Kempinski ni management company au ni investment company? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kempinski ni management company au ni investment company?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mshiiri, Aug 28, 2008.

 1. Mshiiri

  Mshiiri JF-Expert Member

  #1
  Aug 28, 2008
  Joined: Jun 16, 2008
  Messages: 1,893
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 145
  Kempinski
  Kuna tetesi kuwa hawa mabwana Kempinski ni management company na huwa hawana properties zao wenyewe bali wanatoa usimamizi kwa makubaliano maalum na owners wa accommodation properties haswa high calibre hotels. Sasa kwa Tanzania ni nini wanafanya? Hakuna ufisadi hapa kweli kwani makampuni ya nje si yana speciality kama ni management ni management why makampuni yakija Tanzania yanakiuka policy zao na kufanaya kinyume only for Tanzania? I suspect ni kwa vile wanapata msaada wa 10% kwa viongozi wetu walio na gene za kifisadi.

  Ufisadi
  Ufisadi jamani unarithi mbona watoto wa mwalimu ni mfano mzuri wa kuigwa. Tusichague watoto wa mafisadi jamani kwenye uongozi, mfano mwingine mzee ruksa mbona mwanae ni safi, Sokoine, Cleopa Msuya, Kawawa nk wao ni safi na watoto wao ni safi. Ndo kusema kwa utafiti nilofanya ufisadi is a genetic disease that is passed from generation to generation down the line.

  Swali
  1. What is Kempinski?
  2. Is it a management only company?
  3. Is it registered as an investor in Tanzania United Republic of?
  4. Why were they given priority over even the bloody citizens? i.e. Dar Mengi, Arusha Mrema etc. By fortune they were all chaggas. Is it that Kempinski will always out compete bloody citizen chaggas
  5. What is all behind the Kempinski because its background is darkened?


  Wana JF tafadhali mwageni mambo hapa tufumue mengine kwani nasikia sasa wameingia mbugani Serengeti na tufike mahali wananchi wa chini wajue why kuinvest wenyewe tumeshindwa na kuchukua pesa na kuficha kifisadi tunaweza.
   
 2. K

  Kamundu JF-Expert Member

  #2
  Aug 28, 2008
  Joined: Nov 22, 2006
  Messages: 2,109
  Likes Received: 455
  Trophy Points: 180
  Hakuna ubaya wowote kwa Investor kuamua Mgmt company yenye uwezo kuendesha hotel kwani kikubwa ni uendeshaji mzuri.Kampuni nyingi Tanzania zinakufa kwasababu waendeshaji hawana uwezo hivyo ningeshauri kama kuna kampuni Tanzania basi watafute watu wenye pesa na kujaribu ku Manage project zao.
   
 3. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #3
  Aug 29, 2008
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Mshiiri,

  Sijakuelewa vizuri katika hoja yako.

  Ila tu kwa siku hizi tatizo la makampuni mengi au service mbalimbali hapa duniani sio technology na badala yake ni management na ndio maana watu wenye uwezo huo sasa ni lulu hapa duniani.

  Ni rahisi kujenga hotel ya maana lakini sio rahisi kuendesha. Hao Kempinski wana proven record kwenye uendeshaji wa hotels na hivyo hata owners mbalimbali wa hotel mpya wanaona afadhali wawape wao.

  Ukitaka kujua madhara managements mbaya, angalia matatizo kwenye makampuni yetu mbalimbali. Ndio maana hata Guest houses tu watu wanaanza kuajiri wageni.
   
 4. w

  wajinga Senior Member

  #4
  Aug 29, 2008
  Joined: Jun 25, 2008
  Messages: 148
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  watanzania hatutaki kutumwa kila mtu anajua ndio sababu hatuwezi kutoa service mteja akikukosoa unamfukuza sasa unafikiri utaendesha hoteli namna hiyo. Kempiski wanamanage na kuinvest hakuna ubaya cha kushangaza ni kwamba watu wanaowatumia kufanya hiza kazi ni watanzania hao hao,mid level management ni rangi nyeupe.wa ngazi za chini waswahili. go figure
   
 5. Songambele

  Songambele JF-Expert Member

  #5
  Aug 29, 2008
  Joined: Nov 20, 2007
  Messages: 3,435
  Likes Received: 1,015
  Trophy Points: 280
  Jamaa huduma zao ni bomba, ukilinganisha na hotel nyingi za bongo. Sioni sababu yeyote yakuwa na mashaka na watu wanaofanya vizuri na wafanyakazi wengi ni wabongo. Kampuni nyingi bongo zinakufa kama Mshiiri mwenyewe anavyoainisha kutoka na uwelewa mdogo kuhusiana na management.

  Management ni science kama zilivyo science nyingine na management pia sio sawa na siasa tatizo bongo mnachanganya management na siasa. Kama mtoa mada anawataja wanasiasa ambao yeye anaona wamefanikiwa katika siasa. Management wapewe watu wenye uwelewa wa science ya management. Ukidadavua management bongo utaona watu wasio na uwelewa wa management wanafanya kazi za management, na hawataki kujifunza management kwa kuona wao wanajua.

  Watuhumu kama kweli unahakika na huo ufisadi na ushahidi unao, vinginevyo kila mtu kila kampuni itakuwa fisadi bongo.
   
 6. FairPlayer

  FairPlayer JF-Expert Member

  #6
  Aug 29, 2008
  Joined: Feb 27, 2006
  Messages: 4,166
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Tatizo lao kama hotel nyingine ni matumizi ya hela za kigeni ukitaka kulipia kwa hela ya bongo unapewa exchange rate kuubwa!
   
 7. FairPlayer

  FairPlayer JF-Expert Member

  #7
  Aug 29, 2008
  Joined: Feb 27, 2006
  Messages: 4,166
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Dawa ilikuwa ni Wizara ya fedha kuwalazimisha kutumia BOT mean rate, na sio kutumia watakayo.
   
 8. K

  Kifuna JF-Expert Member

  #8
  Aug 29, 2008
  Joined: Aug 7, 2008
  Messages: 426
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Hiki kitu kinahitaji hekima sana kukizungumza, Kwani baada ya wakoloni kututawala na kuondoka kwa kudai wametupa uhuru, wameenda kujipanga upya na kurudi na nguvu kubwa sana ya akili Sio kiuchumi, na sio ya mabavu tena kama walivyokuwa miaka ya 50. Walijua kipindi kile tulikuwa hatujaendelea kielimu na kifikra, baada ya kujua kuwa tunajua wameona dawa ni kujua zaidi (kutuliko) ndio maana wanawekeza mpaka kwenye hoteli.

  toka lini mtu akawekeza Hotelini kama sio kuchota mali zetu na akili zetu pia?
  tunahitaji tupate Nyerere mwingine adai uhuru wa mawazo, wa elimu na fikra pevu, kwani tulichonacho sasa ni uhuru wa Bendera tu.sasa kwa swali hili la mwanzisha mada ni kuwa KEMPINSKI NI WAKOLONI.
   
 9. Mshiiri

  Mshiiri JF-Expert Member

  #9
  Aug 29, 2008
  Joined: Jun 16, 2008
  Messages: 1,893
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 145
  Ufisadi vs Priority
  Na je kwanini wawekezaji wa ndani hawapewi nafasi au kipaufront. Mathalani Bw. Mengi na Bw. Mrema walio na uwezo wa kuinvest lakini wakapigwa stop Kilimanjaro Hotel Dar, 77 Hotel Arusha na wengineo wengi. Ikiwa baadae tunadai wanaiba uchumi wetu n.k mfano mzuri TANESCO na Wa-Sauzi. Tuheshimu na kujali vyetu kusema wameajiri watanzania hiyo ni kuteleza kifikra kwani hawawezi kuleta wazungu kwa kuwa hata mfagizi atapaswa kulipwa kama milioni 2 kwa mwezi na nyumba na gari ambapo kwetu ni cheep labour just kwa sababu serikali haina sera nzuri za ajira. Na haitaki kufanya hivyo ndio maan tuko masikini kwa sababu hata ukifanya kazi huna disposable income cause you earn tantamount to insult. Therefore kwa vyovyote hata kama wangewapa watanzania ajira zingekuwako tena nyingi zaidi na mapato yangetumika kufanya miradi mingine hapa hapa nchini. Hii ni wazi. Mfano, Bw. Mrema amefanya investment Impala Hotel, akazalisha na kufanya project ya Ngurdoto, akazalisha na kufanya project ya Naura Springs zote multibilion projects sasa hawa jamaa huwa hawafanyi hivi wao huvuna na kusepa. Si kwamba decision makers hawana ufahamu ila ni mtindio wa mawazo. Kama wizi wa fedha wameweza kuufanya na ikachukua muda mrefu hivyo kujulikana they must have been best managers to manage what they were doing. We are good managers and not otherwise but matter of getting rich quickly etc.

  Swali la msingi
  Why Tanzanians Investors are last priority when comparing to investment by non native?
   
 10. Mhafidhina

  Mhafidhina JF-Expert Member

  #10
  Aug 30, 2008
  Joined: Feb 6, 2008
  Messages: 548
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Mshiiri unaswali zuri lakini labda umekosea kuliuliza, kwani huwa hakuna tatizo lolote la kuwa na Management Company

  Swali labda ungeuliza, JE KENMPISKI ni jina la biashara tu au ni Kampuni?

  Kwani imegundulika kwamba makampuni mengi sana Tanzania hivi sasa wanatumia Business Names kukwepa kulipa kodi...! Wanachokifanya ni Kuanzisha Kampuni kwa jina lingine halafu kutumia jina lingine kwa kufanyia bihashara hivyo kutumia mwanya huo kukwepa kodi.

  Kwa Mfano, Hoteli ya Movenpik mmiliki wa Hoteli ni Kampuni ya Tanrus Ltd, lakini jina la bihashara ni MOVENPIC (Business Name), sasa hawa wanachokifanya ni kwamba wakati wanalipa kodi (filing of returns) wanalipa kupitia Tanurus Ltd hivyo kupotosha mapato halisi ambayo Tanrus Ltd imeyapata kupitia MOVENPIC.

  Mfano wa pili ni hoteli ya Goldern Tilip, Mmiliki wa hotel hii ni Indian Ocean Ltd, Lakini wanatumia jina la Goldern Tulip kufanyia bishara (Business Name), hivyo wakati wa kulipa kodi wao huwa hawatoi taarifa sahihi ambazo walifanya biashara kama Goldern Tulip.

  Kwa kifupi huu ndio mwanya haya mahoteli wanatumia ili kukwepa kodi na kuendelea kutuibia mapato sisi WADANGANYIKA.
   
 11. Mshiiri

  Mshiiri JF-Expert Member

  #11
  Sep 28, 2011
  Joined: Jun 16, 2008
  Messages: 1,893
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 145
  I heard it is sold again - Kilimanjaro Hotel
   
 12. rasmanyara

  rasmanyara Senior Member

  #12
  Sep 29, 2011
  Joined: Sep 12, 2011
  Messages: 198
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Kwa sasa Tanzania hakuna KEMPINSKI,hawaendesh proparties yeyote.Mwarabu kawapa kampuni tatu tofauti zifanye biashara kwenye majengo yake.
   
Loading...