Kelele za vyuma kukaza hutakaa uzisikie tena kwa sababu wakubwa wanaogelea kwenye pesa sasa hivi

Etwege

JF-Expert Member
Jul 4, 2018
5,733
15,193
Mara nyingi watu wa hali ya chini wamekuwa wakiimbishwa nyimbo wasizozijua hasa lengo lake ni nini.

Licha ya sasa hivi watu wa hali ya chini kuwa na hali mbaya jiuchimi, huduma muhimu kwa jamii kupanda bei kwa kiwango cha kutisha, kuharibiwa biashara zao na wengine kuanza upya kabisa baada ya mitaji kukata lakini hutakaa usikie redio, au gazeti au kiongozi mkubwa akiwatetea.

Badala yake utasikia redio na Tv na magazeti yakitangaza hali ya maisha ni nzuri mno kwa wananchi, vyuma vimelegea na hela zimejaa mitaani!

Lakini ukigusa biashara za wakubwa wasiolipa kodi ,kesho yake magazeti, redio na Tv zitaandika vyuma vimebana hela hamna mfukoni kwa sababu biashara zinafungwa

Yani biashara za wakubwa tu zikifungwa ndiyo shida ila zinapofungwa za walala hoi hapo hamna shida.

Hiyo ndiyo Tanzania.
 
Huyu Mataga kaanza kuwa mpole,😆kutesa kwa zamu ndugu, jiunge na Polepole kwenye Team Manung'uniko.

Wamachinga walikuwa wanatuzibia Barabara sisi wenye vyombo vya moto, ambao tunalipia Kodi ya Road Tax, ambayo ni Pesa nyingi, halafu wao wanapanga biashara ati wamelipa elfu ishirini.B.S
 
Kumbe samtaimu mna akili eeh😅 kipindi mnamtukana hayati tuliwaambia ni swala la muda tu! Hii nchi sio ya matajiri peke yao Magufuli alijaribu sana ku prove hilo kwenu ila kwa uhayawani wa wengi mkakazania kumtukana oh anaua watu oh mara vile! Anagandamiza vyombo vya habari blaah blah!

Kwani ya muhimu si maendeleo jamani hayo mambo ya siasa vipi..Alisema asikwamishwe na watu wasilete taharuki vihele hele wakajifanya manunda ikala kwao😅 mbona mi na wewe hatujafa kama alikuwa anaua watu makusudi.

Acheni nifanye kazi hii ndio ilikuwa kauli yake kuna choko akajifanya anajua sana kuzodoa kilichomkuta anakata viuno ubeligiji sahizi!
Kwa hiyo hakuua watu?
 
Hahaaa sisi tunamcheki tu.
Magufuli alikuwa hawapendi wamachinga ila alikuwa akiwahadaa tu ili akiiba kura aseme Serikali yake ni Legit

Alikuwa anauwezo wa kumwambia Ndugai na Wabunge wa CCm amba ndio wengi wapitishe mswaada uwe sheria ili Kariakoo yote Barabara zifungwe ili Machinga waweze kufanya Biashara.
 
Back
Top Bottom