Kenchi ikikaa muda gani bila bati inaharibika

Kitumburee

Senior Member
Jan 31, 2012
139
88
Salama wanajamvi?

Kama kichwa cha uzi kinavyojieleza. Wiki nne zilizopita Nilifunga mbao za kench ktk site yangu na kuoda bati alaf ila bati bado hazijatoka nimeambiwa nitegemee zitatoka ndani ya wiki tatu zijazo.

Na mvua za masika ndio naona zimeanza hapa Dar. Sasa naingia wasiwasi kama kenchi zinaweza kuharibika. Naombeni ushauri wadau kama kweli zinaharibika zikikaa sana na je nifanye nini kuzuia uharibifu.

Nyumba iko Dar na nimetumia mbao zenye dawa. Ila ni mbao za dawa ya kuchovya sio zile za kuchemsha

Wasalaam
 
Swalama wanajamvi?
Kama kichwa cha uzi kinavyojieleza. Wiki nne zilizopita Nilifunga mbao za kench ktk site yangu na kuoda bati alaf. ila bati bado hazijatoka nimeambiwa nitegemee zitatoka ndani ya wiki tatu zijazo. na mvua za masika ndio naona zimeanza hapa Dar. Sasa naingia wasiwasi kama kenchi zinaweza kuharibika. Naombeni ushauri wadau kama kweli zinaharibika zikikaa sana na je nifanye nini kuzuia uhatibifu.
Wasalaam
Inategemeana na
- mvua na jua

Maana tatizo linaloweza tokea ni kupinda kwa mbao kutokana na unyevunyevu kubadilika ndani ya mbao

So
Labda ufunike lailoni nyumba nzima

Other wise ni itokee zisipinde sana

But one week was enough kuvumilia
 
Kama mfuko wako unaruhusu nunua Nylon kisha funika juu ya mbao zako, by the way week tatu kama mvua hainyeshi kila siku siyo shida
 
Bora zinyeshewe mvua mfululizo kuliko jua maana zikipigwa jua huanza kukauka na kupinda.
 
Swalama wanajamvi?

Kama kichwa cha uzi kinavyojieleza. Wiki nne zilizopita Nilifunga mbao za kench ktk site yangu na kuoda bati alaf. ila bati bado hazijatoka nimeambiwa nitegemee zitatoka ndani ya wiki tatu zijazo. na mvua za masika ndio naona zimeanza hapa Dar. Sasa naingia wasiwasi kama kenchi zinaweza kuharibika. Naombeni ushauri wadau kama kweli zinaharibika zikikaa sana na je nifanye nini kuzuia uharibifu.

Nyumba iko Dar na nimetumia mbao zenye dawa. Ila ni mbao za dawa ya kuchovya sio zile za kuchemsha

Wasalaam
Kumbe upo Dar ambako Kuna viwanda kila sehemu afu unasema umetoa order kupata baada ya wiki tatu kweli na viwanda vimejaa huko na je wamikoani watasemaje.
 
Kumbe upo Dar ambako Kuna viwanda kila sehemu afu unasema umetoa order kupata baada ya wiki tatu kweli na viwanda vimejaa huko na je wamikoani watasemaje.
Wewe usitake kumuingiza chaka mwenzio , kikawaida kulingana na ubora wa bati za ALAF huwa na msururu wa wateja wengi hivyo huwezi kwenda leo alafu leoleo ukapata mzigo wako, lazima uweke order kisha wakupatie invoice uende bank kulipia alafu uwapelekee receipt ya malipo kiwandani, kisha sasa ndio waanze kushughulikia order yako.

Nadhani umeelewa sasa utaratibu wa kupata bati za ALAF
 
Kwa suala lako la muda mfupi vumilia tu - uombe (a) hao wa bati wasikucheleweshe zaidi na (b) hali ya hewa iwe rafiki kwa siku zilizobaki.
 
Pole sana ila umefanya makosa kiasi chake, ingependeza kama ungenunua bati kwanza kisha ndo mbao. mawazo tu lakini
 
Pole sana ila umefanya makosa kiasi chake, ingependeza kama ungenunua bati kwanza kisha ndo mbao. mawazo tu lakini
Hapana mkuu niko sahihi kabisa. Kwa bati za alaf ambazo zinauzwa kwa sqm na zinapatikana kwa foleni lazima uweke kenchi kwanza upime ukubwa kujua kiasi exactly kipimo cha bati zitakazohitajika kisha unaweka oda kiwandani. Vinginevyo unawezanunua bati chache kuliko uhitaji au ukanunua bati nyingi zana kuliko uhitaji ukala hasara
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom