Masanilo
Platinum Member
- Oct 2, 2007
- 22,286
- 4,511
Baada ya bintiye kunyimwa dhamana...Keenja aingilia kati, yatolewa
*Harakati zatumia muda wa saa mbili pekee
*Hakimu achanganyikiwa, ajitoa kwenye kesi
MTOTO wa Mbunge wa Ubungo, Bi Eliaisa Keenja, aliyefutiwa dhamana juzi saa sita mchana na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, amepata dhamana katika kipindi cha saa mbili, baada ya Mahakama Kuu ya Tanzania kutoa amri ya kufanya hivyo.
Tukio hilo lilitokea juzi mbele ya Hakimu Mkazi, Bibi Bernadetha Beda baada ya mshitakiwa huyo kukiuka masharti ya dhamana na kumfutia dhamana aliyokuwa nayo.
Hakimu Beda alitoa uamuzi wa kumfutia dhamana mshitakiwa huyo kutokana na kosa alilofanya la kutoonekana mahakamani wakati kesi hiyo ikitajwa.
Baada ya kufutwa kwa dhamana na mshitakiwa kuwekwa mahabusu, baba yake, Bw. Charles Keenja, alikwenda kwa Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Bw. Sivangilwa Mwangesi na kumwomba kupitia upya uamuzi uliotolewa kwa madai kuwa mwanawe alikuwa amefiwa na mumewe.
Kwa mujibu wa Bw. Mwangesi, baada ya kuombwa kufanya hivyo, alikataa na kumtaka kwenda Mahakama Kuu kuwasilisha ombi hilo ili Mahakama hiyo iweze kutoa maelekezo zaidi.
Bw. Mwangesi alisema Bw. Keenja na wakili wa mshitakiwa, walikwenda Mahakama Kuu na kumwona Jaji Mfawidhi Semistokos Simon ambaye alitoa maelekezo kwa Mahakama ya Kisutu kupitia upya uamuzi wake na kumpa dhamana mshitakiwa.
"Kitu walichokuwa wanaeleza ni kuwa mshitakiwa amefiwa na mumewe na kutofika mahakamani alikuwa ameomba ingawa hakukuwa na taratibu nzuri za kuijulisha Mahakama, hivyo ndiyo sababu kubwa walizokuwa nazo," alisema Bw. Mwangesi.
Kutokana na amri hiyo, Hakimu Beda alilazimika kupitia tena uamuzi wake na kumtaka mshitakiwa kuwa na wadhamini wawili ambao watasaini dhamana ya sh. milioni 20 na kuwasilisha hati zake za kusafiria mahakamani hapo, ambapo alikamilisha masharti hayo na kuwa nje kwa dhamana.
Baada ya kumaliza hilo, Hakimu huyo alijitoa katika kesi hiyo na kuirudisha kwa Bw. Mwangesi kwa ajili ya kumpangia hakimu mwingine, ili aendelee kuisikiliza.
Mshitakiwa huyo awali aliandika barua akiiomba Mahakama kumruhusu kwenda nje ya nchi kwa ajili ya matibabu Septemba mwaka jana kwa muda wa miezi mitatu, lakini aliondoka kabla ya mahakama kutoa kibali hicho.
Kesi hiyo ina washitakiwa watatu ambao kwa pamoja wanadaiwa katika muda ambao haukujulikana wakiwa Dar es Salaam, kula njama ya kutenda makosa ya wizi wa vitu mbalimbali mali ya Raia wa China, Bibi Li Jinglan vyenye thamani ya sh. 333,300,000.
Walidaiwa kuwa Mei 9 mwaka jana Kinondoni, waliingia kwenye nyumba ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) ambayo mpangaji wake ni Bibi Jinglan wakiwa na nia ya kuiba.
Washitakiwa hao walidaiwa kuwa baada ya kuingia, waliiba mabandari 74 ya nguo, kompyuta, dola za Marekani, hereni za dhahabu, kamera na vitu mbalimbali ambavyo ni mali ya mpangaji huyo. Kesi itatajwa Aprili 8 mwaka huu.
Source: Majira
Huyu Eliaisa Keenja yupo nje ya nchi anatumbua pesa zake alizoiba, baba yake fisadi anatumia nguvu za kisiasa kumsaidia, arudi aje ajibu kesi ama mnadhani hatujui alipo?