Uncle Jei Jei
JF-Expert Member
- Jan 7, 2011
- 1,684
- 2,157
hapa Kazi tu ni kauli mbiu mashuhuri hapa Tanzania. Muasisi wa kauli mbiu hiyo anasisitiza tufanye kazi tu yeye shida zetu zoooooooote anazijua! Hana haja ya kuelekezwa kwasababu anazijua, hana haja ya kuambiwa kwa sababu anazijua tayari, hana haja na maoni yenu kwasababu anayo yake tayari jinsi gani atazitatua, hana haja mfanye mikutano ya kumsaidia kuelemisha watu namna gani ya kuhakikisha viongozi wao wanatenda haki kwasababu yeye anatosha kuwadhibiti wote, hahitaji makongamano labda ya kumtukuza tu tofauti na hapo huenda mkapotosha anachokilenga yeye, hamna haja hata ya kutoa michango yenu bungeni, kwenye magazeti, redioni wala mitandaoni mtarudisha juhudi zake nyuma baaaaaana! Mbona hamuelewi!?! Hahahaaaaa!kusoma hamjui hata picha nayo hamuoni!? Hahahaaaaa!! Au picha ngumu kutafsiri mithili ya katuni za masoud kipanya!!!! Hehe hehe! Watanzania bwauna! Au nyie sio watanzania!? Mbona watanzania wameshaelekezwa cha kufanya!!! Mnashangaa nini sasa!? Chadema/ukawa kuzuiliwa maandamano na mihadhara!!? Hao hawajakatazwaaa!!!!!.... Wanakumbushwa kazi yao waliyopewa watanzania wote!! Si nyinyi mmeambiwa mkazane KUOMBA!? Sasa labda mkafanye maandamano, makongamano na mihadhara ya maombi tu!? Ndio kazi ya watanzania juu ya utawala huu. No more!! Hahaha! Eti mahakamani, mbona hata wao wako bize na KUMUOMBEA!!? He he he eti bungeni, mbona na wao wako bize na KUMUOMBEA!?! Duuuuuuh eti redioni, TV, mitandaoni!! Hata wao ni watanzania wameitikia wito huo huo. Sasa wewe thubutu kwenda kinyume nyume uone!! Hatuchangi million 7 saba za kukugomboa!!! Karaga baho!