Kelele za muziki kwenye bar(?)

O-man

JF-Expert Member
Nov 17, 2011
323
65
Kuna bar na guest (mwenyewe ameipa jina la hoteli) jirani yangu inatunyima amani kwa kelele za juke box. Ni kuanzia asubuhi mpaka usiku wa saa 6 au zaidi. Tumezungumza na mmiliki lakini wapi. Ilifikia hatua baadhi ya majirani wanaoishi gorofani kutupia vipande vya matofali juu ya paa la hiyo hoteli ili kufikisha ujumbe wa hizo kelele, bado zinaendelea. Mjumbe, M/kiti wa serikali za mitaa na mtendaji wanazo taarifa. Hapa tumekwama. Msaada wenu unahitajika kutuondolea kadhia hii.
 
Umoja ni NGUVU. Ukiona hamna nguvu, ujue hamna umoja.
Majirani mkiamua bar itafungwa tu
 
Jamani pole lakini kuna haja sheria ya kuhusiana na haya makelele ifanye kazi sio tunaishia kusoma tu darasani coz yanaboa niaje hasa pale ukiwa unataka kupumzia
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom