Kenani Kihongosi: Jumatatu 16.8.2021 kuanzia saa 3 Asubuhi nitakuwepo ofisi za UVCCM Upanga Jijini Dar

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
279
500

KATIBU MKUU WA UVCCM TAIFA NDUGU KENANI LABANI KIHONGOSI ATENGA MUDA WA KUSIKILIZA NA KUPOKEA MAONI NA USHAURI.


KESHO JUMATATU 16.08.2021 SAA 3 ASUBUHI KATIBU MKUU WA UVCCM TAIFA NDUGU KENANI LABANI KIHONGOSI ATAKUWEPO OFISI NDOGO ZA UVCCM UPANGA DAR ES SALAAM VIJANA WOTE MNAKARIBISHWA SANA.


Kesho Jumatatu 16.8.2021 kuanzia saa 3 Asubuhi nitakuwepo ofisi za UVCCM UPANGA Jijini Dar es Salaam kusikiliza pia kupokea maoni na ushauri, napenda kuwakaribisha Vijana wote tuzungumze pamoja. Karibuni sana katika Ofisi yenu Tuzungumze na kupokea mawazo.
.

.
.
Hongera sana Katibu Mkuu (KM) UVCCM Taifa Ndugu KENANI LABAN KIHONGOSI kwa hatua hii kubwa ya kuleta mabadiriko, hakika umeendelea kuihubiri sera yako ya #MtumishiWaWote kwa vitendo.

Binafsi kwangu nimeifurahia hatua hii ambayo naamini litakua na faida nyingi sana.

Kitendo cha sisi vijana kupata nafasi ya kushauri na kutoa maoni kuhusiana na Jumuiya itakua na faida kubwa sana, Miongoni Mwa faida ni;

1 - Unairudisha dhana ya Jumuiya Yetu ni ya kila Kijana si ya watu wachache kama ilivyokuwa ikionekana zamani.

2 - Lakini unaendelea kuishi dhana ya #MtumishiWaWote.

3 - Naamini hatua hii itasaidia sana kuboresha idara ya Hamasa na Chipukizi.

4 - Nashauri zoezi hili litakua liwe Endelevu, walau lifanyike kila baada ya miezi 6 ili kuwa na maboresho ya mara kwa mara.

5 - Lakini zoezi hili linaweza kuigwa na viongozi wetu wa chini

#MtumishiWaWote🙏

IMG-20210815-WA0058.jpg

IMG-20210815-WA0076.jpg
 

Bengal

JF-Expert Member
Aug 29, 2018
6,413
2,000
Ushauri chamakijani kisimame kwa kwa miguu yake cheyewe kama chama cha siasa, kiache kutumia dola na vyombo saidizi. akina neki, wauruginzi, na akina msajili ili kuendelea kuwepo kwake.
 

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
125,012
2,000

Mbelele007

Senior Member
Apr 6, 2017
140
225
Sawa bora wangetoa namba wapate ushauri Tanzania nzima kuliko Dar kama Dar!!!!! Kuna watu wanaushauri bora huku NANJILINJI kuliko hata huko Dar es salaam
 

KingCobra95

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
1,674
2,000
Huko chamani kuna mashindano ya modelling,Mbona hawa jamaa wanajali Sana mapichapicha ?kila tangazo ni mipicha tu
 

KEROZENE

JF-Expert Member
Apr 2, 2015
6,119
2,000
Ushauri wangu UVCCM ikatae mtindo wa Idara Nyeti nchini kuchukua lundo la Vijana wake Kuingia huko kwakuwa tu ni CCM bali waitake Idara irejee ule utaratibu wake wa Kipindi cha Mwalimu cha kuchukua Watu kila Kona ya nchi bila kuangalia Kigezo cha Chama cha Siasa, Dini, Ukabila na Elimu.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom