Eeka Mangi
JF-Expert Member
- Jul 27, 2008
- 3,173
- 481
KCMC hospitali kubwa inayotegemewa kutoa huduma za hali ya juu lakini ina wafanyakazi bomu kabisa.
Nilikwenda pale leo kupata huduma. Nikapata maelekezo kuwa niweke kadi yangu ili wakatafute faili langu lilipo. Yule mhudumu akatuelekeza tuende pahali pa kulipia hayp mafaili. Nilikaa kwa muda wa saa moja, sikusikia jina langu likiitwa.
Nilirudi pale mapokezi nikakuta kadi yangu iko palepale nilikoambiwa niiweke. Nikauliza kulikoni nikajibiwa nikae kwenye benchi nisubiri. Nikamwambia yule dada kuwa nimekaa zaidi ya saa moja sasa kusubiri faili langu liletwe. Akanishangaa na kuanza kuniambia kuwa mimi ni mwongo. Baada ya majibizano ya muda yule dada akanambia nisimfundishe kazi!
Ilibidi nimwonye kuwa yeye ni mhudumu na ni haki ya mteja kupata huduma kwa wakati. Alituacha pale mapokezi na kurudi nyuma ya meza akaanza kuhangaika na laptop yake pale.
Kusema ukweli tulikaa sana hadi sita na nusu. Doctor wangu baada ya kutokuniona alinipigia simu kujua kulikoni. Nikamweleza yaliyotokea ilibidi aende kutafuta faili na kuja kunitibia ingawa sikufanikiwa kupata vipimo vyote.
Hivi jamani hawa wahudumu wa kutunza kumbukumbu wao ni nani na ni nini kinawapa jeuri kiasi cha kuona wateje/wagonjwa kama takataka fulani hivi? KCMC they need to do something about this!