Kelele za Thamani ya dola kupanda dhidi ya shillingi zimekwenda wapi?

Leak

JF-Expert Member
Feb 22, 2012
52,842
43,296
Wasalaam..
Wana JF kama mtakuwa na kumbu kumbu kuwa hapo nyuma kama wiki tatu zilizo pita kila leo wana siasa na watu walikuwa wakipiga kelele kuwa dolla inapanda sana na kusema uchumi unaanguka na kila leo walikuwa wanatupa mwenendo wa dolla dhidi ya shillingi..

Nakumbuka kuna wengine walisema wazi wanataka ifike hata 5000 na wengine wakasema kabisa lazima itafika hata 6000 na walikuwa kila leo wanatupa data za ongezeko la thamani ya dola dhidi ya shillingi yetu huku wakishangilia.

Lakini ni wiki mbili sasa hakuna anayepost au kusema mwenendo wa dolla dhidi ya shillingi uko vipi? je dolla imendelea kupanda? imefika 4000 au 5000?
Mbona hatupewi mrejesho kama tulio kuwa tunapewa kila leo?

Wasalaam.
 
ila shilingi inatia aibu! khaaa...!! napendekeza wakate sifuri 2 kwa kila hela, yani kama ni 10000 iwe 100, na 5000 iwe 50, pia 2000 iwe 20, 500 iwe 5, 200 iwe 2 na 100 iwe sh 1 nadhani hapo thamani ya pesa yetu itakuwa na nguvu sana... sio saivi ukienda dukani kununua kiatu unajaza noti kibao na michenchi kwenye mfuko wa rambo kwa ajili ya jozi moja ya viatu.
 
Back
Top Bottom