kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 13,428
- 13,936
Najua utakimbilia kusema huu uzi ni wa ki..puu.zi lakini itakuwa umevaa miwani ya mbao kama utafanya hivyo. Sio makosa yetu wala yao bali ni makosa wakoloni wetu walioelimisha zaidi watu wa upande mmoja wa nchi kuliko wale wa upande mwingine wa nchi.
Hii imesababisha jamii ya aina moja kupata zaidi elimu, ajira na ujira ambao unawekezwa kwenye elimu za watoto wao, biashara, kilimo, kununua ardhi kubwa za wale waliochelewa kuipata elimu popote walipo nchini.
Hali hii inasababisha Tanzania kuwa na watu wa kabila moja sehemu moja ya nchi na mchanganyiko wa makabila na dini sehemu nyingine nchini.
Hali ikiendelea hivi baada ya miaka 50 mbele iko siku ofisi zoote za umma, biashara, ardhi na mipango zikashikwa na watu wa aina moja tu ambao itakuwa vigumu kwa watu wengine kufurukuta kutokana na network itakayosukwa na kundi hilo la watu wanaokula keki kubwa ya taifa.
Kwa makusudi kuwe na jitihada za makusudi ili kuhakikisha kuwa keki ya taifa inagawanywa kwa usawa.
Kuigawanya keki kwa usawa ni kuhakikisha kuwa makundi ambayo yaliikosa elimu yanapewa kipaumbele kwenye elimu, ajira na fursa nyingine ili kupunguza pengo lililojitokeza katika mgawanyo wa keki. Pato kubwa la taifa linahudumia zaidi upande mmoja tu wa taifa na jamii.
Yako makundi ambayo ardhi yao inazidi kuporwa kwa maeka na maeka na wageni wa kutoka kundi lile lililopendelewaga na wakoloni enzi zile. Hawana mishahara, shule nyingi, hospitali, umeme wala maji kuliko wenzao wa upande ule.
Kundi lile limejenga mtandao wa kuitana kwenye ajira na fursa nyingine mbalimbali na kuwafanya wengine wasifue dafu katika kila jambo.