Keenja aliharibu wapi?

Kwame Nkrumah

JF-Expert Member
Dec 2, 2008
886
376
WAKUU,
Nimekuwa ninajiuliza kila siku kwamba kati ya watendaji ambao binafsi nimefurahishwa nao katika kumbukumbu zangu ni pamoja na Charles Keenja alipokuwa Mkurugenzi wa Jiji la Dar. Huyu jamaa alifanya kazi nzuri sana kuweka jiji safi na pia kuongeza mapato ya jiji. Jambo moja{ miongoni mwa mengi ] la kukumbukwa aliloacha ni pamoja na ujenzi wa High School ya Benjamin Mkapa. Swali ni je, kwa nini Muungwana kamuacha?
Kwa mtazamo wangu ili nchi iende Watanzania wanahitaji matokeo, hamna kiongozi anayetoa matokeo sasa hivi.ni kwa nini watu wa aina ya Magufuli, Mrema au hata Njolay ,[ kwa yeye binafsi kuanzisha mikutano ya wawekezaji kuja mkoani kwake} ni nadra sana kuwapata ?Je viongozi wetu wanaogopa watu wa aina hii ?
Kwa nini basi ni watu aina ya Mohamed Seif Hatib, Nchimbi, Chiligati na wengine ambao hawana chochote wanachokifanya ndiyo wanapata madaraka?
 
Siri ya mtungi aijuaye........
Wote uliowataja wana,majamboz yao mkuu,utamu wa siasa ni kuwa iko dynamic kila kukicha, ya leo si ya jana.Chimba vizuri mzee wale wanaooneana kung'ara jana iko majamboz makubwa nyuma yao na ndo maana wenzao wanawaengua.
 
Hakuna lolote mkuu ni uleule utamaduni wa huyu mwenzetu,huyu si mwenzetu.Kama kuenguliwa kwa madhambi basi JK asingewachukua tena wakina Mramba na Chenge hata baada ya kufanya mabadiliko ya mawaziri.Inawezekana Keenja hakuwa mtandao ndiyo mana.Ikifikia viongozi wa tanzania wakachaguliwa/teuliwa kutokana na usomi,uelewa wa mambo na uchapakazi basi hata hiki kijiwe nitaacha kuja maana hakutakuwa na cha kujadili!!
 
WAKUU,
Nimekuwa ninajiuliza kila siku kwamba kati ya watendaji ambao binafsi nimefurahishwa nao katika kumbukumbu zangu ni pamoja na Charles Keenja alipokuwa Mkurugenzi wa Jiji la Dar. Huyu jamaa alifanya kazi nzuri sana kuweka jiji safi na pia kuongeza mapato ya jiji. Jambo moja{ miongoni mwa mengi ] la kukumbukwa aliloacha ni pamoja na ujenzi wa High School ya Benjamin Mkapa. Swali ni je, kwa nini Muungwana kamuacha?
Kwa mtazamo wangu ili nchi iende Watanzania wanahitaji matokeo, hamna kiongozi anayetoa matokeo sasa hivi.ni kwa nini watu wa aina ya Magufuli, Mrema au hata Njolay ,[ kwa yeye binafsi kuanzisha mikutano ya wawekezaji kuja mkoani kwake} ni nadra sana kuwapata ?Je viongozi wetu wanaogopa watu wa aina hii ?
Kwa nini basi ni watu aina ya Mohamed Seif Hatib, Nchimbi, Chiligati na wengine ambao hawana chochote wanachokifanya ndiyo wanapata madaraka?

Kwanza kutokuwemo ndani ya kundi la wanamtandao ni mojawapo ya sababu ya yeye kufungiwa mlango na JK.
Lakini pili ni kwamba, alipokuwa wizara ya kilimo na chakula enzi za mzee Nkapa aliboronga sana, hakuweza kudeliver kitu kama alivyotarajiwa. Ukumbuke kuwa utendaji wake ndani ya jiji ndio ulumletea umaarufu hadi kupata ubunge na hatimaye uwaziri.Lakini kumbe wapi bwana pale kilimo hata yeye mwenyewe anajua palimfanya kitu mbaya!!hadi wapiga kura wake wakafikia hatua ya kugoma shule ya sekondari kupewa jina lake kule mbezi!!! kwakweli mzee keenja aliporomoka ghafla na sijui kama ataweza kurudia enzi zile.
 
Ndugu yangu Mwita Matanya. Heshima kwako Mkuu.

Unachosema ni siasa ambazo umekuwa ukizisikia kutoka katika kambi mbalimbali za kampeni za 2005. Mzee Keenja hakuboronga hata kidogo alipokuwa Wizara ya Kilimo kama ulivyofanywa ufikirie. Kama unakumbuka vizuri, alipokuwa pale ndipo kwa mara ya kwanza tuliweza kuzalisha chakula kingi na cha kutosha hata kuweza kusaidia nchi zilizokuwa zikihitaji msaada, kama Zimbabwe, Malawi na Zambia. Utakumbuka wakati ule kulikuwa na harakati nyingi zaidi za wadau wa Kilimo nchini. Wafanya biashara wengi zaidi walijikita kwenye zana za Kilimo na mashamba makubwa yalianzishwa sehemu mbalimbali nchini. Mafano ni Kibaigwa (Dodoma). Watu wengi (hata ambao nawafahamu binafsi) walianza kutafuta mashamba makubwa kiasi na kulima mazao ya chakula.

Tatizo ni umuhimu wa Kilimo kwa waTanzania wakati alipokuwa akiingia kwenye Wizara ile. Utakumbuka kuwa Kilimo kilikuwa kimekufa kabisa. Na kufufua kitu kilichokufa ni kazi kubwa. WaTanzania walijikita zaidi kwenye biashara ndogondogo.

Siasa zina madhara sana. Atleast Keenja hajawahi kuwa Fisadi.
 
WAKUU,
Nimekuwa ninajiuliza kila siku kwamba kati ya watendaji ambao binafsi nimefurahishwa nao katika kumbukumbu zangu ni pamoja na Charles Keenja alipokuwa Mkurugenzi wa Jiji la Dar. Huyu jamaa alifanya kazi nzuri sana kuweka jiji safi na pia kuongeza mapato ya jiji. Jambo moja{ miongoni mwa mengi ] la kukumbukwa aliloacha ni pamoja na ujenzi wa High School ya Benjamin Mkapa. Swali ni je, kwa nini Muungwana kamuacha?
Kwa mtazamo wangu ili nchi iende Watanzania wanahitaji matokeo, hamna kiongozi anayetoa matokeo sasa hivi.ni kwa nini watu wa aina ya Magufuli, Mrema au hata Njolay ,[ kwa yeye binafsi kuanzisha mikutano ya wawekezaji kuja mkoani kwake} ni nadra sana kuwapata ?Je viongozi wetu wanaogopa watu wa aina hii ?
Kwa nini basi ni watu aina ya Mohamed Seif Hatib, Nchimbi, Chiligati na wengine ambao hawana chochote wanachokifanya ndiyo wanapata madaraka?

Kwangu mimi Mrema na Magufuli walifanikiwa sana kwenye zao.

Ukiondoa Sokoine, Mrema anafuatia kwa kutimiza kazi zake kama waziri.

Ningelikuwa waziri wa mambo ndani, kitu cha kwanza ingelikuwa kwenda kujifunza kutoka kwa Mrema.

Lakini kama tulivyo Watanzania wengi hatuwezi kusifia wenzetu wachache ambao wameonyesha uwezo mkubwa kwenye majukumu yake na badala yake tutaanza kutafuta mapungufu yao.
 
yeah the likes of mrema are the ones we always needed but ndo hivyo chema huwa hakidumu bwana, utaanza kuingilia maslahi ya wakubwa, hawapendi bwana.
 
kwa mfano mtu kama magufuli angeachwa tu pale pale ujenzi akaendeleza kazi safi kabisa za ujenzi wa bara bara pengine sasa tungekuwa na lami bara bara ya kati toka dar mwanza au mtwara mwanza kama alivyoahidi. lkn ndo wakampeleka kwenye misukosuko huko wakamvuruga kwisha habari yake, sasa anahangaika na wavuvi huko, haya bwana.
 
WAKUU,
Nimekuwa ninajiuliza kila siku kwamba kati ya watendaji ambao binafsi nimefurahishwa nao katika kumbukumbu zangu ni pamoja na Charles Keenja alipokuwa Mkurugenzi wa Jiji la Dar. Huyu jamaa alifanya kazi nzuri sana kuweka jiji safi na pia kuongeza mapato ya jiji. Jambo moja{ miongoni mwa mengi ] la kukumbukwa aliloacha ni pamoja na ujenzi wa High School ya Benjamin Mkapa. Swali ni je, kwa nini Muungwana kamuacha?
Kwa mtazamo wangu ili nchi iende Watanzania wanahitaji matokeo, hamna kiongozi anayetoa matokeo sasa hivi.ni kwa nini watu wa aina ya Magufuli, Mrema au hata Njolay ,[ kwa yeye binafsi kuanzisha mikutano ya wawekezaji kuja mkoani kwake} ni nadra sana kuwapata ?Je viongozi wetu wanaogopa watu wa aina hii ?
Kwa nini basi ni watu aina ya Mohamed Seif Hatib, Nchimbi, Chiligati na wengine ambao hawana chochote wanachokifanya ndiyo wanapata madaraka?

Kwame...Maslahi ya chama kwanza na mengine ndiyo baadaye...Unaweza kuona pia kuwa usalama wa Taifa ni usalama wa vigogo wa chama tawala ambao chama kimekuwa kama genge na Taifa victims.
 
WAKUU,
Nimekuwa ninajiuliza kila siku kwamba kati ya watendaji ambao binafsi nimefurahishwa nao katika kumbukumbu zangu ni pamoja na Charles Keenja alipokuwa Mkurugenzi wa Jiji la Dar. Huyu jamaa alifanya kazi nzuri sana kuweka jiji safi na pia kuongeza mapato ya jiji. Jambo moja{ miongoni mwa mengi ] la kukumbukwa aliloacha ni pamoja na ujenzi wa High School ya Benjamin Mkapa. Swali ni je, kwa nini Muungwana kamuacha?
Kwa mtazamo wangu ili nchi iende Watanzania wanahitaji matokeo, hamna kiongozi anayetoa matokeo sasa hivi.ni kwa nini watu wa aina ya Magufuli, Mrema au hata Njolay ,[ kwa yeye binafsi kuanzisha mikutano ya wawekezaji kuja mkoani kwake} ni nadra sana kuwapata ?Je viongozi wetu wanaogopa watu wa aina hii ?
Kwa nini basi ni watu aina ya Mohamed Seif Hatib, Nchimbi, Chiligati na wengine ambao hawana chochote wanachokifanya ndiyo wanapata madaraka?

kwame nkrumah!
Kuna maneno mazuri sana ambayo aliyekuwa waziri mukuu wa Uingereza Tony Blair aliyoyasema alipokuwa anamaliza kipindi chake. Kwa ufupi alisema naondoka kwenye huu wadhifa wa uwaziri mkuu huki nikijivuna kwa sababu nimeweza kujenga jamii ambayo mchapakazi huona matunda ya uchapakazi wake na mvivu huona matokeo ya uvivu wake.
Hii ni jamii tofauti na ambayo sisi Watanzania tumeijenga kwa sababu kwetu wasio wachapa kazi na wanafiki ndio wanapendwa na kusifiwa na wachape kazi na wasema kweli wanapata maadui. Fanya marejeo kwa watu kama Nape
Nnauye, Makamba, Nchimbi, Mwakyembe, Mama Kilango, Rostam Aziz na hata JK mwenyewe jiuliza alishinda kwa 80% alikuwa amefanya nini cha maana?
 
Kwangu mimi Mrema na Magufuli walifanikiwa sana kwenye zao.

Ukiondoa Sokoine, Mrema anafuatia kwa kutimiza kazi zake kama waziri.

Ningelikuwa waziri wa mambo ndani, kitu cha kwanza ingelikuwa kwenda kujifunza kutoka kwa Mrema.

Lakini kama tulivyo Watanzania wengi hatuwezi kusifia wenzetu wachache ambao wameonyesha uwezo mkubwa kwenye majukumu yake na badala yake tutaanza kutafuta mapungufu yao.

mrema is one person who can stand and talk against whatever he doesnt believe infront of millions. We really need this man back, now anawezekana akawa mzee kidogo ila he is kind of person Tanzania really need. Mtu wa watu, anayeweza kumsema ata rais kama akiona anatenda vibaya
 
Nafikiri pia uwoga wa viongozi wetu kwamba fulani asiwe maarufu "kuliko mimi" inachangia. Najua vijana wengi wanarudi nyumbani kwa moyo na nia ya kweli ya kujenga nchi lakini wakifika nyumbani wanaambiwa "kijana taratibu, nchi hii ina wenyewe".
Lakini pia watu hao waadilifu ni wagumu kutoa rushwa na ku- "kiss ass"- ili wawe kwenye system,hii inawaangusha sana, na zaidi zaidi sisi wananchi ndio tuliwao. Kenya wana system ya kura ya maoni kwa mawaziri, wabunge, RCs na Ma DC kwamba nani anafanya kazi nzuri na nani hafanyi kazi aliyotumwa, ingependeza sana kupata scores za mawaziri wetu. I wonder nani angekuwa kinara !!
 
Hakuna lolote mkuu ni uleule utamaduni wa huyu mwenzetu,huyu si mwenzetu.Kama kuenguliwa kwa madhambi basi JK asingewachukua tena wakina Mramba na Chenge hata baada ya kufanya mabadiliko ya mawaziri.Inawezekana Keenja hakuwa mtandao ndiyo mana.Ikifikia viongozi wa tanzania wakachaguliwa/teuliwa kutokana na usomi,uelewa wa mambo na uchapakazi basi hata hiki kijiwe nitaacha kuja maana hakutakuwa na cha kujadili!!

Mkuu Mtarajiwa ni kweli kabisa kuna dhana ya mwenzetu katika uongozi wa nchi yetu, lakini nayo ni subjective.Kuna wenzetu na wenzetu zaidi.Kuna wanamtandao halisi, kuna wanamtandao maslahi ...nakadhalika
Na ndio nikasema ya leo si ya jana,ukijua huu wenzio wanajua ulee hata kati ya hao wenzetu.
Siyo siri kuwa kwa sasa hivi Mramba na Chenge are a political liability.Na katika chama tawala kuna vikundi vingi vyenye kuongozwa na malengo mbalimbali, wanachoweza kujivunia ni ingalao utamaduni wa kukutana rasmi.Hata hivyo vilevile siyo siri juu ya ugomvi wa mheshimiwa uliyemtaja alipokuwa waziri na kigogo mmoja wa chama tawala
 
- Keenja, aliharibu Kilimo sana tena sana under Mkapa na kule City alileta hasara kubwa sana kwa walipa kodi, ingawa alifanya kazi kubwa sana kusafisha jiji na kulibadilisha to the better, hilo halina ubishi na wala sio siri,

- Tatizo lilikuja pale serikali ilipompeleka kwa makusudi mtu wao Mkama kuchukua nafasi yake kule City, ndipo noma yake ilipoanzia kugundulika, infact kama sio kuwa mume mwenza na Sumaye, Keenja angekua wa kwanza kuburuzwa Kisutu, kutokana na ubadhirifu mkubwa na wa ajabu alioufanya City na mpaka leo haujasemwa wazi to the public, ulizimwa kwa kua ni mwenzetu.

- Mengineyo, ni kutokuwa mtandao na kuwa kampeni manager wa urais kambi ya Sumaye a sworn enemy wa mtandao, halafu ubunge wake pia nao ni wa utatanishi sana, otherwise binafsi nina tatizo sana na kiongozi ambaye akiondoka sekta fulani basi the whole system ya uongozi ina fall apart kama huyu mkuu alipotoka tu City, kila kitu kikaanguka chini, nina wasi wasi sana na viongozi wa namna hii kwamba ni me first! na hawa-delegate power kwa wengine katika maamuzi muhimu wanapokuwa kwenye hizi sekta za taifa ili siku zote wafuatwe wao tu! ndio maana ninaiheshimu sana tabia moja ya muungwana, kwamba kiongozi akimaliza muda tu hakuna kuongeza.
 
Mkuu FMES
Sishangai, maana hata yeye Muungwana anajua hakuna kuongeza, so jicho kwa jicho. Unafikiri angejihakikishia mambo kama ya Guinea Conakry, Libya au Kameruni angewaza hayo?
 
Mkuu Mwalimu Zawadi,

- Heshima mbele, sina uhakika na yeye muungwana na term ya pili, lakini lazima sometimes tumpe credit, hivi umegundua kuwa yale mambo ya kutoka kuharibu uwaziri na kuwa balozi na RC sasa hakuna tena?

- Ingekuwa zamani saa hizi ungesikia Ngasongwa, Meghji, Mungai, Rita Mlaki, Mangula wamekua mabalozi na ma-RC, safari hii hakuna tena saafi sana, ikiiihsa zamu yako umeharibu basi ni zamu ya wengine sasa.

- Ila yeye ana kazi sana maana the Lowassa's people, wanadai piga ua wanarudi sasa sijui itakuwaje, tunasubiri tu kuona!
 
Field Marshal ES

"otherwise binafsi nina tatizo sana na kiongozi ambaye akiondoka sekta fulani basi the whole system ya uongozi ina fall apart kama huyu mkuu alipotoka tu City, kila kitu kikaanguka chini."

Unajua kwa nini mtu kama huyo anapoondoka nafasi inapwaya? ni kwa sababu mtu anayefuatia hajui kazi. Unakumbuka Mrema alipokuwa mambo ya ndani? alijiwekea lengo kwamba Tanzania ina sheria 1400, na lengo lake ni kwamba sheria zote zifanye kazi, na alikuwa kweli anahakikisha hivyo, lakini alipoondoka yeye akaja Nyanda kama sikosei,hatukusikia kitu. Mrema akatolewa hapo akaenda Wizara ya Kazi kila mtu alijua umuhimu wa wizara hiyo baada ya Mrema kwenda huko. Lakini what happened baada ya yeye kuondoka ?Mimi naona siyo suala la umimi tena, ni suala la nani anafanya kazi kumfikia aliyepita ? Point yangu ni kwamba hakuna RESULTS, utundu na ubunifu hamna, kukubali majukumu hamna, kuwa tayari kubeba lawama hamna. Je si kweli mji ulipendeza wakati wa Keenja? Mapato hayakuongezeka baada ya yeye kuingia madarakani ? Nakumbuka mpaka kwetu Kigilagila kulikuwa na trash collection every Tuesday.
Lakini pia Mkuu umenielewesha mambo mengi sana nilikuwa sijui km kuwa alikuwa Chair wa failed Sumaye bid !! heshima mbele.
 
WAKUU,
Nimekuwa ninajiuliza kila siku kwamba kati ya watendaji ambao binafsi nimefurahishwa nao katika kumbukumbu zangu ni pamoja na Charles Keenja alipokuwa Mkurugenzi wa Jiji la Dar. Huyu jamaa alifanya kazi nzuri sana kuweka jiji safi na pia kuongeza mapato ya jiji. Jambo moja{ miongoni mwa mengi ] la kukumbukwa aliloacha ni pamoja na ujenzi wa High School ya Benjamin Mkapa. Swali ni je, kwa nini Muungwana kamuacha?
Kwa mtazamo wangu ili nchi iende Watanzania wanahitaji matokeo, hamna kiongozi anayetoa matokeo sasa hivi.ni kwa nini watu wa aina ya Magufuli, Mrema au hata Njolay ,[ kwa yeye binafsi kuanzisha mikutano ya wawekezaji kuja mkoani kwake} ni nadra sana kuwapata ?Je viongozi wetu wanaogopa watu wa aina hii ?
Kwa nini basi ni watu aina ya Mohamed Seif Hatib, Nchimbi, Chiligati na wengine ambao hawana chochote wanachokifanya ndiyo wanapata madaraka?

Alikuwa ni Mshamba NUMBER ONE. Alipokuwa katika jiji alifanya kazi sio kwa maslahi ya wakazi bali kupata sifa za kupanda vyeo.

Kuonyesha ushamba wake. Mji wowote ni lazima uwe na sehemu za kupumzikia au viwanja vya michezo. Kuchukua viwanja vya uhuru na sehemu za kupumzikia na kujenga shule ya sekondari ni kutotumia akili. Lakini alifanya hivyo kutaka kuonyesha kuwa kazi anaijua.

Pili nafasi yake ilikuwa imevunja katiba. Waziri mkuu hawezi kuvunja serikali ya mitaa kwa sababu imeshindwa kufanya kazi ya kusafisha mji. Madiwani ni watu waliochaguliwa kwa kura za wananchi. Na ni wajibu wa wananchi kutumia demokrasia kuwaondoa wasiofaa.
 
- Keenja, aliharibu Kilimo sana tena sana under Mkapa na kule City alileta hasara kubwa sana kwa walipa kodi, ingawa alifanya kazi kubwa sana kusafisha jiji na kulibadilisha to the better, hilo halina ubishi na wala sio siri,

- Tatizo lilikuja pale serikali ilipompeleka kwa makusudi mtu wao Mkama kuchukua nafasi yake kule City, ndipo noma yake ilipoanzia kugundulika, infact kama sio kuwa mume mwenza na Sumaye, Keenja angekua wa kwanza kuburuzwa Kisutu, kutokana na ubadhirifu mkubwa na wa ajabu alioufanya City na mpaka leo haujasemwa wazi to the public, ulizimwa kwa kua ni mwenzetu.

- Mengineyo, ni kutokuwa mtandao na kuwa kampeni manager wa urais kambi ya Sumaye a sworn enemy wa mtandao, halafu ubunge wake pia nao ni wa utatanishi sana, otherwise binafsi nina tatizo sana na kiongozi ambaye akiondoka sekta fulani basi the whole system ya uongozi ina fall apart kama huyu mkuu alipotoka tu City, kila kitu kikaanguka chini, nina wasi wasi sana na viongozi wa namna hii kwamba ni me first! na hawa-delegate power kwa wengine katika maamuzi muhimu wanapokuwa kwenye hizi sekta za taifa ili siku zote wafuatwe wao tu! ndio maana ninaiheshimu sana tabia moja ya muungwana, kwamba kiongozi akimaliza muda tu hakuna kuongeza.

Mkuu FMES sikubaliani na wewe kabisa katika tathmini yako. Unaweza kutoa kwa uwazi kabisa ni kiasi gani cha hasara au ni kivipi hasara hiyo unayoisema ilisababishwa na Keenja alipokuwa Jiji? Keenja alipoingia Jiji, alikuta mapato yanayokusanywa kwa mwaka yasiyozidi shilingi milioni 800. Alikaa miaka miwili na nusu, na kubuni njia nyingi za mapato pamoja na kuboresha ukusanyaji hadi kufikia Bilioni 3 kwa mwaka, na katika kipindi kifupi sana. Kama unakumbuka, dhumuni la kuundwa kwa Tume y Jiji ni kuweka system mpya ya utendaji. Municipal tatu ziliundwa ili kuongeza utendaji na kuboresha mapato. System unayosema ilisambaratika sijui ni ipi. Waliobadilika ni viongozi na kila mtu ana uwezo wake na malengo yake kiutendaji.

Mkuu ndugu Mkama aliwahi kujisifia katika mkutano na wazee wa Dar, kuwa Jiji ni safi kuliko wakati wa Tume na kuwa Tume haikufanya lolote la kusifiwa. Alizomewa na wazee wale.

Keenja sio Mume mwenza wa Sumaye. Inaonyesha jinsi usivyokuwa na ukweli wowote kuhusu mtu unaemzungumzia.

Haiwezekani kwa mtu mmoja kufanya mambo peke yake, na yakaleta mabadiliko makubwa kama ilivyokuwa kwa Tume ya Jiji. Jiji wakati ule liliongozwa kwa "Team Work" na hiyo ndio siri ya mafanikio yao. System katika nchi hii haiko sawa. Huwa inategemea sana uwezo na jitihada za kiongozi binafsi. Kama kiongozi huyo ni bogus, mambo huaribika, na/ au akifuatiwa na kiongozi asie na uwezo, huwa mambo huharibika pia.

Kumbuka hakukuwa na Madiwani wakati ule, na Tume ilipewa nguvu kubwa ya kuamua na kutekeleza. Hivyo ilikuwa rahisi kutekeleza bila kuingiliwa na siasa za kuyumbishana. Ilibidi waondoke ili kuwezesha wanasiasa kufanya wanayotaka. Na hayo ndio unayoita usambaratikaji wa System.
 
Aisee usiombe kufanya kazi na huyu jamaa.He is too authoritarian,yaani hana hekima katika utendaji wake kabisa,halafu ni mdhalilishaji mkubwa wa watu.Mmmmm,usiombe!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom