Kekundu: Nape na Bashe 'wanaibeba' bajeti na mjadala wake. Mkishtuka, imeshapita kwa kishindo!

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
6,136
17,871
Si Nape Nnauye wala Hussein Bashe aliye mpinzani wa CCM na Serikali yake. Wote ni CCM kindakindaki na wanashiriki kila mpango wa chama hapa Dodoma na nje ya hapa. Mipango ya sasa ni kuhakikisha bajeti za Wizara zote zinapita kwa kishindo. Kunatakiwa strategies tofautitofauti. Hata 'kupoteza maboya' kunasaidia.

Wabunge hawa vijana wamepewa jukumu muhimu la kuhamisha mjadala wa bajeti. Kuuhamisha kwa Wabunge na hata wananchi. Kuwayumbisha wananchi kifikra na kuanza kuwafutilia kauli na matndo yao. Wabunge hawa wanajua kabisa kuwa kama wasipofanya wanavyofanya, mjadala wa bajeti ungekuwa moto wa kuotea mbali.

Nape na Bashe wanazuga kukosoa. Wanazuga kuwa hoja za kujadiliwa Bungeni. Wanazuga kuwa wapinzani chamani. Wanazuga kuungwa mkono na wengine. Wanazuga kuguswa na mambo ya wananchi wa kawaida. Wanazuga kusema na kufanya wanavyoviamini. Kwa Mwenyekiti na Rais tuliyenaye, ingekuwa kweli, wasingethubutu!

They act, we follow. Wanatupoteza na kutupumbaza wakati muhimu wa mjadala wa bajeti ya Serikali unaopaswa kujadili iliyopta na ya sasa. Nape na Bashe wako kwenye mission maalum. Siasa ni ubunifu. Siasa ni usanii. Siasa ni utapeli na ulaghai. Siasa ni kuaminisha cha uongo na kupotosha ukweli.

Bastola ya nini tena jamani!?

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Dodoma)
 
Aliyekupa kadi ww anatakiwa kuchunguzwa akili watu wanasema wanatishiwa maisha ww unasema wako kwenye missions na wakifa je utasema wamekufa kwenye missions au wameuawa ?
 
Kiongozi, mficha maradhi, kilio kitamuumbua. Kama mwaka huu inasemekana utekelezaji ni 34%, mwakani si itakuwa 8%! Kama usemayo ni kweli, hizo ni "strategies" za kijinga kuwahi kutokea kwa sababu mwisho wa siku output ita-reflect uhalisia.
 
Bajeti isiyofata kanuni na idhinisho la bunge bali kwa utashi wa mwenye mamlaka ya nini? inamsaidiaje mwananchi wa chini wakati ni maigizo tu?

Wacha tujadili wakina Roma na Bashe kwani angalau hawa wamekuwa wakiongelea umaskini wa Watanzania na kuhoji ufedhuli na vibweka vya wala nchi.

VUTA-NKUVUTE wewe binafsi umefanya jitihada gani kulisaidia Taifa zaidi ya kula kodi la wavuja jasho na sasa wavuja damu wa Tanzania?!
 
Hizo bajeti feki huwa zinapita tu ,na shangaa ma pro dt kutotumia ujuzi wao ki uhalisia wanakomaa na ulaghai wa kisiasa
 
Si Nape Nnauye wala Hussein Bashe aliye mpinzani wa CCM na Serikali yake. Wote ni CCM kindakindaki na wanashiriki kila mpango wa chama hapa Dodoma na nje ya hapa. Mipango ya sasa ni kuhakikisha bajeti za Wizara zote zinapita kwa kishindo. Kunatakiwa strategies tofautitofauti. Hata 'kupoteza maboya' kunasaidia.

Wabunge hawa vijana wamepewa jukumu muhimu la kuhamisha mjadala wa bajeti. Kuuhamisha kwa Wabunge na hata wananchi. Kuwayumbisha wananchi kifikra na kuanza kuwafutilia kauli na matndo yao. Wabunge hawa wanajua kabisa kuwa kama wasipofanya wanavyofanya, mjadala wa bajeti ungekuwa moto wa kuotea mbali.

Nape na Bashe wanazuga kukosoa. Wanazuga kuwa hoja za kujadiliwa Bungeni. Wanazuga kuwa wapinzani chamani. Wanazuga kuungwa mkono na wengine. Wanazuga kuguswa na mambo ya wananchi wa kawaida. Wanazuga kusema na kufanya wanavyoviamini. Kwa Mwenyekiti na Rais tuliyenaye, ingekuwa kweli, wasingethubutu!

They act, we follow. Wanatupoteza na kutupumbaza wakati muhimu wa mjadala wa bajeti ya Serikali unaopaswa kujadili iliyopta na ya sasa. Nape na Bashe wako kwenye mission maalum. Siasa ni ubunifu. Siasa ni usanii. Siasa ni utapeli na ulaghai. Siasa ni kuaminisha cha uongo na kupotosha ukweli.

Bastola ya nini tena jamani!?

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Dodoma)

Angalia wasije wakakuteka tu, maana hawajali hawa wenzako wa Chama Cha Mauaji.
 
Miaka yote bajeti za wizara zote zinajadiliwa na kupitishwa.Haijawahi tokea bajeti ikakataliwa.Usilete maneno yasio na maana.Acha mijadala mingine nje ya bunge iendelee tu.Hata tukifuatilia hizo bajeti hakuna jipya maisha ndio kwanza yanazidi kubana.Waendelee na vikao wamalize maisha yaendelee.Bunge live hakuna utafuatilia nini?
 
sikumbuki kama kuna siku bajeti ya serikali ilishindwa kupita huko dodoma....ingawa haitekelezeki kila mwaka.
 
Huo mkwara sijui wakupiga kelele hauna maana kabisa.

Watoto ndo hawajui kwamba wabunge watapitisha hiyo bajeti kwa kelele za ndio na vigelegele.

Hakuna jipya, si tunaendelea kuisoma namba miaka 10 ipite aje mwingine.
 
Back
Top Bottom