Kendrick Lamar & SZA- all the stars: Wasanii wetu mna nini cha kujifunza?

MALCOM LUMUMBA

JF-Expert Member
Jul 26, 2012
20,897
63,783
Hii video ilivyotengenezwa imeniacha mdomo wazi na wala sichoki kuiangalia,
Wanasema kuna vitu ameiba lakini niseme tu kwamba ubunifu uliotumika hapa ni wa kiwango cha hali ya juu sanaa. Ameitengenezea katika mazingira ya Kiafrika na bado umebamba sana: Hasashasa ukiongezea kile alichoimba na beat iliyotumika ndiyo hatari kabisaa.


NB: Hakika wasanii wetu wana kitu cha kujifunza hapa,
Siyo lazima kila video iwe na Lamborghini, Ferrari, Chevy Impala, Majumba ya kifahari au ifanyiwe nje ya nchi ili iwe nzuri. Japo naomba nieleweke kwamba sisemi kufanya hivi ni vibaya kabisa, lakini mara nyingine tunahitaji kujaribu vitu vya kitofauti ambavyo vitafanya muziki wetu uwe wa kipekee. Magari ya kifahari na majumba wasanii karibia dunia nzima ndiyo wanayatumia, sasa ni wakati tufanye kama Wahindi na nyimbo zao ambazo zinawapa Utofauti sanaaa na watu wengine.

CC: Red Giant , Benny , wick, travis 1
 
Malcom wasanii wetu naweza sema hawajui kuvaa uhalisia au wanatufanya tusione uhalisia wa kitu wanachofanya!.. Hebu cheki ile nyimbo ya Harmonize ile matatizo anataka tuone kapigika lakini anavaa fashion ya wakati huo!..Huyo ni mfano tu sasa uje ukutane na wasanii wanaact kama choka mbaya lakini kichwani wana dreadlocks wana nguo zipo vizuri!..
Unajua kuna watu wengine huwa tunaangalia na mandhari iliyotumika ili kurelate kama kinachoimbwa kinalingana!..
Ukimcheki Kendrick Lamar kwenye video zake huwa yupo soo simple lakini anazipa uniqueness flani hasa kama kwenye All the Light, Alright, Humble, DNA na ile nyimbo na drake!..
Sasa ukija kwetu unaona kabisa huyu mtu either ushamba au hajiamini, hebu mcheki Diamond kwenye ile nyimbo na Ne-yo pale anashuka gari, anashangaa demu kwenye traffic lights, anaingia ndani.
Labda mie pekee ndio naziona hizi scene za kujishtukia wasanii wetu!..
-wick
 
Kitu ambacho Nimegundua ni Lifestyle tu ...wakina kendrick wamekuliaa sehem ambayo imeshaendelea kiuchumi na pia sehem ambayo ina watu wengii wenye IQ kubwaa hivo basi kwa namna moja au nyingine inawasaidia wao katika shughuli zao mbali mbali....Tofauti na awa ndugu zangu wa bongo....Tumekulia katika mazingira ya umbea na umaskini kwahyo idea kama izo ni ngumu sana kwa mtu kuziwasilisha katika jamii....Tumeshalemazwa na lifestyle yetu
 
Waafrika wabaguzi sana ila tunawasingizia wazungu wanatubagua, Mara watengeneze muvi ya mablack tupu Mara waunde TV ya mablack tupu 'bet', miafrika ni mibaguzi sana
 
Jamaa namkubali mnoo.
Anatumia sana akili kufanya vitu, hii nafasi alianza nayo Lupe Fiasco lakini akaja kuharibu mbele.
Ile Album yake The Cool, Jay Z aliisifia sana akasema It's a breath of fresh air....Lakini kwenye Beautiful Lasers akaweka U-Main Stream mwingiiiii sana akaharibu.......though it was a good Album!
This man is
 
SZA anafanya vizuri sana hata kwenye Love garone akiwa na Travis skot alifanya vizuri sana anajua

Dada anajiweza sanaaa!
Siku hizi hakuna wanawake wakali kwenye RnB kama ilivyokuwa zamani.
Yaaani kuna upungufu mkubwa sana wa wasanii wa kike RnB marekani hadi nashangaa!
 
Kitu ambacho Nimegundua ni Lifestyle tu ...wakina kendrick wamekuliaa sehem ambayo imeshaendelea kiuchumi na pia sehem ambayo ina watu wengii wenye IQ kubwaa hivo basi kwa namna moja au nyingine inawasaidia wao katika shughuli zao mbali mbali....Tofauti na awa ndugu zangu wa bongo....Tumekulia katika mazingira ya umbea na umaskini kwahyo idea kama izo ni ngumu sana kwa mtu kuziwasilisha katika jamii....Tumeshalemazwa na lifestyle yetu

Hahahaha Braza bwana!
Hata bongo hapa kuna watu wana IQ kubwa sanaaa sanaaaa!
Sema shida yetu ni kwamba tunafanya vitu kwa tamaa, ubinafsi na kukomoana.
Hatuna visima vya kuteka vipaji kama hawa jamaa walivyo . Tuna macho lakini hatutambui vipaji hata tukiviona, tunamkubali mtu ana kipaji cha kuimba mpaka awe anafanya aina fulani fulani za muziki ambayo sisi tunaitaka (To me this is very wrong); Kwasababu inaua Originality na Creativity mwishowe tunakua na muziki yebo yobo usio na Identity.
 
Back
Top Bottom