Keenja akanusha vikali tuhuma za kununua jimbo la Ubungo 2005 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Keenja akanusha vikali tuhuma za kununua jimbo la Ubungo 2005

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by AMARIDONG, Oct 23, 2010.

 1. AMARIDONG

  AMARIDONG JF-Expert Member

  #1
  Oct 23, 2010
  Joined: Jun 24, 2010
  Messages: 2,506
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 0
  Akionyesha kumuunga mkono mgombea wa CHADEMA Ubungo (John John Mnyika), waziri wa zamani na mbunge wa Ubungo Mh Keenja amesikitishwa na habari ya kuwa alinunua jimbo la Ubungo akiwa maeneo ya Marangu Mtoni.

  Ndugu Keenja amesikika akisema "Kuna uwezekano kwamba Mnyika alishinda 2005 lakini tume ndio iliyotangaza matokeo sio mimi, ni kweli kuwa John anakubalika sana hasa na vijana ambao ni wengi pale Ubungo na lolote linawezekana kwani nimesikia hata wazee na kina mama wanamkubali sana siku hizi na nasikia amefanya kazi za kibunge japo hakuwa bungeni"

  Keenja ameendelea kuonya kuwa ni hatari kwa wananchi kuanza kujenga chuki kwa wagombea kwa kuwasingizia mambo ya uongo ambayo mengi ni tuhuma zisizodhibitika, uzushi na udanganyifu.

  Nionavyo huyu bwana keshapima upepo na anajua mbunge ajaye Ubungo!

  Chagua CHADEMA, Chagua Mnyika mbunge, Slaa rais.
   
 2. Superman

  Superman JF-Expert Member

  #2
  Oct 23, 2010
  Joined: Mar 31, 2007
  Messages: 5,702
  Likes Received: 97
  Trophy Points: 145
  Source?
   
 3. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #3
  Oct 23, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Nina mashaka na hii habari!

  Nakumbuka ya Tunduma kama yalivyowasilishwa na huyu MTOTO WA MKULIMA pamoja na mwenzake wa 16!
  "Matumoki Doyi"...(najisemea Kimaasai)
   
Loading...