana alikuwa anatuomba nauli sh 200 kwenda mazoezini, leo ghafla anaweza akanunua mtaa mzima pale kwao Mbagala Kimbangulile! Lakini vijana wa leo hilo hawalioni, kweli kwenye miti hakuna wajenzi.
  Inasikitisha leo, wachezaji wanapopewa majina makubwa sana kama vile Vidic, Canavaro, Eto’o, Lunyamila, Rooney, Stam, Veron lakini wanashindwa kuyafurahia na kuyaenzi kwa kufanya mazoezi, ili angalau hata kwa asilimia 40 wasogee kutoka hapo kuyafikia majina hayo na vyombo vyetu vya habari vinayakuza sana majina hayo, kama humjui utadhani kweli huyu ni Vidic, kumbe wapi! Tunabaki tumeduwaa.
  Leo mimi kwa kutambua kuwa mazingira yalinifanya nishindwe kufikia soka la mtaalamu wangu Ahmed Amasha, basi leo angalau nichukue kalamu nimkumbuke, kama alikuwa hajui basi jina lake nimelitumia sana wakati wa enzi yangu pale Mwadui, lakini soka lile la jana sio kama la leo, leo liko wazi sana na watu wanatoa macho, zamani ilikuwa ni sifa tu mtaani inatoshaa.
  Ni wakati sasa, wachezaji wa Kitanzania kutobweteka na kupewa majina makubwa, ni wakati wa kupigana hadi tone la mwisho kuhakikisha mpira unakupa daraja la kuelekea utajiri, si wakati wa kununua Tv, fenicha wala magari, ni wakati wa kuvuja jasho ili kesho uje ulie kivulini.
  Ni wakati wa kukonda leo, uje unenepe kesho, leo lazima uvuje jasho la damu, ni wakati wa kutengeneza jina lako leo, ili watu duniani wakuite jina lako, lakini kimsingi ule matunda yako tofauti na ilivyokuwa nyuma.
  Ronaldo de Lima, leo kila siku anaongezeka kilo msubiri kesho Nwanko Kanu uone kilo zake ni watu waliovuja jasho, leo wako kivulini wanakula bata, kazi yao wameishamaliza lakini maisha kwao bado ni marefu mno, maana hata miaka 40 hawajafika, kwenye soka wanaitwa wazee! Inasikitisha mno, ndio hali halisi. Namalizia kwa kumpa changamoto, wajina Amasha, busara zake katika soka la nchi hii zinahitajika.


  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
Loading...