Kazi za Tutorial Assistants, Lecturers, Associate Professors na Professors wameishaitwa UDOM?

rwosile

Member
Oct 4, 2011
7
0
Wapendwa wa Jamii Forums, naomba mnifahamishe kama wale waliomba nafasi za kazi za kufundisha UDOM yaani kazi za TUTORIAL ASSISTANTS,
LECTURERS, ASSOCIATE PROFESSORS NA PROFESSORS, je, wameishaitwa kwenye usaili au bado maana muda ni mrefu. Kazi zilitangazwa mwezi wa
Mei, 2011 na wakati wale waliomba mwezi wa Agosti tayari wameishaitwa kwenda kwenye usaili. Nauliza maana ninafatilia lakini sijaona tangazo la kuwaita na wakipigiwa simu majibu hayaeleweki mara wasiliana na watu wa HR wakati namba
zao za simu hazijulikani.
 
Mkuu pole,walikwisha waita na wameanza kazi muda kidogo,tangu miezi miwili iliyopita....kuna jamaa yangu kaanza kazi pale chuo cha elimu.
 
Mimi nilifanya interview mwishoni mwa mwezi July, nikaitwa kuripoti September ili nifundishe ila bado sijawasili. Nilipigiwa simu siku 3 kabla ya interview. Ila nadhani pia inategemea na Collage
 
mkuu umejichanganya sana ktk hii post yako. yaani umeenda mbele then ukarudi nyuma, mithili ya kifurugobe!
 
Ukiona hivyo ujue wamekumwaga jaribu chuo kingine...

Kuna mwana JF alisema kama unaomba kazi UDOM jitahidi kuweka jina la kiislam la uongo eti watakuita fasta bila kauzibe
 
Ukiona hivyo ujue wamekumwaga jaribu chuo kingine...<br>
<br>
Kuna mwana JF alisema kama unaomba kazi UDOM jitahidi kuweka jina la kiislam la uongo eti watakuita fasta bila kauzibe
<br>Acha hizo sielewi ni vigezo gani wanafuata lkn kuna jamaa sifa anazo na ni muislam na hajaitwa hata mara moja na ameomba mara nyingi lkn bila ya mafanikio jaribu tena,kama afanyavyo labda kuna kipindi wakihitaji tena watu utaitwa.kuna kipindi walienda hata kurecruiti watu India na kenya na wakaacha watanzania nafikiri hili lilikaa kipadiemu zaidi na mengine sijajui.Usikate tamaa,jaribu tena ndugu yangu!
 
kuna dadangu aliomba post ya hr manager, nadhani interview ni jumamosi ya kesho!
 
jamani huko UDOM kuna ubabaishaji kupita kiasi, nimeomba mara mbili bila majibu na kati ya hizo mojawapo nilipeleka na kukabidhi barua mimi mweyewe, cha ajabu nilipofuatilia baada ya muda mrefu kwa kutumia mtu niliyemfahamu too late ilionekana katika barua zilizopokelewa yangu haikuwepo, hii ina maana haikuwa registered. hawa jamaa wanatupa barua za watu ili jamaa zao wenye sifa dhaifu wapate kwani kuna wakati walichukua hadi GPA 3.5 wakati mimi nilikuwa na GPA 4 sikuonekana. KAAMA UNA NDUGU MWENYE WADHIFA, I ASURE YOU WILL GET A JOB. Tafakari nchi inapokwenda na uchakachuaji huu ktk taaluma
 
Mimi nilifanya interview mwishoni mwa mwezi July, nikaitwa kuripoti September ili nifundishe ila bado sijawasili. Nilipigiwa simu siku 3 kabla ya interview. Ila nadhani pia inategemea na Collage

Collage? Huyu ndio mwalimu mtarajiwa pale Udom,tunategemea graduate wake watakuaje? Looh!
 
Mimi nilifanya ile interview ya mwezi July kwenye College of Health and Allied Sciences. Mwezi huohuo (July), kuna rafiki yangu alifanya interview kwenye school of natural sciences na tayari alisahitwa kuanza kazi mwishoni mwa mwezi Sept . Kwa kifupi kama mpaka leo hujaitwa ujue umeikosa, endelea kutafuta kwingine kwani lazima ufanye kazi UDOM?.
 
Mimi nilifanya interview mwishoni mwa mwezi July, nikaitwa kuripoti September ili nifundishe ila bado sijawasili. Nilipigiwa simu siku 3 kabla ya interview. Ila nadhani pia inategemea na Collage

tatizo la muogo ni kwamba memory yake inakuwa na mambo mengi yasiyotimia.muongo hana kumbukumbu
 
Mimi nilifanya ile interview ya mwezi July kwenye College of Health and Allied Sciences. Mwezi huohuo (July), kuna rafiki yangu alifanya interview kwenye school of natural sciences na tayari alisahitwa kuanza kazi mwishoni mwa mwezi Sept . Kwa kifupi kama mpaka leo hujaitwa ujue umeikosa, endelea kutafuta kwingine kwani lazima ufanye kazi UDOM?.

we mwenyewe vp mbona unamsemeha mwenzako aliitwa mwez sept instead of nimeanza kazi mwez sept
 
Sijaitwa, kwa hiyo najihesabia nimeikosa ndo maana nikamtumia rafiki yangu kama reference kuwataarifu wanaoendelea kusuburi kuitwa watambue kuwa tayari watu wanakula mshahara. Nisamehe kama sijaeleweka.
 
Back
Top Bottom