Kelele Kubwa Matangazo ya TVs Zinakera Sana

MPUNGA

JF-Expert Member
Nov 10, 2010
838
559
Hivi hawa TCRA hawana kanuni za kuwadhibiti hawa jamaa wenye kurusha matangazo ya TV, wanatukera saaaaana na kelele kubwa za matangazo yao ya biashara. Nakumbuka nyuma kidogo ama ni Marekani au Ulaya wamepiga marufuku kuongeza sauti kubwa ya matangazo yao ya biashara. Umekaa sehemu unasikiliza kipindi murua chenye kuhabarisha na kuelemisha mara ghafla unasikia sauti imepaa ghafla sababu ya matangazo yao mnaanza kutafuta remote control ambayo kumbe mtoto kaichukua anacheza nayo sehemu nyingine. Hii kero ipo sana hasa kwa hawa jamaa wanaopewa shavu la 'super brand'.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom