Kazi zenye pesa zisizojadiliwa na vijana hizi hapa

Natumai hamjambo, kichwa Cha habari kinajieleza, Kuna kazi vijana wengi hawazijadili ila ukizizingatia unaweza ukatengeneza kampuni kubwa Tena yenye kuheshimika

1; Shoe care, hi inajumuisha kushona viatu vilivyochanika, mikoba, begi, nk, kung'arisha viatu na kufua viatu, Hakika, kwa mtaji wa elfu 50 unaheshimika mtaani na familia pia, Mimi nipo naifanya hii, sema nipo kijijini, natamani nipate mtu wa kuungana nae sehemu ya mjini, kwa siku huwa sikosi elf 7

2. Ku repair viti vya plastic na vombo vyote vitokanavyo na plastic. Hapa ukitaka utajirike haraka, tafuta eneo la kuhifadhia bidhaa za wateja wako, pia uwe na electronic drill nyembamba na zile waya laini zakwenye transformer za redio au hata wire mesh lain kwa kushonea viti, nakwambia wateja utawakataa, hili wazo nalifanyia kazi sema Sina nakosa mtu wa kuungana nae ili tuwe tunakimbiza kazi hiyo haraka

3. Kuchimba vyoo, na kutapisha vyoo. Kuchimba shimo la choo, futi inagharimu Tsh 7000 mpaka elf 10000 Sasa ukiwa na bidii, ukachimba futi 5 kwa siku, utalala njaa? Hapa kinachotakiwa, ili mheshimike, mnakuwa na ofsi yenu yenye bango kubwa likisema, TUNACHIMBA VYOO NA KUTAPISHA VYOO VILIVYOJAA KWA BEI RAHISI. Mnaweka na mawasiliano, kwasababu nyie Ni kampuni, mkipata kazi, mnagawanya majukumu, yaani Kama wanavyofanya kazi TANROAD na TANESCO. Hapa kampuni yenu itaheshimika na hakuna mtu wa kuwadhalau/ kuwakejeri

4. Kutengeneza vifàa vya michezo ya watoto. Mfano, gari zitokanazo na spoku za baiskeli/ pikipiki, gari za mabox na yeboyebe/ slippers, kuchonga puzzles kwa kutumia slippers, na vitu vingine vinavyovutia watoto. Nakwambia, wateja wapo hasa shule za English medium, pia mnatakiwa muwe kampuni ili bidhaa zenu ziwe na label kuzifanya ziheshimike zaidi. Kea atakaye penda mawazo yangu anataka tushirikiane, tafadhari njoo PM/ INBOX tujadiliane. Kwa mwenye pesa ila amependa mawazo haya/ wazo mojawapo, anaweza akatuunganisha vijana tutakaokuwa tayari ili tujikwamue zaidi.

Note: UOGA WAKO NDIYO UMASIKINI WAKO
Kuna jamaa ni foreigner alikuwa kaoa mtanzania sema akamgeuka akamtimua na kumdhurumu kila kitu. Na alimtimua kipindi amabacho alikuwa anaumwa amegeuka kuwa kipofu. Foreigner mwenzake akamchukua kaanza ishi naye wanahangaika makanisani kwa mwaka mzima jamaa akaanza ona. Akapata ela kanisani akaanza shona viatu akapanga chumba, yule mwenzake akawa analalamika kuwa jamaa anawaibisha bora hata hiyo kazi angeenda kuifanya mtaa wa mbali.
Jamaa ni msafi, anafika ofisini kwake saa 12 unakuta anafanya usafi.
Ni mwaka wa pili sasa, ofisi kaipanua now ana frem, amenunua machine ya kushona cover za viti, viatu vya kimasai, anashona vitu kibao, anauza viatu na sole kwa wingi. ameajiri vijana wengine.
Kweli maisha ni malengo hata yule aliyekuwa anamcheka kakili kuwa alikuwa anakosea.
 
Safi kabisa,dhana ya ujasiriamali inaendana na usafi pamoja na kujali muda kitu ambacho watu wengi tunakipuuzia,ukifanikiwa hili biashara yeyote unatoboa hata ya mtaji mdogo kiasi gani.
 
Back
Top Bottom