Kelele zawaponza mke na mume, watengwa na jamii

Jul 11, 2015
69
125
Kaya mbili zimetengwa na wananchi wa Mtaa wa Nyantorotoro katika Halmashauri ya Mji Geita akiwemo mume na mke waliopewa adhabu ya kulipa faini ya ng’ombe kwa kila mmoja ama shilingi 100,000 kufuatia tukio lililotokea zaidi ya miezi mitano la kupiga kelele nyakati za usiku kwa madai ya kuvamiwa ilhali ukweli ukidaiwa kuwa walikuwa kwenye ugomvi binafsi.

Adhabu hiyo imepigiwa msumari katika mkutano wa wakazi hao wakiwemo na wazee wa kimila pamoja kufuatia kuwasili kwa Diwani wa eneo hilo aliyefika kumwakilisha mkurugenzi wa halmashauri baada ya kupata taarifa za kutengwa kwa wakazi hao kupitia sheria za mila za wakazi Geita.

Watu hao waliotengwa kwa mujibu wa mila itawapasa kukaa mbali na ushiriki wa shughuli za kijamii na maendeleo zikiwemo misiba, maongezi wala salamu, baina yao na jamii inayowazunguka huku biashara zao wanazofanya za kuongeza kipato cha familia kutoungwa mkono.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom